Mjukuu wa Sechenga
Member
- Nov 13, 2015
- 34
- 37
Kutokana na spidi aliyoanza nayo Mh JPM ni wazi kwamba nguvu ya chama kikubwa cha upinzani kitafifia na kupotea midomoni mwa watu kutokana na sababu mbalimbali.
Ni ukweli usiopingika kuwa JPM ndani ya siku 100 ameweza kuonesha muelekeo mzuri kwa wananchi ambapo utafiti uliofanywa unaonesha wananchi kwasasa wanamkubali zaidi Magufuli kuliko aliyekuwa mgombea wa chama pinzani ndugu Edward Lowassa.
Zipo sababu ambazo zitapelekea kufifia na kufa kwa nguvu yake ya upinzani;
1. Spidi ya JPM
Tangu raisi aingie madarakani amekuwa akijibu hoja nyingi ambazo wapinzani walikuwa wakizipigia kelele. Hivyo uwepo wa Magufuli kwa sasa umefanya watanzania waamini kuwa mabadiliko yanaweza kufanyika hata ndani ya CCM hivyo miaka ijayo ni wazi kuwa watanzania hawataona haja ya kuijaribu upinzani ilhali wanapata majibu ya maswali yao kutoka kwa CCM.
2. Wapinzani kujenga hoja nyepesi
Wimbo mkuu wa upinzani hauchezeki kwa sasa hasa baada ya Magufuli kuingia ikulu, hoja nyingi za wapinzani kwa sasa hazina nguvu, mfano wanapokuja kusema kwanini rais Magufuli hataki kusafiri nje ya nchi ni hoja ya kuchekesha sana wakati haohao walikuwa wa kwanza kukemea safari za nje za aliyekuwa raisi wa awamu ya nne ila leo hii wanabadilika.
Hizo ni baadhi tu ya sababu na najua zipo nyingi ila amini usiamini CHADEMA itakufa kabla ya uchaguzi ujao.