CHADEMA itakufa kabla ya uchaguzi ujao

CHADEMA itakufa kabla ya uchaguzi ujao

Mawazo yako mjukuu hayafai kabisa kwenye jamii ya sasa. Mtaka maendeleo wa aina yeyote hawezi kuchekelea upinzani unapokosa nguvu katika nchi yoyote. Mpinzani ni yule anayekuonyesha ni wapi unakosea. Kwa sasa upinzani umenyamaza kwa kuwa mambo sio mabaya sana. Tuombe upinzani uongezeke nguvu ili tip are maendeleo
 
Waswahili husema mwanzo mgumu lakini jpm ni kama anaona kutumbua majipu ni jambo rahisi. Mimi nina mashaka makubwa
 
Kutokana na spidi aliyoanza nayo Mh JPM ni wazi kwamba nguvu ya chama kikubwa cha upinzani kitafifia na kupotea midomoni mwa watu kutokana na sababu mbalimbali.

Ni ukweli usiopingika kuwa JPM ndani ya siku 100 ameweza kuonesha muelekeo mzuri kwa wananchi ambapo utafiti uliofanywa unaonesha wananchi kwasasa wanamkubali zaidi Magufuli kuliko aliyekuwa mgombea wa chama pinzani ndugu Edward Lowassa.

Zipo sababu ambazo zitapelekea kufifia na kufa kwa nguvu yake ya upinzani;

1. Spidi ya JPM
Tangu raisi aingie madarakani amekuwa akijibu hoja nyingi ambazo wapinzani walikuwa wakizipigia kelele. Hivyo uwepo wa Magufuli kwa sasa umefanya watanzania waamini kuwa mabadiliko yanaweza kufanyika hata ndani ya CCM hivyo miaka ijayo ni wazi kuwa watanzania hawataona haja ya kuijaribu upinzani ilhali wanapata majibu ya maswali yao kutoka kwa CCM.

2. Wapinzani kujenga hoja nyepesi
Wimbo mkuu wa upinzani hauchezeki kwa sasa hasa baada ya Magufuli kuingia ikulu, hoja nyingi za wapinzani kwa sasa hazina nguvu, mfano wanapokuja kusema kwanini rais Magufuli hataki kusafiri nje ya nchi ni hoja ya kuchekesha sana wakati haohao walikuwa wa kwanza kukemea safari za nje za aliyekuwa raisi wa awamu ya nne ila leo hii wanabadilika.

Hizo ni baadhi tu ya sababu na najua zipo nyingi ila amini usiamini CHADEMA itakufa kabla ya uchaguzi ujao.

Heading ya mada yako... "CHADEMA itakufa........" na ndani ya habari ".....ITAFIFIA NGUVU..."

Hii inaonesha hata wewe mwenyewe hujui wala hukiamini kile ulichokiandika na kupost hapa!!

Eti kila anayemkosoa JPM na staili ya utendaji wake ni CHADEMA!

Lol ni upuuzi uliovuka mipaka na kukosa kufikiri vizuri na pia inaonesha hofu yenu dhidi ya CHADEMA/UKAWA!!

Haitakufa wala kufifia ng'o isipokuwa ndiyo ita - gain strength mara 100 ktk kipindi cha huyu ndugu yenu kwani ushahidi unaonesha dhahiri hivyo kuwa tangu ianzishwe haijawahi kupungua wala kufifia nguvu zake!

Mwenzenu Steven Wassira marehemu wa kisiasa (apumzike kwa amani huko aliko) aliwahi kuipa mwaka mmoja CHADEMA kuwa itakuwa imekufa, natokeo yake kafa yeye. Na wewe angalia uta rest in peace shauri lako ooooh!!

Kwa hiyo hebu jipange vizuri na leta mambo ya maana hapa
 
Back
Top Bottom