Mkuu huu utetezi nimeanza kuusikia zaidi ya 8yrs sasa. Kwamba kila wakati utetezi huwa ni kwamba mazingira hayaruhusu, tusipoangalia anaweza kukaa miaka 30 kwa kisingizio cha hali iliyopo hairuhusu. Kwa mfano sasa Magufuli atakaa 10 yrs madarakani, ni dhahiri Magufuli sio rafiki wa demokrasia, hiyo pekee inaweza kumfanya Mbowe akae madarakani zaidi ya 25yrs kwa kisingizio cha hali hairuhusu.
Tuje kwenye uhalisia, mpaka sasa Mbowe ni mwenyekiti lakini wabunge na madiwani wengi wameondoka kwa kununuliwa, chaguzi zote zinaendeshwa kibabe huku chama kikiporwa kura kiwaziwazi na wala haendi mahakamani kama ameshindwa kuitisha nguvu ya umma. Juzi mbunge wake amefutwa ubunge huku yeye na uongozi wa chama ukiwa hauna taarifa za mahudhurio yake huko bungeni. Ofisi ya chama ambayo kila siku tunatukanwa hapa jukwaani iko vile vile, hata huyo Lowassa aliyepokelewa na kusifiwa ni tajiri alikuwa haendi hapo ofisini kwamba haina hadhi, Mbowe alishindwa hata kumshawishi ajenge ofisi ya below 500m? Hakuna matawi mapya yanafunguliwa tukasikia baada ya hii 2015 japo kweli mazingira ya kisiasa sio mazuri, lakini sio utetezi wa kuringia.
Mkuu kama mapungufu yote hayo yanatokea huku yeye akiwa mwenyekiti ni muujiza upi ataufanya zaidi ya haya yanayoendelea sasa na atayafanya lini? Shida Mbowe alishindwa kukubali dhana ya kupokezana vijiti hali ikiwa nzuri enzi za JK, akawa na tamaa ile ile waliyonayo viongozi wote wa kiafrika kupenda madaraka. Kama bado unaamini Mbowe anastahili kuendelea kuwa mwenyekiti zaidi ya muda aliokaa, halafu umekuja na post ndefu kwamba cdm ni taasisi naona kama unatuona watoto. Tukubali tu kwamba wakati ni ukuta, mwambie Mbowe maana najua mnakutana mwambie kuna mtu anajiita Tindo wa jf namshauri kiroho safi kwamba ubora wa kiongozi ni miaka 10 tu, nje ya hapo anajiandaa kufuta ubora wa kazi yake kwa mikono yake.