CHADEMA isipomvua Zitto uanachama...!

CHADEMA isipomvua Zitto uanachama...!

Salama ya CDM na Demokrasia ndani ya CDM ni lazima Zito Afukuzwe uanachama. vinginevyo CDM itaathirika sana kama itamwachia uanachama Zito. 1. Kubwa kuliko yote kukosoana ndani ya chama kutakufa kabisa na kila mmoja anajua athari za chama kutojikosoa. 2. Wanachama na wapenzi ama washabiki wa CDM watakaoonekana wako na Zito wataonekana wasaliti. 3. Kama inavyoaminika na wanachadema Zito anatumika na ccm. ccm hawataacha kumtumia Zito kuivuruga CDM. 4. Kuwepo kwa Zito kutabariki na kuzalisha makundi mengine yenye nia na malengo yaleyale ya kuivuruga CDM. 5. Zito anaonekana ni mtalaam wa siasa za kunyemeleana kuviziana ,Makundi na siasa za kibinafsi si rahisi akaacha harakati hizo
 
Mkuu mimi nitarudisha kadi ya CDM na kubaki kuwa yatima wa kisiasa, Zitto kafanya mabaya mengi sana hata hili la kumchafua Mbowe kahusika na soon tutaleta ushaidi humu.

Sipo tayari kuishi na nyoka nyumba moja.
Hee kumbe mbowe kachafuka, nilikuwa siju
 
Natangaza rasmi kuwa Chadema isipomvua Zitto uanachama nitakuwa wa kwanza kuiviruga kupitia mtandao huu wa JF bila kujali lolote.
Nina details za kuvuruga chama zaidi ya Zitto.

Cc Crashwise

Watajua wenyewe uko chadema sina imani nayo atakidogo isije tuletea vita bure amani yetu ikaja toweka bure mungu ibarik tz.
 
Zito hata hatambikie na kuhonga mpaka fedha zote za washirika ziishe hawezi kusalimika. Watu watakula fedha na bado atapigwa chini..
 
Ukifuatilia siasa za Tanzania utagundua kwamba mara zota Zitto Kabwe anapokuwa kwenye mgogoro na chama chake, utaona viongozi wengi wa CCM wakimtetea kuwa anaonewa, huku wakiingiza masuala ya ukanda na ukabila, Kwenye kikao cha Bunge cha juzi naibu spika akimjibu mbunge wa nyamagana muheshimiwa Wenje alitumia fursa hiyo kuongelea masuala ya zito huku akionyesha kumtetea kwenye mgogoro wa chama chake. Mtela mwampamba ambaye kwa sasa ni kiongozi wa UVCCM amekuwa karibu sana kumtetea zitto ali asivuliwe uongozi, Muheshimiwa Lemma alishambuliwa kwenye mitandao na vijana wa CCM baada tu ya kuwepo vita ya maneno kati yake na Zitto kabwe, na jana tu Muheshimiwa Mbowe ameshambuliwa na Mwigulu Chemba kwa mambo binafsi tu, lakini ukiunganisha dots utajua kuwa hii yote ni kujibu mapigo kutokana na sakata la mtu wao zotto kabwe.
Sasa wana jamii tujiulize kuna masilahi gani ambayo CCM inaendelea kuyapata kwa Zitto kabwe kuendelea kubaki Chadema? Ni kwa nini basi kama zitto ni kiongozi bora hatujasikia kiongozi yoyote wa CCM kumshawishi kujiunga na chama chao? Sasa naanza kuamini kuwa Zitto kabwe ndio karata ya mwisho ya CCM waliyobaki nayo mkononi.

CCM wanafanya hivyo ili kuivuruga zaidi CDM ndo maana chadema wanatakiwa kua makini sana,cha ajabu km ZZK angekua naye anaungana nao hapo ndo ingekua makosa lakin saiv kuna emotions zaid kuliko facts
 
umetumwa na maccm hilo jambo ni la kamati kuu wewe hata halikuhusu kwanza huna hata kadi ya chama
 
Zito hata hatambikie na kuhonga mpaka fedha zote za washirika ziishe hawezi kusalimika. Watu watakula fedha na bado atapigwa chini..

so what??? afukuzwe au aondoke mwenye hasara ni nani?? zitto?? u will b wrong
 
chadema is very interesting party, nakwambia kwa ela akina wasira, mwigulu, nchimbi et al walizokuwa wakimpa zito kabwe ili akiangamize chama real kama ingekua cuf, nccr, tlp nk. zingekufa mda mfup sana.

ivo ni lazima tuwape mda pia tuwaunge mkono viongoz wetu wa chama ili waandae mikakati ya kukiweka sawa chama pia kuandaa hatua madhubut dhid ya msalit zito kwani sio siri chama tayari kiliishajeruhiwa kiasi, kumbuka sakata la akina mtela, mchange, shonza et al na la uyu zito

siku zote huwa nasema huyu bwana ni wakutupilia mbali kabisa liwalo na liwe bora kubaki na wanachama wachache waaminifu kuliko wengi mamluki, huyu bwana nihatari kuliko mnavyofikiri
 
ni kweli kaka maccm ndivyo walivyo wanacho kifanya wao ni kuangalia sehemu ambayo kwao ni karata na kutafuta sehemu ya kuongelea kwa lengo la kukichafua chama kama zzto alienda kinyume na katiba ya chama lazima aadhibitiwe na hiyo ndio tofauti kubwa chadema na ccm kwa hiyo wanatumia karata ya zzto kuvuliwa uongozi kama karata yao ya kutangaza ukanda lakini kwa sasa watanzania wanaona na kusikia
 
Salama ya CDM na Demokrasia ndani ya CDM ni lazima Zito Afukuzwe uanachama. vinginevyo CDM itaathirika sana kama itamwachia uanachama Zito. 1. Kubwa kuliko yote kukosoana ndani ya chama kutakufa kabisa na kila mmoja anajua athari za chama kutojikosoa. 2. Wanachama na wapenzi ama washabiki wa CDM watakaoonekana wako na Zito wataonekana wasaliti. 3. Kama inavyoaminika na wanachadema Zito anatumika na ccm. ccm hawataacha kumtumia Zito kuivuruga CDM. 4. Kuwepo kwa Zito kutabariki na kuzalisha makundi mengine yenye nia na malengo yaleyale ya kuivuruga CDM. 5. Zito anaonekana ni mtalaam wa siasa za kunyemeleana kuviziana ,Makundi na siasa za kibinafsi si rahisi akaacha harakati hizo

Tulia mzee cdm wako makini sana, hii ndio karata ya mwisho ya mwigulu iliyobakia kitambo kidogo tu utajua hili.
 
Natangaza rasmi kuwa Chadema isipomvua Zitto uanachama nitakuwa wa kwanza kuiviruga kupitia mtandao huu wa JF bila kujali lolote.
Nina details za kuvuruga chama zaidi ya Zitto.

Kama unaipenda chadema hizo details zitoe ili kukinusuru
 
Zitto na wenzake watoeni haraka siku kumi na nne tayari, msifikiri mara mbili kuhusu kumvua uanachama. Mkimrudisha atarekebisha makosa aliyofanya na wasaliti wake watakuja smart zaidi ili kuua chama na hapo itakuwa 2015, bora sasa hivi muwatoe huyo ambaye hamjamjua kwanza sio tishio na bora awe mmoja kuliko wawe wengi.

Msikubari kushauriwa, katiba ndio msingi na simamieni katiba. . . mtaonesha kuwa hamuwezi ongoza nchi na mtakuwa hamfuati katiba kama CCM, hatutaweza ona tofauti na wenzenu wa CCM na huo pia ni mtego wao mkimwacha watawavaa.

Kama Zitto na wenzake wanapendwa na watu na ni maarufu waunde chama chao au wahamie chama ambacho watu watawafuata, wanang'ang'ania nini? ebu jiulizeni !!!! Ebo !

ni hayo tu yangu.
 
Subiri tutoke kula krismas Moshi tutamfukaza msaliti huyo masalia.
 
Huo ushaur ungempa bibi ako enz ameshiikwa uchawi lindi,CDM haiendeshwi kwa chuk wala maneno ya wasiojua siasa kama ww,wNamjua Zitto kabwe n nan ktk Chadema ma wanaamin ktk hil
No ZZK No CDM
 
Mkuu! Nakuunga mkono 100%
CHADEMA ni lazima wafanye MAAMUZI HAYO.
Athari ya kuondoka kwa Zitto na wenzake mbona inaonekana imekipa nguvu CHAMA,
Nimeshiriki mikutano kadhaa ya CHADEMA tangu Zitto na wenzake kuvuliwa madaraka, Mikutano na hoja zilizotolewa na Wawezeshaji, Zimepokelewa vizuri na kueleweka vizuri sana.

Naungana nawe. ZITTO na wenzake watimuliwe mapema.
 
Binafsi nimekuwa pamoja na CDM tokea 2007 nikiwa chuoni lakini kwa mara ya kwanza ntarudisha kadi na sitakuja kupiga kura tena katika siasa za nchi hii

Kama mtaamua kumuona ZZK ni bora zaidi ya chama,ni bora zaidi ya maiti ya Mwandosi,ni bora kuliko maiti za Arusha,ni bora kuliko Katiba basi mwacheni ila msije kuilaumu halaiki pale historia itakapokuwa inareveal.
 
wenzako wamejadili usiku na mchana wameshindwa wamefanya vikao mpaka dubai wamekwama wewe unaleta ushauri wako mwepesi hapa.
 
Zitto na wenzake watoeni haraka siku kumi na nne tayari, msifikiri mara mbili kuhusu kumvua uanachama. Mkimrudisha atarekebisha makosa aliyofanya na wasaliti wake watakuja smart zaidi ili kuua chama na hapo itakuwa 2015, bora sasa hivi muwatoe huyo ambaye hamjamjua kwanza sio tishio na bora awe mmoja kuliko wawe wengi.

Msikubari kushauriwa, katiba ndio msingi na simamieni katiba. . . mtaonesha kuwa hamuwezi ongoza nchi na mtakuwa hamfuati katiba kama CCM, hatutaweza ona tofauti na wenzenu wa CCM na huo pia ni mtego wao mkimwacha watawavaa.

Kama Zitto na wenzake wanapendwa na watu na ni maarufu waunde chama chao au wahamie chama ambacho watu watawafuata, wanang'ang'ania nini? ebu jiulizeni !!!! Ebo !

ni hayo tu yangu.

Nenda Moshi ukanywe mbege
 
Wanaosema ZZK aondolewe wote ni kutoka KASKAZINI!Ila kumbukeni DHAMBI ya UBAGUZI haiishi!
 
Back
Top Bottom