Mwaka 2005, ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na kijana nguri wa siasa Zitto Zuberi Kabwe. Nakumbuka ilikuwa eneo maarufu kama Kontena pale chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tulikuwa katika harakati za uchaguzi wa Serikali ya wanafunzi DARUSO.
John Mrema ndiye aliyenitambulisha kwa mwanasiasa huyu kijana na mahiri kwa siasa zake za kuvizia. Ulikuwa uchaguzi wa serikali ya wanafunzi, ambapo Mwita Waitara Mwikwabe ndiye aliyeibuka kidedea. Huyu alijifanya kuvaa nguo za kijani nje kumbe ndani ni gwanda.
Hata kabla ya mwaka huo (2005) nilikuwa nikimsikia Zitto jinsi anavyofanya siasa ndani ya UDSM wakati yeye sio mwanafunzi. Pia nikawa nasikia siasa hizo anazifanya hata vyuo vingine isipokuwa Mzumbe ambapo UVCCM ilikuwa imeweka mizizi.
ZITTO apingwe tu, tena sana.
Nadhani watu wanaweza kudhani nimeungana na Umbowe au Ubabu kumsema Zitto hasha, nilitokea kutopenda siasa za Zitto toka kale. Kwasababu nilimuona ni kijana mahiri na mweredi wa siasa lakini akiwapoteza vijana wengi sana nchini, tena wenye elimu zao.
1. Zitto amewafanya vijana wengi sana kujiunga na chama cha wajanja wajanja (CDM) wakati akijua chama hicho, sio chama kitakachowaletea maendeo watanzania, bali kukuza malalamiko na usanii.
2. Zitto aliwadanganya vijana wengi sana katika elimu ya juu, wakaingia katika migomo katika vyuo vyao. Wengine walifukuzwa na wengine walisimamishwa. Kisa ulikuwa ni mkakati wake wa kuimarisha Chadema.
3. Zitto amewapotosha vijana wengi, ambao sasa wanaona mbele giza, hawajui wafanye nini. Kwasababu aliwapa matumaini makubwa juu ya CDM wakati akijua sio chama cha siasa bali genge la wanasihasa
4. Zitto, baada ya kuwapotosha vijana wengi, sasa hataki kuwaambia ukweli, nini kilichomo ndani ya CDM, zaidi anafanya mipango ya kuwakimbia/kuwatelekeza.
5. Zitto amewafitinisha vijana na serikali yao. Ili waione CDM ni malaika.
Kwa dhati kabisa, Chadema mchapeni viboko vingi, tena vingi.