CHADEMA inavyoliangamiza Taifa!

CHADEMA inavyoliangamiza Taifa!

Uchambuzi makini kabisa kwa wakati muafaka..hicho sio chama bali ni genge la wapiga dili

Kiukweli ccm wamekuwa mstari wa mbele kuwagawa watznia kwa kutumia ukanda,udini maana sikuwah kusikaa cdm wakiyaongelea sana haya maswala ya udini,ukabila,ukanda zaidi ya ccm wao ndy wanaleta udini nakusababisha dini moja kuichukia dini nyingine ccm mmeuwa watu wengi sana na ushahidi tunao na hata watznia ni mashahidi mkotayari kuuwa ili muendele kutawala.JAMANI HEBU JARIBUNI KUMUOGOPA MUNGU
 
Unajitahidi kumdanganya nani ?

CCM ni wezi kila mtu anajua hivyo.

CCM ni wachovu kila mtu anajua hivyo.
CCM ni propaganda daima kila mtu anajua hivyo.

Bado hunishawishi hata kidogo.
 
MEA MTWARO! Hongera sana kwa kuisemea haki, Tuache ushabiki wa kinazi bali uzalendo utawale
 
Kweli CHADEMA ndio waliofanya ufisadi huu:
Richmond
Kagoda
Mwananchi Goldmine
EPA
Dowans
IPTL
Jairo saga
Tajeni muendelee,
Kuwapa wazungu madini bure
 
Kachukue posho wee Gamba.
Katibu mkuu wa CHADEMA taifa kwa sasa yuko hoi bin taabani kuongoza chama chake, ambacho hivi karibuni kiliweza kujizolea sifa hapa nchini, kwa kile kinacho daiwa kuwa kiliweza kutoa changamoto kubwa kwa chama tawala (CCM).

Jambo la kushangaza na kushtua kuhusu hiki chama, ni kuporomoka kwa umaarufu wake nchini, baada ya watanzania kugundua kuwa sio chama cha 'demokrasia' na 'maendeleo' kama wanavyo jipambanua, ila ni chama cha vurugu, fujo na maandamano yenye kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.

Sifa hizi mpya kwa chama hiki, ambazo ni fujo na vurugu, zimetolewa na wananchi baada tu ya CHADEMA kumpa mamlaka Dr Slaa ya kuwa mtendaji mkuu wa chama hicho, Dr Slaa kwa siasa na mbinu zake, alidhani kwa kutumia maandamano basi ndio itakuwa njia pekee ya kuzidi kuinua jina na hadhi ya chama, kumbe imekuwa kinyume chake.

Mikakati ya Dr Slaa ya kuleta mageuzi ya siasa hapa nchini kupitia chama chake (CHADEMA) na washirika wake IMEDODA, na badala yake mikakati hiyo imefanikiwa kuondoa na kutokomeza kabisa sentensi isemayo "Tanzania ni kisiwa cha amani", na kwa sasa kuwa kisiwa cha wahanga wa mabomu.

Hoja ya msingi hapa ni kwamba, kama Dr Slaa amechemka na yuko hoi kuiongoza CHADEMA kwenye kufanya siasa za kistaarabu na safi. Je, atawezaje kuongoza nchi yetu yenye changamoto za kila aina?, haya ni mambo ya msingi sana kuhoji, kwani kushabikia uozo ambao utaenda kuliangamiza taifa sio UZALENDO hata kidogo.
 
Sasa ni VIPI CHADEMA kimeliangamiza TAIFA???? Unajua CCM kunyamazisha MBUNGE SELII na kumpa kiti kiupendeleo KIGANGWALLA mtoto wa MAMA SALMA hauoni huo UPENDELEO ndio UTAKAO LIMALIZA TAIFA HILI??

UPENDELEO; URAFIKI; UKUADI; UNAFIKI; UDINI; UKABILA... ndio inavyotukuzwa... SELIII alikuwa anaikosoa serikali kwa Manufaa ya Wananchi wote... lakini wewe na KIGANGWALLA na Rais wako kwasababu ni waislamu hamkupenda hivyo
 
Unasemaaa? unakatikakatika sikusikii vizuri mzeee, unasemaaaa?
 
Katibu mkuu wa CHADEMA taifa kwa sasa yuko hoi bin taabani kuongoza chama chake, ambacho hivi karibuni kiliweza kujizolea sifa hapa nchini, kwa kile kinacho daiwa kuwa kiliweza kutoa changamoto kubwa kwa chama tawala (CCM).

Jambo la kushangaza na kushtua kuhusu hiki chama, ni kuporomoka kwa umaarufu wake nchini, baada ya watanzania kugundua kuwa sio chama cha 'demokrasia' na 'maendeleo' kama wanavyo jipambanua, ila ni chama cha vurugu, fujo na maandamano yenye kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.

Sifa hizi mpya kwa chama hiki, ambazo ni fujo na vurugu, zimetolewa na wananchi baada tu ya CHADEMA kumpa mamlaka Dr Slaa ya kuwa mtendaji mkuu wa chama hicho, Dr Slaa kwa siasa na mbinu zake, alidhani kwa kutumia maandamano basi ndio itakuwa njia pekee ya kuzidi kuinua jina na hadhi ya chama, kumbe imekuwa kinyume chake.

Mikakati ya Dr Slaa ya kuleta mageuzi ya siasa hapa nchini kupitia chama chake (CHADEMA) na washirika wake IMEDODA, na badala yake mikakati hiyo imefanikiwa kuondoa na kutokomeza kabisa sentensi isemayo "Tanzania ni kisiwa cha amani", na kwa sasa kuwa kisiwa cha wahanga wa mabomu.

Hoja ya msingi hapa ni kwamba, kama Dr Slaa amechemka na yuko hoi kuiongoza CHADEMA kwenye kufanya siasa za kistaarabu na safi. Je, atawezaje kuongoza nchi yetu yenye changamoto za kila aina?, haya ni mambo ya msingi sana kuhoji, kwani kushabikia uozo ambao utaenda kuliangamiza taifa sio UZALENDO hata kidogo.

To hell you stupid fool. Huna kazi ya kufanya wewe? Seva za Jf inajaa upuuzi wako, kwa kweli mods inabidi wascan hii system imeingiliwa na kirusi kinachoitwa hamy d! Hili jukwaa la great thinkers sasa hivi limeingiliwa sana na hawa mburula!
 
Kwa kawaida watu makini hawaongozwi na Ubinafsi katika kujadili masuala mbalimbali muhimu ya kitaifa. Hawasukumwi na Umimi, ukabila, ukanda na Udini katika kutoa michango na maoni katika ujenzi wa Taifa, hali ipo tofauti kwa Waumini wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wanajitambulisha kwa Udini,ukabila,ukanda,Umimi na Ubinafsi katika kujadili mambo nyeti ya Kitaifa.

Aidha Watu wanaojipofisha jicho la kulia na kuacha la kushoto kuangalia mambo mabaya tu hawawezi kuitwa 'Great Thinkers' kama wanavyojidanganya Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Mitandao ya Kijamii.

Naam! Ndugu wapendwa, kabla ya kusogeza Mguu mbele, naomba kusema kuwa, ni Ibara ya 18(a)ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inayonipa haki ya kuandika Makala hii kwani Ibara hiyo inatoa Uhuru wa Mtu kutoa Mawazo na Fikra zake kuhusu Nchi yake

Ndiyo! nimeamua kuandika Makala hii kutokana na maoni na michango mbalimbali iliyotolewa na Waumini wa CHADEMA katika Mtandao wa Jamiiforums ambapo walikuwa wakichangia Makala iliyoandikwa na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Khamisi Kigwangalla. Michango na maoni hayo ni Ushahidi tosha kwamba CHADEMA inawahujumu Watanzania na Taifa kwa Ujumla.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 30,May 2013, Mbunge wa Jimbo la Nzega,Mkoani Tabora, Dk. Kigwangwalla aliandika Makala katika Mtandao wa Jamiiforums. Katika Makala hiyo Dk. Kigwangalla alieleza Matatizo mbalimbali yanayolikabili Taifa letu huku akipendekeza njia mbadala kuyakabili Matatizo hayo.Kubwa zaidi Dk. Kigwangalla aliwataka Watanzania kubadilika Kifikra huku akisema kuwa,"Uoga wa kubalika ni sumu kwa Wapenda Maendeleo". Ngoja niendelee kumnukuu Mbunge huyo ili kwayo Maoni yake yaweze kulinganishwa na kile kilichochangiwa na 'Wanamagwanda'.

"Napenda kuona Watanzania, Sote kwa pamoja tukibadilika kifikra. Tuanze kuwa Wabunifu zaidi, wenye Uthubutu,Wachapa kazi, Waaminifu, kuweka mbele Uzalendo kwa faida ya wote badala ya Umimi zaidi kwa faida yangu. Napenda kuona Watanzania Wenzangu tukizaliwa Upya leo na kuanza nguvu mpya leo ya kuleta mabadiliko ya kifikra na Kiutendaji. Tuondoke kwenye Umbumbumbu wa kuamini kuwa,kila kitu kitaletwa na Serikali. Tuanze kuamini kuwa, tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kuchukua hatua sahihi katika maisha yetu binafsi na katika jamii yetu. Tuanze kuamini vingine kuwa, tunaweza kuamua kuibalisha Nchi yetu sisi wenyewe na kutoka hapa tulipo leo na kuingia Dunia nyingine kabisa kiuchumi na kijamii".

Bila shaka Mawazo yaliyoandikwa katika Makala hiyo ni ya kupongezwa,kuungwa mkono,kuhamasishwa na kufanfanyiwa kazi kwa Watu wenye Ujenzi wa Fikra kwani Mwandishi wa Makala hiyo ameonekana kuandika kwa hisia kali na hivyo kudhihirisha kuwa, ameguswa na kukerwa na matatizo yanayolikabili Taifa letu. Hongera sana Kigwangalla.

Lakini tazama! hali inakuwa tofauti kwa Wafuasi wa CHADEMA,baada ya kuunga mkono,kuhamasisha na kufanyia kazi mawazo hayo, wametumia Wino wao kubeza na kutweza mawazo hayo kwa kuwa tu yamesemwa na Mtu wa CCM. Yangesemwa na Kiongozi wa CHADEMA yangekuwa lulu. Huu ni Uzandiki wa Fikra unaoweza kuliangamiza Taifa letu kwa Misingi ya Uchama, Ubinafsi na Umimi na kwamba vitendo hivi vya hovyo hufanywa na Wasomi Uchwara na Wanasiasa Makapi wasiolitakia Taifa mema na haya ni matokeo ya kushindwa kujenga hoja na kutumia hoja za nguvu kuyafanya mambo yao yakubalike.

Aidha, ni bora kuwasilisha kwenu baadhi ya michango na maoni ya baadhi ya Wanamtandao huo wa Jamiiforums ambao mara nyingi wanajitambulisha na kujigamba kwa Uchama badala ya Utaifa kama ifuatavyo:

Mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Steven Robert Masatu amesema "Huwezi kuhubiri Fikra mbadala ilihali wewe upo kwenye fikra mgando. Mkuu toka kwanza huko uliko( CCM)". Evi ni kweli kwa mfano si sahihi kwa mnyonge kuwatetea wanyoge wenzake kwa kuwa tu naye ni Mnyoge? kama hivyo ndivyo basi Mwalimu Nyerere asingeliwatetea Watanzania maana alikuwa Mnyonge, kama si upotoshaji nini?.Ingawa hata hivyo Kigwanga haonekani kuwa na Fikra mgando maana aliyoyanena hapo hunenwa na wachache tu.

Nderingosha kama anavyojitambulisha katika Mtandao huo amesema "Hizi Makala ungekuwa unawaandikia Wabunge wenzako wa CCM maana wao ndio wanatakiwa kubadilika kifikra na siyo Wananchi". Huu ni ukweli au kuwahujumu Watanzania?

Vilevi Meningits amesema kuwa "Badiliko la kwanza ni kuitoa CCM mwaka 2015" huku akifuatiwa na mwenzake anayejitambulisha kwa jina la Verified na kusema kuwa, "Tatizo ni CCM" hawa ndio wasomi wetu wanaoyaangalia mambo kwa jicho moja tena la kushoto. Ewe Mwenyezi epusha janga hili katika Taifa letu.

Hivyo,Wachangiaji hawa wanne ni wachache kati ya Wengi wanaojitambulisha kwa Uchadema katika mtandao huo wa kijamii ambao wanaonekana kukifia chama kuliko Taifa, kupinga 'Constructive Ideas' kwa sababu tu yamesemwa na Mtu wa CCM na kuyaangalia mambo kwa jicho la kushoto huku wakiziba la kulia wasione mazuri. Huku ni kulitafuna Taifa kwa Misingi ya Uchama, Umimi na Ubinafsi.

Nisingependa kumaliza makala hii pasi na kuwashauri viongozi wa CHADEMA na Wafuasi wake kuwa, wawe tayari kulifia Taifa kuliko Chama, Wawaunge mkono viongozi wetu pale wanapokuja na mikakati ya kuljenga Taifa,kuwapa moyo viongozi wetu kwa mawazo yao pale yanapoonekana ni ya tija kuliko kuwabeza, tweza na kuwakatisha tamaa kwani kufanya hivyo kwaweza kupelekea viongozi wetu kujihusisha na malumbano badala ya kusisimamia shughuli za kimaendeleo na hatimaye kulipeleka Taifa kwenye Mdomo wa Mamba. Kwa faida ya nani?

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Ninaitwa BAKARI MADAYA (Mwanatunduru).
Ninapatikana simu: 0789357823 au barua pepe madayabakar@hotmail.com

Huna lolote, njaa tu
 
Arusha ni mji wa kitalii na mlango wa kuingia TZ kwa watalii na wageni! walalahoi wengi hujipatia mkate wao tokana na sifa hizi za Arusha!
Kwanini chama cha upinzani CDM wanaitumia Arusha kuwa kitovu cha machafuko na misukosuko? kwanini hawaendi Kilimanjaro kulikoasisiwa Chadema? walalahoi wa Arusha wanataabika kwasababu Chadema wameamua kuwaadhibu wananchi wa Arusha kwa kuifanya Arusha kuwa mji wa maasi na machafuko ili Arusha iathirike kiuchumi na lengo lao la kuhujumu uchumi wa Arusha lifanikiwe!

Ombi langu kwa Wana Arusha wasikubali kutumiwa na CDM kuhujumu uchumi wa Arusha kwani watakaoathirika niwao na familia zao huku wenzao wa Kilimanjaro wakineemeka kwa kulinda amani na mshikamano wao!

i. Wewe ni msemaji wa wanaArusha?
ii. Hao wananchi wa Arusha ni misukule?
iii. Wa uhujumu uchumi wa Arusha ili iweje?

Tuanze na hayo matatu kwanza.

Kwa kawaida watu makini hawaongozwi na Ubinafsi katika kujadili masuala mbalimbali muhimu ya kitaifa. Hawasukumwi na Umimi, ukabila, ukanda na Udini katika kutoa michango na maoni katika ujenzi wa Taifa, hali ipo tofauti kwa Waumini wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wanajitambulisha kwa Udini,ukabila,ukanda,Umimi na Ubinafsi katika kujadili mambo nyeti ya Kitaifa.

Aidha Watu wanaojipofisha jicho la kulia na kuacha la kushoto kuangalia mambo mabaya tu hawawezi kuitwa 'Great Thinkers' kama wanavyojidanganya Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Mitandao ya Kijamii.

Naam! Ndugu Wapendwa, kabla ya kusogeza Mguu mbele, naomba kusema kuwa, ni Ibara ya 18(a)ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inayonipa haki ya kuandika Makala hii kwani Ibara hiyo inatoa Uhuru wa Mtu kutoa Mawazo na Fikra zake kuhusu Nchi yake. Hivyo naomba ieleweke kuwa, natekeleza ibara hiyo.

Ndiyo! nimeamua kuandika Makala hii kutokana na maoni na michango mbalimbali iliyotolewa na Waumini wa CHADEMA katika Mtandao wa Jamiiforums ambapo walikuwa wakichangia Makala iliyoandikwa na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Khamisi Kigwangalla. Michango na maoni hayo ni Ushahidi tosha kwamba CHADEMA inawahujumu Watanzania na Taifa kwa Ujumla.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 30,May 2013, Mbunge wa Jimbo la Nzega,Mkoani Tabora, Dk. Kigwangwalla aliandika Makala katika Mtandao wa Jamiiforums. Katika Makala hiyo Dk. Kigwangalla alieleza Matatizo mbalimbali yanayolikabili Taifa letu huku akipendekeza njia mbadala kuyakabili Matatizo hayo.Kubwa zaidi Dk. Kigwangalla aliwataka Watanzania kubadilika Kifikra huku akisema kuwa,"Uoga wa kubalika ni sumu kwa Wapenda Maendeleo". Ngoja niendelee kumnukuu Mbunge huyo ili kwayo Maoni yake yaweze kulinganishwa na kile kilichochangiwa na 'Wanamagwanda'.

"Napenda kuona Watanzania, Sote kwa pamoja tukibadilika kifikra. Tuanze kuwa Wabunifu zaidi, wenye Uthubutu,Wachapa kazi, Waaminifu, kuweka mbele Uzalendo kwa faida ya wote badala ya Umimi zaidi kwa faida yangu. Napenda kuona Watanzania Wenzangu tukizaliwa Upya leo na kuanza nguvu mpya leo ya kuleta mabadiliko ya kifikra na Kiutendaji. Tuondoke kwenye Umbumbumbu wa kuamini kuwa,kila kitu kitaletwa na Serikali. Tuanze kuamini kuwa, tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kuchukua hatua sahihi katika maisha yetu binafsi na katika jamii yetu. Tuanze kuamini vingine kuwa, tunaweza kuamua kuibalisha Nchi yetu sisi wenyewe na kutoka hapa tulipo leo na kuingia Dunia nyingine kabisa kiuchumi na kijamii".

Bila shaka Mawazo yaliyoandikwa katika Makala hiyo ni ya kupongezwa,kuungwa mkono,kuhamasishwa na kufanfanyiwa kazi kwa Watu wenye Ujenzi wa Fikra kwani Mwandishi wa Makala hiyo ameonekana kuandika kwa hisia kali na hivyo kudhihirisha kuwa, ameguswa na kukerwa na matatizo yanayolikabili Taifa letu. Hongera sana Kigwangalla.

Lakini tazama! hali inakuwa tofauti kwa Wafuasi wa CHADEMA,baada ya kuunga mkono,kuhamasisha na kufanyia kazi mawazo hayo, wametumia Wino wao kubeza na kutweza mawazo hayo kwa kuwa tu yamesemwa na Mtu wa CCM. Yangesemwa na Kiongozi wa CHADEMA yangekuwa lulu. Huu ni Uzandiki wa Fikra unaoweza kuliangamiza Taifa letu kwa Misingi ya Uchama, Ubinafsi na Umimi na kwamba vitendo hivi vya hovyo hufanywa na Wasomi Uchwara na Wanasiasa Makapi wasiolitakia Taifa mema na haya ni matokeo ya kushindwa kujenga hoja na kutumia hoja za nguvu kuyafanya mambo yao yakubalike.

Aidha, ni bora kuwasilisha kwenu baadhi ya michango na maoni ya baadhi ya Wanamtandao huo wa Jamiiforums ambao mara nyingi wanajitambulisha na kujigamba kwa Uchama badala ya Utaifa kama ifuatavyo:

Mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Steven Robert Masatu amesema "Huwezi kuhubiri Fikra mbadala ilihali wewe upo kwenye fikra mgando. Mkuu toka kwanza huko uliko( CCM)". Evi ni kweli kwa mfano si sahihi kwa mnyonge kuwatetea wanyoge wenzake kwa kuwa tu naye ni Mnyoge? kama hivyo ndivyo basi Mwalimu Nyerere asingeliwatetea Watanzania maana alikuwa Mnyonge, kama si upotoshaji nini?.Ingawa hata hivyo Kigwanga haonekani kuwa na Fikra mgando maana aliyoyanena hapo hunenwa na wachache tu.

Nderingosha kama anavyojitambulisha katika Mtandao huo amesema "Hizi Makala ungekuwa unawaandikia Wabunge wenzako wa CCM maana wao ndio wanatakiwa kubadilika kifikra na siyo Wananchi". Huu ni ukweli au kuwahujumu Watanzania?

Vilevi Meningits amesema kuwa "Badiliko la kwanza ni kuitoa CCM mwaka 2015" huku akifuatiwa na mwenzake anayejitambulisha kwa jina la Verified na kusema kuwa, "Tatizo ni CCM" hawa ndio wasomi wetu wanaoyaangalia mambo kwa jicho moja tena la kushoto. Ewe Mwenyezi epusha janga hili katika Taifa letu.

Hivyo,Wachangiaji hawa wanne ni wachache kati ya Wengi wanaojitambulisha kwa Uchadema katika mtandao huo wa kijamii ambao wanaonekana kukifia chama kuliko Taifa, kupinga 'Constructive Ideas' kwa sababu tu yamesemwa na Mtu wa CCM na kuyaangalia mambo kwa jicho la kushoto huku wakiziba la kulia wasione mazuri. Huku ni kulitafuna Taifa kwa Misingi ya Uchama, Umimi na Ubinafsi.

Nisingependa kumaliza makala hii pasi na kuwashauri viongozi wa CHADEMA na Wafuasi wake kuwa, wawe tayari kulifia Taifa kuliko Chama, Wawaunge mkono viongozi wetu pale wanapokuja na mikakati ya kuljenga Taifa,kuwapa moyo viongozi wetu kwa mawazo yao pale yanapoonekana ni ya tija kuliko kuwabeza, tweza na kuwakatisha tamaa kwani kufanya hivyo kwaweza kupelekea viongozi wetu kujihusisha na malumbano badala ya kusisimamia shughuli za kimaendeleo na hatimaye kulipeleka Taifa kwenye Mdomo wa Mamba. Kwa faida ya nani?

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

.
Ninapatikana simu: 0789357823

Mimi sijasoma makala yako ila kichwa cha habari tu kinatosha kunifanya nitoe mchango wangu. Hivi unavyosema chadema kinaangamiza taifa una maana gani? Chadema ndo kinaongoza serikali? Jamani watanzania hizi siasa za ubaguzi tutaacha lini? Badala ya kuishukuru Chadema inavyoisukuma seriakali kuboresha maisha ya walalahoi ninyi mmekalia ujinga na majungu tu.
 
tindikali ni chadema, sumu chadema, mabomu chadema, bastola chadema uzushi uongo na uzandiki chadema
 
Mimi sijasoma makala yako ila kichwa cha habari tu kinatosha kunifanya nitoe mchango wangu? Hivi unavyosema chadema kinaangamiza taifa una maana gani? Chadema ndo kinaongoza serikali? Jamani watanzania hizi siasa za ubaguzi tutaacha lini? Badala ya kuishukuru Chadema inavyoisukuma seriakali kuboresha maisha ya walalahoi ninyi mmekalia ujinga wa kulaumu.
watu wanaangalia issues kama vile
kumwagia watu tindikali
kulisha watu sumu
kujilipua kwa mabomu nk. hayo unayowadanganya watu eti kuisukuma serikali ni uzushi mtupu
 
Chadema ndio wauza madawa ya kulevya. Chadema ndio watekaji na wauaji wa waandishi wa Habari kisha hawakamatwi. Chadema ndio wanaouza wanyama hai nje ya nchi. Chadema ndio wanaofanya kila kitu kiovu hapa TZ.

Kwa taarifa yako watu tunaakili zetu. Hatukai kusikiliza porojo zako zilizopitwa na wakati. Hata kama sio Chadema sawa ila tumechoka na CCM.

Halafu unaandika huku umeshindwa kuishirikisha akili yako na kizazi chako kijacho kwa sababu ya njaa yako. Shame on u.
 
Back
Top Bottom