CHADEMA inavyoliangamiza Taifa!

CHADEMA inavyoliangamiza Taifa!

attachment.php

Kazi kweli kweli. Hapa hakuna kitu. Wanatumia sare na miavuli ya ccm kupanga namna ya kupata masoko mapya ya ndani na nje baada ya kuonekana Chine kimenuka na pia usalama wao. Pengine hicho kingine kitakuwa kimewapa uzoefu namna kilivyopona pona kitanzi kwa MAO.
 
"Kwa kawaida watu makini hawaongozwi na Ubinafsi katika kujadili masuala mbalimbali muhimu ya kitaifa."

Mstari wako wa kwanza tu unakinzana na kile unachokiamini.Ungekuwa mzalendo kweli nilitegemea makala yako iongelee hati chafu ktk Halmashauri zetu,huduma mbovu za jamii,mikataba ya siri kubwa isiyo na maslahi kwa taifa,rushwa na ukiritimba.Lakini kwa sababu haya yana uhusiano wa moja kwa moja na chama chako umeamua kuweka ubinafsi mbele na utaifa nyuma.
 
Kwa wasiotumia akili wataona umenena lkn ukweli ni kwamba wanawezaje kuliangamiza taifa wakati sio chama tawala? Chama tawala kinafanya nini mpaka taifa linaangalia wenyewe wanaangalia tuu?, CCM ndio wanaoongoza sasa iweje wengine CDM waangamize wao waangalie na kushangilia? mpaka hapo umejichanganya mwenyewe WANAO ANGAMIZA NI CCM:

Kwa jinsi CDM wanavyobambikiwa kesi ni wazi kabisa wakifanya makosa ndio kaburi lao. hiyo tu inaonyesha kuwa wako makini. kama wangekuwa wanauza unga wangeshafia jela siku nyingi maana wasingehangaika na kesi za kubambikia.

Ukiona mtu ambaye wewe unamdharau halafu anahesimiwa na kupendwa na watu zaidi yako basi ujue wewe Thamani yako ni ndogo kuliko ya huyo unayemdharau. WACHENI CDM ipendwe, iheshimiwe na kuthaminiwa na watu hata kama nyie CCM hamuipenda kinawauma nini?

Ccm wanahangaika sana,na hasa misukule ya uvccm iliyomo humu wanajidai hawaoni matukio ya kipuuzi yanayofanywa na viongozi wao eti wanatetea

Unaemtetea anayo nyumba nzuri,gari zuri,maisha yake pamoja na familia yake ni mazuri sana tu Vipi we pangu pakavu ambaye haujui familia yako inaishije,maisha ya kubahatisha,umetembea mpaka viatu soli imekwisha upande halafu unajidai una maslahi kwenye chama cha mafisadi,poor you
 
kigwangalla ni mjinga tena sana na aseme chadema wanajitambulisha kwa ukanda na ni ukanda gani? chadema wanajitambulisha kwa ukabila ni kabila gani ambalo halipo ccm? na ni dini gani ambayo haipo ccm?

Narudia tena kigwangalla ni mjinga maana anajifanya kuhamasisha watu kwenye mitandao kuhusu maendeleo wakati ameshindwa kuwahamasisha wabumge wenzie anao kuwa nao kila leo wanapinga hoja za waponzani hata zikiwa na faida kwa taifa kazi yao ni kusema ndio kwa kitu hata vonavyo waumiza wananchi.

kigwangalla atwambie kwamza ameweza kuwabadili wanaccm wenzake wàache kusuma ndio kwa kila k itu? ni hoja ngapi nzuri za wapinzani mmekuwa mkizipinga?

hatuwezi kukubali unafiki wako wakijifanya una hubiri maendeleo kwenye mitandao wakati bungeni unashindwa kuwahubiria wenzio.

Ni mjinga pekee anaweza kuami hii makala yako eti chadema wanabeza maendeleo,kila mtu anajua fika kinachotufanya kulumbana nim kutaka maendeleo na ndio maana hatuachi kuwasifu watu kama Anna Tibaijuka,Mwakyembe na Magufulu na tumekuwa tukiwasifun na kutamani waame chama chenu maana kina wachafua hawa wapendamaendeleo.

Hatutaki muhubiri maendeleo bali tunahitaji wanaotenda.Maneno mengi yaninim kwenye mitandao wakati matendo sifuri? tunahutaji matendo ya watu kama hao hapo.

Kigwangalla ni mnafiki sana unashindwa kuwabadilisha wenzio unajifanya kuja kuhubiri humu.

Tunataka matendo si maneno.
 
MEA MTWARO! Hongera sana kwa kuisemea haki, Tuache ushabiki wa kinazi bali uzalendo utawale

ni ukweli gani anaisema HKigwangalla? ni kweli kama ni muhamasisha maendeleo angeshindwa kuwahubiria wanaccm wenzio wasiseme ndio kwa kila kitu? umesahau kuwa ndiyo ya kigwangalla na wenzie ndio imezaa kodi ya simu sasa hivi wana hangaika kujinusuru?

hebu tuwe wa kweli ni maendeleo gani yana hubiriwa na kigwangalla?
 
Last edited by a moderator:
Kwa kawaida watu makini hawaongozwi na Ubinafsi katika kujadili masuala mbalimbali muhimu ya kitaifa. Hawasukumwi na Umimi, ukabila, ukanda na Udini katika kutoa michango na maoni katika ujenzi wa Taifa, hali ipo tofauti kwa Waumini wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wanajitambulisha kwa Udini,ukabila,ukanda,Umimi na Ubinafsi katika kujadili mambo nyeti ya Kitaifa.

Aidha Watu wanaojipofisha jicho la kulia na kuacha la kushoto kuangalia mambo mabaya tu hawawezi kuitwa 'Great Thinkers' kama wanavyojidanganya Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Mitandao ya Kijamii.

Naam! Ndugu wapendwa, kabla ya kusogeza Mguu mbele, naomba kusema kuwa, ni Ibara ya 18(a)ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inayonipa haki ya kuandika Makala hii kwani Ibara hiyo inatoa Uhuru wa Mtu kutoa Mawazo na Fikra zake kuhusu Nchi yake

Ndiyo! nimeamua kuandika Makala hii kutokana na maoni na michango mbalimbali iliyotolewa na Waumini wa CHADEMA katika Mtandao wa Jamiiforums ambapo walikuwa wakichangia Makala iliyoandikwa na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Khamisi Kigwangalla. Michango na maoni hayo ni Ushahidi tosha kwamba CHADEMA inawahujumu Watanzania na Taifa kwa Ujumla.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 30,May 2013, Mbunge wa Jimbo la Nzega,Mkoani Tabora, Dk. Kigwangwalla aliandika Makala katika Mtandao wa Jamiiforums. Katika Makala hiyo Dk. Kigwangalla alieleza Matatizo mbalimbali yanayolikabili Taifa letu huku akipendekeza njia mbadala kuyakabili Matatizo hayo.Kubwa zaidi Dk. Kigwangalla aliwataka Watanzania kubadilika Kifikra huku akisema kuwa,"Uoga wa kubalika ni sumu kwa Wapenda Maendeleo". Ngoja niendelee kumnukuu Mbunge huyo ili kwayo Maoni yake yaweze kulinganishwa na kile kilichochangiwa na 'Wanamagwanda'.

"Napenda kuona Watanzania, Sote kwa pamoja tukibadilika kifikra. Tuanze kuwa Wabunifu zaidi, wenye Uthubutu,Wachapa kazi, Waaminifu, kuweka mbele Uzalendo kwa faida ya wote badala ya Umimi zaidi kwa faida yangu. Napenda kuona Watanzania Wenzangu tukizaliwa Upya leo na kuanza nguvu mpya leo ya kuleta mabadiliko ya kifikra na Kiutendaji. Tuondoke kwenye Umbumbumbu wa kuamini kuwa,kila kitu kitaletwa na Serikali. Tuanze kuamini kuwa, tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kuchukua hatua sahihi katika maisha yetu binafsi na katika jamii yetu. Tuanze kuamini vingine kuwa, tunaweza kuamua kuibalisha Nchi yetu sisi wenyewe na kutoka hapa tulipo leo na kuingia Dunia nyingine kabisa kiuchumi na kijamii".

Bila shaka Mawazo yaliyoandikwa katika Makala hiyo ni ya kupongezwa,kuungwa mkono,kuhamasishwa na kufanfanyiwa kazi kwa Watu wenye Ujenzi wa Fikra kwani Mwandishi wa Makala hiyo ameonekana kuandika kwa hisia kali na hivyo kudhihirisha kuwa, ameguswa na kukerwa na matatizo yanayolikabili Taifa letu. Hongera sana Kigwangalla.

Lakini tazama! hali inakuwa tofauti kwa Wafuasi wa CHADEMA,baada ya kuunga mkono,kuhamasisha na kufanyia kazi mawazo hayo, wametumia Wino wao kubeza na kutweza mawazo hayo kwa kuwa tu yamesemwa na Mtu wa CCM. Yangesemwa na Kiongozi wa CHADEMA yangekuwa lulu. Huu ni Uzandiki wa Fikra unaoweza kuliangamiza Taifa letu kwa Misingi ya Uchama, Ubinafsi na Umimi na kwamba vitendo hivi vya hovyo hufanywa na Wasomi Uchwara na Wanasiasa Makapi wasiolitakia Taifa mema na haya ni matokeo ya kushindwa kujenga hoja na kutumia hoja za nguvu kuyafanya mambo yao yakubalike.

Aidha, ni bora kuwasilisha kwenu baadhi ya michango na maoni ya baadhi ya Wanamtandao huo wa Jamiiforums ambao mara nyingi wanajitambulisha na kujigamba kwa Uchama badala ya Utaifa kama ifuatavyo:

Mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Steven Robert Masatu amesema "Huwezi kuhubiri Fikra mbadala ilihali wewe upo kwenye fikra mgando. Mkuu toka kwanza huko uliko( CCM)". Evi ni kweli kwa mfano si sahihi kwa mnyonge kuwatetea wanyoge wenzake kwa kuwa tu naye ni Mnyoge? kama hivyo ndivyo basi Mwalimu Nyerere asingeliwatetea Watanzania maana alikuwa Mnyonge, kama si upotoshaji nini?.Ingawa hata hivyo Kigwanga haonekani kuwa na Fikra mgando maana aliyoyanena hapo hunenwa na wachache tu.

Nderingosha kama anavyojitambulisha katika Mtandao huo amesema "Hizi Makala ungekuwa unawaandikia Wabunge wenzako wa CCM maana wao ndio wanatakiwa kubadilika kifikra na siyo Wananchi". Huu ni ukweli au kuwahujumu Watanzania?

Vilevi Meningits amesema kuwa "Badiliko la kwanza ni kuitoa CCM mwaka 2015" huku akifuatiwa na mwenzake anayejitambulisha kwa jina la Verified na kusema kuwa, "Tatizo ni CCM" hawa ndio wasomi wetu wanaoyaangalia mambo kwa jicho moja tena la kushoto. Ewe Mwenyezi epusha janga hili katika Taifa letu.

Hivyo,Wachangiaji hawa wanne ni wachache kati ya Wengi wanaojitambulisha kwa Uchadema katika mtandao huo wa kijamii ambao wanaonekana kukifia chama kuliko Taifa, kupinga 'Constructive Ideas' kwa sababu tu yamesemwa na Mtu wa CCM na kuyaangalia mambo kwa jicho la kushoto huku wakiziba la kulia wasione mazuri. Huku ni kulitafuna Taifa kwa Misingi ya Uchama, Umimi na Ubinafsi.

Nisingependa kumaliza makala hii pasi na kuwashauri viongozi wa CHADEMA na Wafuasi wake kuwa, wawe tayari kulifia Taifa kuliko Chama, Wawaunge mkono viongozi wetu pale wanapokuja na mikakati ya kuljenga Taifa,kuwapa moyo viongozi wetu kwa mawazo yao pale yanapoonekana ni ya tija kuliko kuwabeza, tweza na kuwakatisha tamaa kwani kufanya hivyo kwaweza kupelekea viongozi wetu kujihusisha na malumbano badala ya kusisimamia shughuli za kimaendeleo na hatimaye kulipeleka Taifa kwenye Mdomo wa Mamba. Kwa faida ya nani?

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Ninaitwa BAKARI MADAYA (Mwanatunduru).
Ninapatikana simu: 0789357823 au barua pepe madayabakar@hotmail.com

Mkuu Bakari, hapo kuna kitu usichokielewa juu ya hoja zitolewazona maProCHADEMA! Kama ingekuwa huwa wanapinga kila kitu kama unavyojadiri, hebu angalia kwenye thread ya mama Ana Tibaijuka! Tatizo si dini, kabila, kanda au chochote ulichoandika kwenye uzi wako, tatizo ni je huyo mtu anaishi kama anavyo hubiri? Ungewauliza why critisise him na siyo, Mwakyembe, Tibaijuka, Kagasheki! Ungepata jibu, watu wana data za kila mtu hapa! Ukianza kusema tuvae nguo wakati wewe uko uchi watakuhoji accordingly! Umekosa upeo wa kina katika kujenga hoja yako!
 
hahaha... nae anataka ubunge?

Kama CHADEMA ikiendelea na utaratibu wa kupokea tu watu wa aina hiyo na kuwafanya makamanda wao, basi nadiriki kusema bado CHADEMA haipo serious.

Kwani huku CCM kuna utaratibu maalumu wa kupata wanachama, ni ndio maana tuna 'wafia' chama wengi kwa taratibu tulizo jiwekea.

CHADEMA jifunzeni kutoka kwa baba.

ina maana Nakaya mlimpokea kwa utaratibu gani? unataka kusema kuwa hao wangekuja kwenu mge wa kataa? hizi ni kauli za kushindwa? kama agenda ya kujivua gamba ina washinda hivi uoni aibu kusema ccm ni chama cha utaratibu na wafia chama.
 
Kwa kawaida watu makini hawaongozwi na Ubinafsi katika kujadili masuala mbalimbali muhimu ya kitaifa. Hawasukumwi na Umimi, ukabila, ukanda na Udini katika kutoa michango na maoni katika ujenzi wa Taifa, hali ipo tofauti kwa Waumini wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wanajitambulisha kwa Udini,ukabila,ukanda,Umimi na Ubinafsi katika kujadili mambo nyeti ya Kitaifa.

Aidha Watu wanaojipofisha jicho la kulia na kuacha la kushoto kuangalia mambo mabaya tu hawawezi kuitwa 'Great Thinkers' kama wanavyojidanganya Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Mitandao ya Kijamii.

Naam! Ndugu wapendwa, kabla ya kusogeza Mguu mbele, naomba kusema kuwa, ni Ibara ya 18(a)ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inayonipa haki ya kuandika Makala hii kwani Ibara hiyo inatoa Uhuru wa Mtu kutoa Mawazo na Fikra zake kuhusu Nchi yake

Ndiyo! nimeamua kuandika Makala hii kutokana na maoni na michango mbalimbali iliyotolewa na Waumini wa CHADEMA katika Mtandao wa Jamiiforums ambapo walikuwa wakichangia Makala iliyoandikwa na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Khamisi Kigwangalla. Michango na maoni hayo ni Ushahidi tosha kwamba CHADEMA inawahujumu Watanzania na Taifa kwa Ujumla.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 30,May 2013, Mbunge wa Jimbo la Nzega,Mkoani Tabora, Dk. Kigwangwalla aliandika Makala katika Mtandao wa Jamiiforums. Katika Makala hiyo Dk. Kigwangalla alieleza Matatizo mbalimbali yanayolikabili Taifa letu huku akipendekeza njia mbadala kuyakabili Matatizo hayo.Kubwa zaidi Dk. Kigwangalla aliwataka Watanzania kubadilika Kifikra huku akisema kuwa,"Uoga wa kubalika ni sumu kwa Wapenda Maendeleo". Ngoja niendelee kumnukuu Mbunge huyo ili kwayo Maoni yake yaweze kulinganishwa na kile kilichochangiwa na 'Wanamagwanda'.

"Napenda kuona Watanzania, Sote kwa pamoja tukibadilika kifikra. Tuanze kuwa Wabunifu zaidi, wenye Uthubutu,Wachapa kazi, Waaminifu, kuweka mbele Uzalendo kwa faida ya wote badala ya Umimi zaidi kwa faida yangu. Napenda kuona Watanzania Wenzangu tukizaliwa Upya leo na kuanza nguvu mpya leo ya kuleta mabadiliko ya kifikra na Kiutendaji. Tuondoke kwenye Umbumbumbu wa kuamini kuwa,kila kitu kitaletwa na Serikali. Tuanze kuamini kuwa, tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kuchukua hatua sahihi katika maisha yetu binafsi na katika jamii yetu. Tuanze kuamini vingine kuwa, tunaweza kuamua kuibalisha Nchi yetu sisi wenyewe na kutoka hapa tulipo leo na kuingia Dunia nyingine kabisa kiuchumi na kijamii".

Bila shaka Mawazo yaliyoandikwa katika Makala hiyo ni ya kupongezwa,kuungwa mkono,kuhamasishwa na kufanfanyiwa kazi kwa Watu wenye Ujenzi wa Fikra kwani Mwandishi wa Makala hiyo ameonekana kuandika kwa hisia kali na hivyo kudhihirisha kuwa, ameguswa na kukerwa na matatizo yanayolikabili Taifa letu. Hongera sana Kigwangalla.

Lakini tazama! hali inakuwa tofauti kwa Wafuasi wa CHADEMA,baada ya kuunga mkono,kuhamasisha na kufanyia kazi mawazo hayo, wametumia Wino wao kubeza na kutweza mawazo hayo kwa kuwa tu yamesemwa na Mtu wa CCM. Yangesemwa na Kiongozi wa CHADEMA yangekuwa lulu. Huu ni Uzandiki wa Fikra unaoweza kuliangamiza Taifa letu kwa Misingi ya Uchama, Ubinafsi na Umimi na kwamba vitendo hivi vya hovyo hufanywa na Wasomi Uchwara na Wanasiasa Makapi wasiolitakia Taifa mema na haya ni matokeo ya kushindwa kujenga hoja na kutumia hoja za nguvu kuyafanya mambo yao yakubalike.

Aidha, ni bora kuwasilisha kwenu baadhi ya michango na maoni ya baadhi ya Wanamtandao huo wa Jamiiforums ambao mara nyingi wanajitambulisha na kujigamba kwa Uchama badala ya Utaifa kama ifuatavyo:

Mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Steven Robert Masatu amesema "Huwezi kuhubiri Fikra mbadala ilihali wewe upo kwenye fikra mgando. Mkuu toka kwanza huko uliko( CCM)". Evi ni kweli kwa mfano si sahihi kwa mnyonge kuwatetea wanyoge wenzake kwa kuwa tu naye ni Mnyoge? kama hivyo ndivyo basi Mwalimu Nyerere asingeliwatetea Watanzania maana alikuwa Mnyonge, kama si upotoshaji nini?.Ingawa hata hivyo Kigwanga haonekani kuwa na Fikra mgando maana aliyoyanena hapo hunenwa na wachache tu.

Nderingosha kama anavyojitambulisha katika Mtandao huo amesema "Hizi Makala ungekuwa unawaandikia Wabunge wenzako wa CCM maana wao ndio wanatakiwa kubadilika kifikra na siyo Wananchi". Huu ni ukweli au kuwahujumu Watanzania?

Vilevi Meningits amesema kuwa "Badiliko la kwanza ni kuitoa CCM mwaka 2015" huku akifuatiwa na mwenzake anayejitambulisha kwa jina la Verified na kusema kuwa, "Tatizo ni CCM" hawa ndio wasomi wetu wanaoyaangalia mambo kwa jicho moja tena la kushoto. Ewe Mwenyezi epusha janga hili katika Taifa letu.

Hivyo,Wachangiaji hawa wanne ni wachache kati ya Wengi wanaojitambulisha kwa Uchadema katika mtandao huo wa kijamii ambao wanaonekana kukifia chama kuliko Taifa, kupinga 'Constructive Ideas' kwa sababu tu yamesemwa na Mtu wa CCM na kuyaangalia mambo kwa jicho la kushoto huku wakiziba la kulia wasione mazuri. Huku ni kulitafuna Taifa kwa Misingi ya Uchama, Umimi na Ubinafsi.

Nisingependa kumaliza makala hii pasi na kuwashauri viongozi wa CHADEMA na Wafuasi wake kuwa, wawe tayari kulifia Taifa kuliko Chama, Wawaunge mkono viongozi wetu pale wanapokuja na mikakati ya kuljenga Taifa,kuwapa moyo viongozi wetu kwa mawazo yao pale yanapoonekana ni ya tija kuliko kuwabeza, tweza na kuwakatisha tamaa kwani kufanya hivyo kwaweza kupelekea viongozi wetu kujihusisha na malumbano badala ya kusisimamia shughuli za kimaendeleo na hatimaye kulipeleka Taifa kwenye Mdomo wa Mamba. Kwa faida ya nani?

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Ninaitwa BAKARI MADAYA (Mwanatunduru).
Ninapatikana simu: 0789357823 au barua pepe madayabakar@hotmail.com

Bwana Bakari inaonyesha wewe ni kati ya watu makini katika nchi hii ila unatatizo la kujishau haraka. umenukuu Ibara ya 18(a)ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo iliyokupa haki ya kuandika Makala hii kwani Ibara hiyo inatoa Uhuru wa Mtu kutoa Mawazo na Fikra zake kuhusu Nchi yake, unafikiri watu wengine hiyo Ibara haiwahusu?. Wametumia Ibara hiyohiyo kusema hayo waliyo sema kama hukubaliani nao hilo ni swala lingine.

Unasema CHADEMA ni wabaguzi!. kama nilivyo ainisha hapo JUU unajisahau haraka, kwani hujui kwamba ubaguzi ni kosa la jinai hapa nchini kwa mujibu wa katiba yetu? aliyeaminiwa na wananchi kusimamia sheria na mambo yanayo husu nchi ni CCM Kigwangala ni mbunge wake huo ubaguzi hawauoni? kama upo kwanini hatua hazichukuliwi?. Najaribu kukuonyesha kuwa na wewe unataka kufia chama chako badala ya taifa kwa kuendekeza propaganda za kisiasa.

Kupuuza maoni ya Kigwangala ni kutokana na mambo yalivyo ndani ya chama chake, hata angekuwa na mawazo mazuri kiasi gani hayawezi kufanyiwa kazi ni sikio la kufa. We fikiria kitu kama kodi ya SIMCARD alishiriki kupitisha kwa kishindo halafu unataka tuamini maneno yake.

Kabla ya kuwashauri viongozi wa CHADEMA kuwa tayari kulifia taifa lao kwanza tutajie viongozi wa CCM walio tayali kulifia taifa. Unapo sema wawaunge mkono wanapokuja na mkakati wa kujenga taifa wengi hatukuelewi unamaanisha nini hasa. Maana viongozi wengi wa CCM kama sio wote ni mafisadi huo mkakati wa kujenga taifa utatoka wapi Rafiki yangu Bakari?. Angalia EPA, RICHMOND, MEREMETA, WANYAMA HAI KUUZWA NJE KINYEMELA, WIZI WA NAURI YA RAISI, WIZI WA HELA ZA MIKUTANO MBALMBALI, MIGODI KUWA NA MIKATABA MIBOVU, RADA, KUPANGA MATOKEO YA WANAFUNZI MEZANI BADALA YA MATKEO HALISI, POLISI KUBAMBIKIA WANANCHI KESI, MADAWA YA KULEVYA, VIONGOZI WA CCM KUWA MAJANGILI ni mengi mengi nani anafia taifa lake huko?
 
Kila mnapozungumzia udini,ukabila na ukanda mnanikumbusha ile video ya Lipumba(CUF) akikiri kumsaidia Kikwete(CCM)kuupata uraisi!Kweli Chadema imewashika pabaya!

ukitaka kujua kigwangalla ni mtu mnafiki na aaiyejiamini kwa nini ameshindwa kusema udini unao hubiriwa una hubiriwa kwa dini gani? anaogopa kutaja hiyo dini kwakuwa atasemwa anapiga dini hiyo vita?.

Anasema tuna hubiri ukabila kwanini ameshindwa kulitaja hilo kabila? anaogopa nini? anaogopa atasemwa anawafukuza hilo kabila?

kwanini tusiseme HKigwangalla ni mnafiki na muoga tena ni dhaifu?

kwanini ameshindwa kuitaja hiyo kanda? anaogopa watu wa kanda hiyo watasema hawatakiwi?

HKigwangalla ni kiongozi muoga,dhaifu na mnafiki.
 
Last edited by a moderator:
Ujinga mtupu.. wazee wa kodi za line na madawa ya kulevya

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nina mashaka na ufinyu wa fikra za huyu mleta hii mada. Sina uhakika sana kama aliwaza alichokiandika kwani heading na kilichopo ndani ya mada ni vitu viwili tofauti kabisa, naomba asinielewe vibaya kama alivyo kwisha athirika kisaikolojia, kwamba atakae kwenda kinyume na mtazamo wake, basi ni mfuasi wa chadema. Muheshimiwa huyo uliye mtaja ndio kazungumza kile ulicho dhani wewe ni kuleta mshikamano katika kuleta maendeleo, ts ok! lakini ulivyo anza kukishutumu chadema, kwamba ni cha ukanda ukabila sielewi hili linauhusiano gani na mada yako! jingine. Aliyo yazungumza mheshimiwa huyu wewe unaemwamini anaweza kuleta mabadiliko. eti kwa kutoitegemea serikali. hapo hukufikiri mbali kidogo kazi tumekuwa tukifanya tangu hata kabla ya uhuru, lakini bado hali zetu kiuchumi ni mbaya sana kwnini? hii ni kwasababu serekali yetu imefinya fursa, leo hii vijana tupo mitaani hatuna ajira, machinga tunafukuzwa na mgambo wa jiji, garama za vyakula juu, mama ntilie hatuna pa kuumulia mishahara isiyo kimu mahitaji na kodi kubwa huku makaburu wakifurahia resource zetu, kweli hili nalo ni la ukanda? je hili lina dini ya mtu? je hili nalo ni chadema na wafuasi wake wameliasisi? au kwasababu chadema wameifunua nguo serekali kwa kufichua ufisadi mkubwa unaofanywa na serekali ilihali walala hoi tunaongezeka acha ushabiki
 
Shida nyingine hii MED-MTWIRO ! Umefoka povu lakutosha bure. Kumbe unaonekana bado unahitaji elimu ya mapinduzi, hujui watanzania kwanini hawataki uongozi wa CCM na kauli yoyote yenye uzuri kutoka kwao. CHARITY BIGINS AT HOME.. unajua maana ya huu msemo? Kigwangala hajasema chochote kile kipya ndugu yangu MED-MTWIRO, hakuna kitu. Kauli ngapi zamatumaini zimetolewa na Rais: maisha bora, Komputer kwa kila mwanafunzi, kupambana na madawa ya kulevya, kujivua gamba, viwanda, kilimo kwanza, michezo nk. Mizengo nae lukuki. Mkama na siku 90, Mangula na miezi sita. Watende tuone siyo maneno maneno tu...! Sasa wewe unanishawishi nimpongeze Kigwangala kwa kipi kipya usichokijua. Anayoyasema ndiyo maisha tunayoyaishi na kuvurugwa na CCM hasa huo mwenendo wa Mwigulu na siasa zake. Sisi tunachapa kazi kwanguvu kubwa sana na kupata kidogo sana tofauti na nguvu tunazotumia.Hatuulizani Dini wa Kabila. Natumeyasikia maneno hayo kwa zaidi ya miaka 20 sasa bila hata kuyafanyia editing kidogo. Umesahau kuwa tuliambiwa niwavivu wa kufikiri na kutakiwa tuchape kazi kwa juhudi na maarifa? Balaa zaidi umesahau kuwa waTZ siyo wale wezake na Baba yako. Hawa wa sasa siyo wakuwaambia nyeusi ni blue, wanakukatalia kwakusema No. ni nyeusi hivyo umekosea. Sasa wewe unapoambiwa ukweli unaanza eti.. aah. CHADEMA.. Uzandiki..wa fikra... Pole sana ndugu yangu rudini mkajipange upya kabla ya kutoa kaulizenu hadharani fagieni uozo mnaoruka vyumbani mwenu kwanza kisha mje tusemezanane ukumbini Mafisadi/ wezi/ majangili/matapeli/majanga/majambazi/mauza sembe wakubwa nyinyi.
 
Heading yako iko kishabik,nachelea kusema umeandika ujinga yan unachokosoa kwa chadema ndicho umekifanya ndani ya post yako! Pili si kila anayesema haipendi ccm ni cdm! Tatu,ukabila uko wapi? Acha uchochezi!
 
Back
Top Bottom