CHADEMA inavyoliangamiza Taifa!

CHADEMA inavyoliangamiza Taifa!

vijana wa LUMUMBA mkishapewa izo buku 7 mnafanya vitu bilathata kufikiri!!! Sasa unajua ulichokiandika?? Zinduka kijana usiandike habar bila utafit!! Huweo utumbo apa sio mahali pake peleeka FB
 
bastola chadema

ffffffffffffffffffff.jpg
 
Najaribu ku avoid hawa watu wa buku 7 toka Lumumba.When you argue with a fool you will become a fool.
Niishia hapa maana sitaki kuwa juha kuwa na dialogue na huyu mwenye thread.
 
Mwenye asili aachi asili, ukabila, udini, na umimi hiyo ndio asili Yao CHADEMA.
 
Mimi sijasoma makala yako ila kichwa cha habari tu kinatosha kunifanya nitoe mchango wangu. Hivi unavyosema chadema kinaangamiza taifa una maana gani? Chadema ndo kinaongoza serikali? Jamani watanzania hizi siasa za ubaguzi tutaacha lini? Badala ya kuishukuru Chadema inavyoisukuma seriakali kuboresha maisha ya walalahoi ninyi mmekalia ujinga na majungu tu.

hata kama nikikueleza hutajua kwasababu umekaa kubisha tu na kwamba haupo tayari kupokea mapya
 
watu wanaangalia issues kama vile
kumwagia watu tindikali
kulisha watu sumu
kujilipua kwa mabomu nk. hayo unayowadanganya watu eti kuisukuma serikali ni uzushi mtupu
Endelea na list yako basi.....1;Kuuza twiga uarabuni 2;kuiba fedha za umma mkiulizwa mnaziita vijisenti 3:,kuuza unga 4; kung'oa watu kucha,4;EPA,Merermeta,AnnBen,Kagoda,Ndiyoooooooooooooooooo!Wapigwe tu...endelea na list mkuu!
 
Kwa wasiotumia akili wataona umenena lkn ukweli ni kwamba wanawezaje kuliangamiza taifa wakati sio chama tawala? Chama tawala kinafanya nini mpaka taifa linaangalia wenyewe wanaangalia tuu?, CCM ndio wanaoongoza sasa iweje wengine CDM waangamize wao waangalie na kushangilia? mpaka hapo umejichanganya mwenyewe WANAO ANGAMIZA NI CCM:

Kwa jinsi CDM wanavyobambikiwa kesi ni wazi kabisa wakifanya makosa ndio kaburi lao. hiyo tu inaonyesha kuwa wako makini. kama wangekuwa wanauza unga wangeshafia jela siku nyingi maana wasingehangaika na kesi za kubambikia.

Ukiona mtu ambaye wewe unamdharau halafu anahesimiwa na kupendwa na watu zaidi yako basi ujue wewe Thamani yako ni ndogo kuliko ya huyo unayemdharau. WACHENI CDM ipendwe, iheshimiwe na kuthaminiwa na watu hata kama nyie CCM hamuipenda kinawauma nini?
 
watu wa buku saba wanaongezeka kupata hela ya kulipia kodi ya simu[/QUOTE
Kama hiyo ni kweli afadhali ya mimi kuliko wewe unayetumika kumnufaisha Padri Slaa peke yake na Mradi wa UVIWASU, unaujua? amekwapua mamilioni ya Fedha. Upo tayari kuhabarishwa?
 
Kwa wasiotumia akili wataona umenena lkn ukweli ni kwamba wanawezaje kuliangamiza taifa wakati sio chama tawala? Chama tawala kinafanya nini mpaka taifa linaangalia wenyewe wanaangalia tuu?, CCM ndio wanaoongoza sasa iweje wengine CDM waangamize wao waangalie na kushangilia? mpaka hapo umejichanganya mwenyewe WANAO ANGAMIZA NI CCM:

Kwa jinsi CDM wanavyobambikiwa kesi ni wazi kabisa wakifanya makosa ndio kaburi lao. hiyo tu inaonyesha kuwa wako makini. kama wangekuwa wanauza unga wangeshafia jela siku nyingi maana wasingehangaika na kesi za kubambikia.

Ukiona mtu ambaye wewe unamdharau halafu anahesimiwa na kupendwa na watu zaidi yako basi ujue wewe Thamani yako ni ndogo kuliko ya huyo unayemdharau. WACHENI CDM ipendwe, iheshimiwe na kuthaminiwa na watu hata kama nyie CCM hamuipenda kinawauma nini?

Chadema wanaliangamiza Taifa kwa kuwahujumu Wananchi kwa Propaganda zao kwa Maslhi binafsi. Kwa mfano tarehe 1 juni Padri Slaa
 
Umeandika utumbo mrefu sana bila sababu. Taifa linaangamizwa na ccm na serikali yake kwa kung'ang'ania madaraka, kuendekeza rushwa na ufisadi, kutawala bila sheria, kukiuka katiba ya nchi, kujali maslahi ya watawala na mafisadi huku hakuna nia yoyote ya dhati ya kujali tabu za wa tanzania wa chini, na kung'ang'ania madaraka kwa miaka hamsini bila maendeleo. udanganyifu, uwongo, na ulaghai wa serikali kwa wananchi unajenga pengo kubw kati ya wananchi na serikali ya ccm. Mauaji ya raia wasio na hatia na mfumo wa utawala wa kifalme ni tabu kwa Tanzania ya leo na ya kesho.

Taifa hilil linaharibiwa na ccm kwa ujinga ujinga wa viongozi na u mangi meza wenu halafu unasema CDM. CDM kwa sababu inaweka hadharani maovu ya ccm ambayo hampendi yajulikane? CDM ambayo inawafungua watu macho na kuwapa elimu sahihi ili wajue haki zao za kiraia na kikatiba? CDM inaharibu nchi kwa sababu inakubalika kwa wananchi kuliko ccm? CDM inaharibu nchi kwa kuwa inaonekana kuwa na watu makini wenye uwezo wa kuratibu mipango bora, uitekeleza na kuisimamia ili kuboresha maisha ya wanyonge ambao ndio wengi?? Uharibifu huo ni kwa sababu sasa wananchi wengi wanapay attention kwa CDM kuliko ccm na mambo yake mafu?

WHAT YOU ARE NOT TRYING TO SAY NI UWEZO MDOGO WA CCM WA KUKABILI WIMBI LA USHINDANI TOKA CDM, NA KWA KUKOSA UBUNIFU WA KISIASA, MNATUMIA MABAVU NA FUJO AMBAZO ZINAHARIBU DIRA NZIMA YA NCHI NA KUANGAMIZA MAELFU YA WATANZANIA. WATANZANIA WANAKOSA MWELEKEO WANAZIDI KUWACHUKIA. UHARIBIFU WA NCHI UTAKWISHA TU PALE CCM MTAKAPOONDOLEWA MADARAKANI KWA NAMNA YOYOTE INAYOWEZEKANA. TULMECHOKA
 
Mimi sijasoma makala yako ila kichwa cha habari tu kinatosha kunifanya nitoe mchango wangu. Hivi unavyosema chadema kinaangamiza taifa una maana gani? Chadema ndo kinaongoza serikali? Jamani watanzania hizi siasa za ubaguzi tutaacha lini? Badala ya kuishukuru Chadema inavyoisukuma seriakali kuboresha maisha ya walalahoi ninyi mmekalia ujinga na majungu tu.

hii ndo akili mgando. Mleta mada kabainisha kwa hoja zilizo wazi kabisa jinsi wanamagwanda wanavyoleta ubaguzi kwa kuendekeza uchama tu hata kwa mambo yaliyo wazi.Siwezi kusema chadema ni janga bali wanamagwanda wanaoichafua hapa kwa kubisha hata kwa mambo ya wazi.
 
Kwa kawaida watu makini hawaongozwi na Ubinafsi katika kujadili masuala mbalimbali muhimu ya kitaifa. Hawasukumwi na Umimi, ukabila, ukanda na Udini katika kutoa michango na maoni katika ujenzi wa Taifa, hali ipo tofauti kwa Waumini wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wanajitambulisha kwa Udini,ukabila,ukanda,Umimi na Ubinafsi katika kujadili mambo nyeti ya Kitaifa.

Aidha Watu wanaojipofisha jicho la kulia na kuacha la kushoto kuangalia mambo mabaya tu hawawezi kuitwa 'Great Thinkers' kama wanavyojidanganya Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Mitandao ya Kijamii.

Naam! Ndugu Wapendwa, kabla ya kusogeza Mguu mbele, naomba kusema kuwa, ni Ibara ya 18(a)ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inayonipa haki ya kuandika Makala hii kwani Ibara hiyo inatoa Uhuru wa Mtu kutoa Mawazo na Fikra zake kuhusu Nchi yake. Hivyo naomba ieleweke kuwa, natekeleza ibara hiyo.

Ndiyo! nimeamua kuandika Makala hii kutokana na maoni na michango mbalimbali iliyotolewa na Waumini wa CHADEMA katika Mtandao wa Jamiiforums ambapo walikuwa wakichangia Makala iliyoandikwa na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Khamisi Kigwangalla. Michango na maoni hayo ni Ushahidi tosha kwamba CHADEMA inawahujumu Watanzania na Taifa kwa Ujumla.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 30,May 2013, Mbunge wa Jimbo la Nzega,Mkoani Tabora, Dk. Kigwangwalla aliandika Makala katika Mtandao wa Jamiiforums. Katika Makala hiyo Dk. Kigwangalla alieleza Matatizo mbalimbali yanayolikabili Taifa letu huku akipendekeza njia mbadala kuyakabili Matatizo hayo.Kubwa zaidi Dk. Kigwangalla aliwataka Watanzania kubadilika Kifikra huku akisema kuwa,"Uoga wa kubalika ni sumu kwa Wapenda Maendeleo". Ngoja niendelee kumnukuu Mbunge huyo ili kwayo Maoni yake yaweze kulinganishwa na kile kilichochangiwa na 'Wanamagwanda'.

"Napenda kuona Watanzania, Sote kwa pamoja tukibadilika kifikra. Tuanze kuwa Wabunifu zaidi, wenye Uthubutu,Wachapa kazi, Waaminifu, kuweka mbele Uzalendo kwa faida ya wote badala ya Umimi zaidi kwa faida yangu. Napenda kuona Watanzania Wenzangu tukizaliwa Upya leo na kuanza nguvu mpya leo ya kuleta mabadiliko ya kifikra na Kiutendaji. Tuondoke kwenye Umbumbumbu wa kuamini kuwa,kila kitu kitaletwa na Serikali. Tuanze kuamini kuwa, tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kuchukua hatua sahihi katika maisha yetu binafsi na katika jamii yetu. Tuanze kuamini vingine kuwa, tunaweza kuamua kuibalisha Nchi yetu sisi wenyewe na kutoka hapa tulipo leo na kuingia Dunia nyingine kabisa kiuchumi na kijamii".

Bila shaka Mawazo yaliyoandikwa katika Makala hiyo ni ya kupongezwa,kuungwa mkono,kuhamasishwa na kufanfanyiwa kazi kwa Watu wenye Ujenzi wa Fikra kwani Mwandishi wa Makala hiyo ameonekana kuandika kwa hisia kali na hivyo kudhihirisha kuwa, ameguswa na kukerwa na matatizo yanayolikabili Taifa letu. Hongera sana Kigwangalla.

Lakini tazama! hali inakuwa tofauti kwa Wafuasi wa CHADEMA,baada ya kuunga mkono,kuhamasisha na kufanyia kazi mawazo hayo, wametumia Wino wao kubeza na kutweza mawazo hayo kwa kuwa tu yamesemwa na Mtu wa CCM. Yangesemwa na Kiongozi wa CHADEMA yangekuwa lulu. Huu ni Uzandiki wa Fikra unaoweza kuliangamiza Taifa letu kwa Misingi ya Uchama, Ubinafsi na Umimi na kwamba vitendo hivi vya hovyo hufanywa na Wasomi Uchwara na Wanasiasa Makapi wasiolitakia Taifa mema na haya ni matokeo ya kushindwa kujenga hoja na kutumia hoja za nguvu kuyafanya mambo yao yakubalike.

Aidha, ni bora kuwasilisha kwenu baadhi ya michango na maoni ya baadhi ya Wanamtandao huo wa Jamiiforums ambao mara nyingi wanajitambulisha na kujigamba kwa Uchama badala ya Utaifa kama ifuatavyo:

Mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Steven Robert Masatu amesema "Huwezi kuhubiri Fikra mbadala ilihali wewe upo kwenye fikra mgando. Mkuu toka kwanza huko uliko( CCM)". Evi ni kweli kwa mfano si sahihi kwa mnyonge kuwatetea wanyoge wenzake kwa kuwa tu naye ni Mnyoge? kama hivyo ndivyo basi Mwalimu Nyerere asingeliwatetea Watanzania maana alikuwa Mnyonge, kama si upotoshaji nini?.Ingawa hata hivyo Kigwanga haonekani kuwa na Fikra mgando maana aliyoyanena hapo hunenwa na wachache tu.

Nderingosha kama anavyojitambulisha katika Mtandao huo amesema "Hizi Makala ungekuwa unawaandikia Wabunge wenzako wa CCM maana wao ndio wanatakiwa kubadilika kifikra na siyo Wananchi". Huu ni ukweli au kuwahujumu Watanzania?

Vilevi Meningits amesema kuwa "Badiliko la kwanza ni kuitoa CCM mwaka 2015" huku akifuatiwa na mwenzake anayejitambulisha kwa jina la Verified na kusema kuwa, "Tatizo ni CCM" hawa ndio wasomi wetu wanaoyaangalia mambo kwa jicho moja tena la kushoto. Ewe Mwenyezi epusha janga hili katika Taifa letu.

Hivyo,Wachangiaji hawa wanne ni wachache kati ya Wengi wanaojitambulisha kwa Uchadema katika mtandao huo wa kijamii ambao wanaonekana kukifia chama kuliko Taifa, kupinga 'Constructive Ideas' kwa sababu tu yamesemwa na Mtu wa CCM na kuyaangalia mambo kwa jicho la kushoto huku wakiziba la kulia wasione mazuri. Huku ni kulitafuna Taifa kwa Misingi ya Uchama, Umimi na Ubinafsi.

Nisingependa kumaliza makala hii pasi na kuwashauri viongozi wa CHADEMA na Wafuasi wake kuwa, wawe tayari kulifia Taifa kuliko Chama, Wawaunge mkono viongozi wetu pale wanapokuja na mikakati ya kuljenga Taifa,kuwapa moyo viongozi wetu kwa mawazo yao pale yanapoonekana ni ya tija kuliko kuwabeza, tweza na kuwakatisha tamaa kwani kufanya hivyo kwaweza kupelekea viongozi wetu kujihusisha na malumbano badala ya kusisimamia shughuli za kimaendeleo na hatimaye kulipeleka Taifa kwenye Mdomo wa Mamba. Kwa faida ya nani?

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

.
Ninapatikana simu: 0789357823




Hauwezi na haiwezekani kwa mtu kama wewe kujiita Great Thinker wakati hauna jipya kwenye akili yako,kila wakati mnajadili CHADEMA hamna matukio ambayo ni tatizo kwenye taifa letu?

Vijana wanaojiona wao wasomi mawazo yao siku zote ni kuitangaza Chadema wakati hizo kazi za Uenezi kuna watu walioajiriwa maalum kwa kazi hiyo,lakini kwa watu kuwa na single face kama umeme ni kujadili Chadema inaonekana Chadema kinawanyima watu usingizi sana nchi hii hasa Vibaraka ambao hukesha humu jf kuandika siasa za maji taka,zitawasaidia nini?

Ifikie wakati mjadili matatizo na sio kujadili watu,unakuta mtu mzima na makengele yake anamjadili Dr Slaa,Mbowe,Mshumbusi,Lissu na anachojadili ni uongo,uzushi na umbea,

Tanzania imekuwa nchi ya vijana wambea wenye majungu,wasiopenda kazi,walalamishi ndio maana wanatumiwa kusafirisha madawa [Drug Muller] sababu hawataki kuumiza kichwa kufikiria afanye nini yeye anataka maisha rahisi,na njia za mkato,kama kumeza pipi,kupanda ndege hata kama anaenda kukamatwa hajui,

Vijana tujitambue,majungu,fitina,uongo kusema watu sio suluhisho la maisha magumu uliyonayo

Amka ujitambue
 
Mtoa mada kama uko CDM ondoka humo utafute chama kingine kitakachokufaa. Jaribu kujiunga na ccm ambao wanapitisha kodi ya kutuma pesa kwenye simu, intaneti kwenye simu, whatsApp kwenye simu, kuongeza kodi kwenye muda wa kupiga simu, na kodi kwenye sim card. Walipitisha hayo Bungeni kwa kishindo na kupiga meza wakati Wabunge wenzao wa CDM na NCCR wakisusia kwa kutoshiriki dhuluma. Sheria waliyoipitisha ilipoanza kutekelezwa upepo ukaanza kuwavumia vibaya ccm, wakaanza kukilaani (kupitia Nape) kitu walichokipitisha kwa kishindo na sasa wanataka eti kodi ya simcard tu (ambayo ni ndogo ukilinganisha na hizo nyingine nilizozitaja) ndio iondolewe. Hizo nyingine nilizozitaja hapo juu hawazisemi, kwa maana ziendelee. Kama sio kutuzuga ni nini? Kajiunge kule pengine utapewa buku 7 kwa uchafuzi kama wenzako wa humu.
 
Back
Top Bottom