Mantissa
JF-Expert Member
- Jul 24, 2010
- 876
- 168
Katibu mkuu wa CHADEMA taifa kwa sasa yuko hoi bin taabani kuongoza chama chake, ambacho hivi karibuni kiliweza kujizolea sifa hapa nchini, kwa kile kinacho daiwa kuwa kiliweza kutoa changamoto kubwa kwa chama tawala (CCM).
Jambo la kushangaza na kushtua kuhusu hiki chama, ni kuporomoka kwa umaarufu wake nchini, baada ya watanzania kugundua kuwa sio chama cha 'demokrasia' na 'maendeleo' kama wanavyo jipambanua, ila ni chama cha vurugu, fujo na maandamano yenye kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.
Sifa hizi mpya kwa chama hiki, ambazo ni fujo na vurugu, zimetolewa na wananchi baada tu ya CHADEMA kumpa mamlaka Dr Slaa ya kuwa mtendaji mkuu wa chama hicho, Dr Slaa kwa siasa na mbinu zake, alidhani kwa kutumia maandamano basi ndio itakuwa njia pekee ya kuzidi kuinua jina na hadhi ya chama, kumbe imekuwa kinyume chake.
Mikakati ya Dr Slaa ya kuleta mageuzi ya siasa hapa nchini kupitia chama chake (CHADEMA) na washirika wake IMEDODA, na badala yake mikakati hiyo imefanikiwa kuondoa na kutokomeza kabisa sentensi isemayo "Tanzania ni kisiwa cha amani", na kwa sasa kuwa kisiwa cha wahanga wa mabomu.
Hoja ya msingi hapa ni kwamba, kama Dr Slaa amechemka na yuko hoi kuiongoza CHADEMA kwenye kufanya siasa za kistaarabu na safi. Je, atawezaje kuongoza nchi yetu yenye changamoto za kila aina?, haya ni mambo ya msingi sana kuhoji, kwani kushabikia uozo ambao utaenda kuliangamiza taifa sio UZALENDO hata kidogo.
Mheshimiwa, mbona hiki chama kinaendelea kuwanyang'anya kata nyingi tu kama watanzania hawakipendi? au ni maoni yako tu bila kuwa na taarifa sahihi?
Mi nadhani siku vyombo vya dola vikiacha kutumia nguvu katka chaguzi, ndo pale tutaconfirm kuwa hiki chama hakipendwi. Lakini kwa saa hz, CCM haiko akilini mwa watu kabisa, isipokuwa watawala na familia zao tu. Huu ndo ukweli kaka.