CHADEMA inashiriki Uchaguzi Kinondoni, Siha na Kata Nane

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Taarifa nilizozipata kutoka katika chanzo cha kuaminika ndani ya CHADEMA zimenithibitishia kuwa taarifa kuwa CHADEMA Wamejitoa kushiriki katika uchaguzi wa marudio ktk Majimbo ya Kinondoni na Siha pamoja na Kata si za kweli.

Kwa kuongezea tu ni kuwa, Timu ya Kampeni ya CHADEMA inaendelea kufunga kampeni katika maeneo mbalimbali na kule Jimbo la Siha, CHADEMA wanafunga kampeni zao eneo la Ngaranairobi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, John Mrema( Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA) ameandika ujumbe ufuatao;

Screenshot from 2018-02-16 16-11-02.png

''Kuna barua inasambazwa kwenye Mitandao kuwa CHADEMA imejitoa kwenye uchaguzi WA Majimbo ya Kinondoni na Siha.

Hizi ni propaganda dhaifu za waliokwisha kushindwa hasa baada ya Kujuwa kwa uhakika baada ya kikao Chao cha tathimini Jana kuwa wananchi hawatawachagua na wanafanya hivi kuwakatisha tamaa wapiga kura ili wasijitokeze kesho kupiga kura.

Wapuuzeni Hao, Aidha walivyo dhaifu hawajui hata utaratibu kuwa Ni Mgombea tu ndio mwenye haki ya kuandika barua ya kujitoa na sio M.kiti wa Chama.

Mwenyekiti Mbowe anafunga kampeni Kinondoni Muda huu na Mzee Lowassa anafunga Kampeni Siha Muda huu''

____________

Ahsanteni!

=======

Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amesema;

Kuhusu habari za kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHAADEMA) kimejitoa kushiriki uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Kinondoni, Siha na kata nane;

1. Ni uzushi unaosambazwa na watu ambao wameona dalili za kushindwa uchaguzi huo, hivyo wanafanya mbinu za kuuhadaa umma wa Watanzania hususan wapiga kura ili wasijitokeze kwa wingi kupiga kura hapo kesho Februari 17, 2018.

2. CHADEMA inashiriki Uchaguzi katika maeneo hayo na itaibuka mshindi.

3. Tunatoa wito kwa Watanzania wote na hasa wapiga kura wa majimbo hayo na kata hizo kuzipuuza hadaa hizo badala yake wajitokeze kwa wingi kesho kutumia HAKI YAO YA KIKATIBA kwenda kupiga kura kwa wagombea wa CHADEMA kwa ajili ya MABADILIKO.

4. Muda huu Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe anaongoza mkutano wa kufunga kampeni za kumnadi mgombea wa CHADEMA Jimbo la Kinondoni, Ndugu Salum Juma Mwalim huku Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Mhe. Edward Lowassa akiongoza timu nyingine katika Jimbo la Siha kumnadi mgombea wa CHADEMA Ndugu Elvis Christopher Mossi na viongozi wengine waandamizi wa chama wakiongoza mashambulizi ya mwisho kuwanadi wagombea wa udiwani katika kata hizo nane.

4. Chama kitamwandikia barua Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili ichukue hatua dhidi ya chama na mgombea wake ambao wanasambaza uzushi huo mitandaoni, kwa sababu kitendo hicho ni kinyume cha Sheria ya Uchaguzi na kanuni zake.

5. Tunasisitiza tena kuwaomba wapiga kura wote kukumbuka kuwa kesho Jumamosi. Februari 17, 2018 ndiyo siku ya kupiga kura, wajitokeze kwa wingi kuwachangua wagombea wa CHADEMA.

Makene
 
CCM wamekabwa koo, wamejaribu kufanya figisu ya kutowaapisha mawakala wakastukiwa sasa wanatapatapa.
 
Back
Top Bottom