CHADEMA Inaongoza nchi Indirectly

Hata katiba mpya yenyewe haikuwepo kwenye Sera za CCM ndiyo maana hata waziri wa sheria yule mwanamama sijui anaitwaga nani alishatoa tamko la Serikali hadharani kwamba Serikali ya CCM haina mpango wa kuandika katiba mpya kwani iliyopo haina matatizo lakini baadaye wakaona sera zao ni za kipumbavu ikabidi warudi nyuma waangalie sera za Chadema then Rais akaamua huu mchakato uanze mara moja.

Via Mobile
sera za kipumbavu ni zile za kutembea na sumu hadi bar ili uwekee wenzako kwenye vinywaji
 
Kweli hata kipindi kile CHADEMA walipoweka shinikizo bungeni hata wakatoka nje, waziri wa sheria alikuwa Celina Kombani akachemsha kwa kupingana kauli na rais. CHADEMA walikwenda ikulu wakaongea na rais umuhimu wa katiba mpya mpaka kimeeleweka!

mkuu pale kwenye red walikwenda kunywa kahawa ya ikulu
 
juice ya ikulu iliwafanya waende ikulu wala sio katiba, angalia vizuri kwenye meza karibu na kwa Dj mbowe
 
sura ya 1 ibara ya 1(4) ya rasimu ya katiba mpya inasema ''tanganyika itaitwa jimbo la tanganyika na zanzibar itaitwa jimbo la zanzibar na kila jimbo litaongozwa na gavana'' hii ni sera ya chadema ya majimbo. Cha kushangaza mwenyekiti wa tume alisema tume haijapendekeza serikali ya majimbo. Nimeamini chadema ndio inaongozahttps://www.jamiiforums.com/usercp.php nchi indirectly.

jamani tuache kutafuta sifaa zisizokuwa na mashiko. Ndio chadema walichagiza kupatikana kwa katiba ila katiba sii ya chadema na walichagiza kwa maslahai yao binafsi which happens to be also maslahi kwa watanzania wote na sifa kwa kikwete. This is win win win situation. Mimi naona unachokitafuta wewe ni win lo0se, loose situation. Hapo meno yotee utakenua.

Sifa mpeni mhe. Rais ni haki yake na kweli anastahili na mwisho msisahau anapenda.. Sasa mpaka sifa mnataka msifiwe nyie chadema that is too selfish.. Nyie ni waanzilishi na wachagizaji be there we need you

rais ana nafasi yake mpeni haki yake. Ccm wanataka katiba ielekee upande wao sasa hapo ndipo chadema mnahitajika. Muda wa kupeana sifa na kugonga glass kwa chadeama bado sanaa na sioni mnakoutoa... Kazeni buti tunataka katiba iliyotulia ya kisasa kama au zaidi ya majirani zetuu kenya
 
Hii inaitwa DHANA YA RASIMU SIFURI YA MAPENDEKEZO YA WADAU KUHUSU KATIBA MPYA YA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA TANZANIA.
mkuu, mbona unapotosha? soma hapa chini
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
SEHEMU YA KWANZA
MIPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA
Jamhuri ya
Muungano 1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.
(2) Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho la kidemokrasia
linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu,
kujitegemea, utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu.
(3) Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika Ibara
ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa
Makubaliano hayo.
Eneo la
Jamhuri ya
Muungano
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara
ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha
sehemu yake ya bahari.
Alama na Siku
Kuu za Taifa 3.-(1) Alama za Taifa ni:
(a) Bendera ya Taifa;
(b) Wimbo wa Taifa; na
(c) Nembo ya Taifa,
kama zitakavyoainishwa katika sheria itakayotungwa na Bunge.
(2) Siku Kuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a) Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
Disemba;
(b) Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12
Januari;
(c) Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili; na
(d) Siku Kuu nyingine zita
ri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa
zifuatazo:
(a) utu;
(b) uzalendo;
(c) uadilifu;
(d) umoja;
(e) uwazi;
(f) uwajibikaji; na
(g) lugha ya Taifa.
SEHEMU YA PILI
MAMLAKA YA WANANCHI, UTII NA HIFADHI YA KATIBA
Mamlaka ya
wananchi 6. Jamhuri ya Muungano ni nchi inayofuata misingi ya
demokrasia inayozingatia haki ya kijamii, na kwa hiyo:
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka za nchi, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi
ambao kwa umoja na ujumla wao wanaimiliki na kuipatia
Katiba hii uhalali;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa
wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi; na
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa
mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Watu na
Serikali 7.-(1) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo
vyake, katika uendeshaji na utekelezaji wa shughuli zake utazingatia
azma ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara ndogo (1), mamlaka
ya nchi na vyombo vyake vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake
zote kwa lengo la kuhakikisha kwamba:
(a) utu na haki nyingine zote za binadamu zinaheshimiwa na
kuthaminiwa;
(b) sheria za nchi zinasimamiwa na kutekelezwa;
(c) Serikali itahakikisha kuwa shughuli zinazofanywa
zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba
utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na
unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na
pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
(d) ardhi ikiwa rasilima
u, heshima na haki nyingine zote za binadamu
zinahifadhiwa na kudumishwa kwa kuzingatia mila na
desturi za kitanzania na kwa kufuata mikataba mbalimbali
iliyoridhiwa na Jamhuri ya Muungano;
(h) mamlaka za nchi zinatoa fursa na haki zilizo sawa kwa
wananchi wote, wanawake na waume, bila ya kujali rangi,
kabila, nasaba, dini au hali ya mtu;
(i) aina zote za dhulma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji,
rushwa, uonevu au upendeleozinaondolewa nchini;
(j) utajiri wa rasilimali na maliasili za Taifa unaelekezwa
katika kuleta maendeleo, kuondoa umaskini, ujinga na
maradhi; na
(k) nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na
kujitegemea.
Mamlaka na
utii wa Katiba 8.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za Washirika wa
Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano, Katiba hii itakuwa sheria
kuu katika Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu yeyote, chombo, taasisi, jumuiya na wakala wowote wa
mamlaka ya nchi na mamlaka binafsi zinao wajibu wa kuzingatia
masharti ya Katiba hii na kuyatii.
(3) Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo
cha dola, ofisa wa Serikali au mtu binafsi ni sharti ufuate na kuendana na
masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba, sheria, mila, desturi
au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na masharti
ya Katiba hii utakuwa batili.
Hifadhi ya
Katiba 9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia
mamlaka ya nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya
(1) ni batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria
za nchi.
(3) Kwa madhumuni ya kuhifadhi masharti ya Ibara ndogo ya (1)
na (2), Serikali itaweka utaratibu wa kuisambaza Katiba hii kwa
wananchi na kuiweka katika mitaala ya elimu ili kuwezesha wananchi
kuifahamu, kuilinda na kuitii.
 
sera za kipumbavu ni zile za kutembea na sumu hadi bar ili uwekee wenzako kwenye vinywaji
Kutembea na sumu si hoja mbona hata machinga wanatembea nazo mitaani tena wakizinadi na vipaza sauti? Hivi na wale wanaong'oa watu kucha na meno bila ganzi ni wa upande gani mkuu?
 
hata hii katiba mpya ilikuwa sera ya CDM tena ya kwanza kabisa katika ilani yao ya uchaguzi ya 2010. Inaruhusiwa copy /paste cha msingi tu mambo yawe mazuri kwa manufaa ya watanzania wote.

Haswaaa.
CCM wanaruhusiwa ku copy na ku paste mazuri ya wenzao
 
Sura ya 1 Ibara ya 1(4) ya Rasimu ya Katiba Mpya inasema ''Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana'' Hii ni sera ya CHADEMA ya Majimbo. Cha Kushangaza Mwenyekiti wa Tume alisema Tume haijapendekeza Serikali ya Majimbo. Nimeamini CHADEMA ndio inaongoza nchi indirectly.

serikali za kidikteta wewe sasa hivi ungekuwa jela, hayo maneno umeyanukuu wapi?
 
Huyu habariyamujini kila anaponijibu kwenye posts zangu naona huwa anajibu kitu tofauti kabisa na anakuwa anajibu haraka sana hata kama Post imeenda shule kiasi gani nikajua labda ananifanyia mimi tu ili kunifanyia fujo humu JF, lakini katika thread hii nimejaribu kufuatilia michango yake katika post za watu tofauti nimegundua ni mpuuzi tu fulani aliyedhamilia kuifanya JF ionekane ni forum ya mahayawani, nimeamua nimuweke rasmi kwenye Ignore list yangu.

Post
Hata katiba mpya yenyewe haikuwepo kwenye Sera za CCM ndiyo maana hata waziri wa sheria yule mwanamama sijui anaitwaga nani alishatoa tamko la Serikali hadharani kwamba Serikali ya CCM haina mpango wa kuandika katiba mpya kwani iliyopo haina matatizo lakini baadaye wakaona sera zao ni za kipumbavu ikabidi warudi nyuma waangalie sera za Chadema then Rais akaamua huu mchakato uanze mara moja.

Majibu
sera za kipumbavu ni zile za kutembea na sumu hadi bar ili uwekee wenzako kwenye vinywaji

Post
Kweli hata kipindi kile CHADEMA walipoweka shinikizo bungeni hata wakatoka nje, waziri wa sheria alikuwa Celina Kombani akachemsha kwa kupingana kauli na rais. CHADEMA walikwenda ikulu wakaongea na rais umuhimu wa katiba mpya mpaka kimeeleweka!

Majibu
mkuu pale kwenye red walikwenda kunywa kahawa ya ikulu

Post
Kweli hata kipindi kile CHADEMA walipoweka shinikizo bungeni hata wakatoka nje, waziri wa sheria alikuwa Celina Kombani akachemsha kwa kupingana kauli na rais. CHADEMA walikwenda ikulu wakaongea na rais umuhimu wa katiba mpya mpaka kimeeleweka!

Majibu
juice ya ikulu iliwafanya waende ikulu wala sio katiba, angalia vizuri kwenye meza karibu na kwa Dj mbowe
 
Kutembea na sumu si hoja mbona hata machinga wanatembea nazo mitaani tena wakizinadi na vipaza sauti? Hivi na wale wanaong'oa watu kucha na meno bila ganzi ni wa upande gani mkuu?

unafikiri mng'oa watu kucha na mtembea na sumu watu wawili tofauti? Ndiye huyo huyo aliyetaka kumwekea kubwa Kabwera sumu ndiye anayetekeleza vitendo hivyo vya kinyama, tusimtafute mchawi mwingine
 
Sura ya 1 Ibara ya 1(4) ya Rasimu ya Katiba Mpya inasema ''Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana'' Hii ni sera ya CHADEMA ya Majimbo. Cha Kushangaza Mwenyekiti wa Tume alisema Tume haijapendekeza Serikali ya Majimbo. Nimeamini CHADEMA ndio inaongoza nchi indirectly.

Yaani MODs hamuoni kwamba rasimu ya Katiba inachezewa kwa ku-editiwa? hakika hili litaufunga huu mtandao na tunaweza kuukosa.
 
Hii inaitwa DHANA YA RASIMU SIFURI YA MAPENDEKEZO YA WADAU KUHUSU KATIBA MPYA YA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA TANZANIA.

VYMOMBO VYA ULINZI TUSAIDIENI HUYU MTU AKAMATWE hii attachment aliyoiweka hapa kuwa ndiyo rasimu ya katiba ni feki huu ni uhaini mkubwa-mjumbe tume katiba mpya.
 
Huyu habariyamujini kila anaponijibu kwenye posts zangu naona huwa anajibu kitu tofauti kabisa na anakuwa anajibu haraka sana hata kama Post imeenda shule kiasi gani nikajua labda ananifanyia mimi tu ili kunifanyia fujo humu JF, lakini katika thread hii nimejaribu kufuatilia michango yake katika post za watu tofauti nimegundua ni mpuuzi tu fulani aliyedhamilia kuifanya JF ionekane ni forum ya mahayawani, nimeamua nimuweke rasmi kwenye Ignore list yangu.

Post

Majibu

Post

Majibu

Post

Majibu
Mkuu huyo hayuko peke yake, ukitaka kuamini nilisemalo angalia hao wanaoni-Reply with Qute hapo juu. Utagundua ni wale wale wa kuwekwa kwenye "ignore list".
 
Mkubwa polepole nilitaka kujua wangapi wamesoma rasimu, ha ha ha.
VYMOMBO VYA ULINZI TUSAIDIENI HUYU MTU AKAMATWE hii attachment aliyoiweka hapa kuwa ndiyo rasimu ya katiba ni feki huu ni uhaini mkubwa-mjumbe tume katiba mpya.
 
chadema walishasema hawamtambui rais kiliwapeleka nini ikulu ndo ujue kwamba walikosa pakutokea ikabidi wakapige magoti.
 
Back
Top Bottom