CHADEMA inamtakatisha Dkt. Hosea kugombea TLS?

CHADEMA inamtakatisha Dkt. Hosea kugombea TLS?

Au wakina Boniface wanajua kuwa yeyote watakaempigia debe hataruhusiwa kushinda na hivyo ushindi kupewa yule ambae ndio hasa wanamtaka?

Amandla.....
 
Kwa ufupi sana

Dkt. Hosea ni moja kati ya watu wanaogombea urais wa TLS.

Aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa PCCB. Katika uongozi wake serikali enzi Rais Kikwete serikali ilikumbwa na kashfa kubwa kumbwa kama EPA, Kagoda, Richmond nk.

Nimeona baadhi ya viongozi (sio chama) wakimpa promo Dkt. Hosea.

Tunataka kujua ni hao viongozi kwa utashi wao binafsi au ni chama kinamtakatisha?

Kama ni chama je, mnatumia vigezo gani kumtakatisha? Ni lini na wapi amekuwa akisimamia yale ambayo watu wenye uchungu na nchi hii wamekuwa wakisimamia?

Ni wapi na lini amewahi kuzungumzia katiba mpya?

Ni wapi amewahi kuzungumzia sheria za hovyo kandamizi kwa demokrasia?

Ni wapi amewahi kuzungumzia uchaguzi 2020 na wizi wa kura?

Na kama itakuwa utashi wa hao viongozi tunawashauri tu jitunzieni heshima.
Ukiwachunguza sana wafuasi wa chadema na chama,utagundua ni watu wasiojua nini wanataka
Siku Mwigulu Nchemba akihamia chadema,watampa tu ugombea urais,
 
Wewe ndio uliyekurupuka. Mwanzo alisema Dr. Hoseah alikuwa AG na alirekebisha baada ya kuelimishwa.

Amandla...
kumbe wew unaangalia kauli ya kwanza,, mim nimeongelea kauli yake ya pili baada ya kutengua ya kwanza... Hapo unaelewa kama aliyeuliza swali alikurupuka kwa kutojua kama kuna marekebisho kwenye kauli ya Pili
 
Back
Top Bottom