CHADEMA inamtakatisha Dkt. Hosea kugombea TLS?

CHADEMA inamtakatisha Dkt. Hosea kugombea TLS?

makorokoro yoote siju EPA siju ESCROW sijui IPTL hakuwa ndio mkamata rushwa mkuu, usabato wake unasaidia nini kama yeye angekua mwanaume angejiuzulu sio analialia tu eti ooh viongozi wangu hawakuwa willing , willing ya mavi kwanini asinge resign hasafishiki huyo kima kwa gia ya usabato
Mbona Unamchukia Mtu wa Mungu.. Basi tuache tunaomwamini waweze kututumikia maana anao weledi wa Kisheria..
 
Dr. Hosea wa nini???
Huyu ndiye aling'olewa na Hayati kwa kushindwa kudhibiti RUSHWA!!!
Isitoshe he is too old to handle the office!
Msando wa nini? hatumtaki kabisa kabisa. Hana msimamo. Kazi kujikomba kwa watawala tu.
 
Yule dogo Hilda? Vipi Kileo? Hao ni wachache niliopata jumbe zao na hii inatoa taswira halisi

Na mimi nimemuona Hilda Newton kweli akimfanyia kampeni. Ingawa sidhani kama ni msimamo wa chama chao, lakini wanafanya kosa kubwa kujaribu kumuuza mgombea yeyote katika uchaguzi ambao kwa kweli hauwahusu. Wangekaa kimya bila kuchagua upande. Hoja ya kuwa Hosea hapendwi na CCM aliyoitoa Boniface Jacob haina mashiko. Wanarudia makosa yale yale ya kumpigia debe Lowassa.

Amandla...
 
Mbona Unamchukia Mtu wa Mungu.. Basi tuache tunaomwamini waweze kututumikia maana anao weledi wa Kisheria..
jibu hoja mkuu,usikimbilie kwenye ucha Mungu. hatuna chuki tunaangalia maslahi ya nchi
 
Wasituchagulie tu huyu anayeitwa Albert Msando. Ni mwanaCCM asiye na chembe ya ubinadamu wala msimamo wala nidhamu wala hoja wala kufikiri wala huruma. Aliamua kujiunga chama chenye vkosi vya wasiojulikana waliowapoteza waandishi wa habari, wanasiasa na kuwapiga risasi wenzao akiwemo Lissu. Itakuwa ni aibu taasisi inayoheshimika kama TLS kuongozwa na Msando.
Tatizo la Serikali ya CCM mtu ata akiwa ana sifaa zoooooote kabisa kabisa....tatizo awe Upinzani au kukosea CCM basi hatakiwi!!
Angalia ysliyotokea kwa Antipas na Shangazi....!!!!
 
Kwa hiyo ni haramu mtu kutoa mawazo yake au kumpigia kampeni mtu anayeamini anaweza yaani unataka watu wasiwe huru kutoa maoni yao? Kama wao wametoa hayo ni kwa utashi wao siyo wa chama chao tangu lini vyama vikaingilia uchaguzi wa chombo huru cha kisheria ambacho chama cha siasa siyo sehemu ya wanachama? Acha watu wawe huru kutoa maoni yao kama hawavunji sheria tu haya mambo ya kuminya watu uhuru ndiyo huleta migogoro isiyo na maana

Kama wao wameona huyu Mzee wa kanisa anafaa na wewe kampendekeze umtakaye simple
 
Waliopitishwa kugombea urais wa TLS ni:
1. Dr. Hoseah.
2. Flaviana Charles.
3. Shehzad A Wall
Kwa kumfanyia kampeni ya wazi Dr. Hoseah kunaonyesha kuwa hao wawili waliobaki hawafai. Ingekuwa vyema kama wangeeleza kwa nini Flaviana Charles na Shehzad A Wall hawafai kushika nafasi hiyo. Kama kosa la Flaviana Charles ni kutaka kugombea ubunge kupitia CCM ( ambayo inaonyesha kuwa ni kada wa CCM) itakuwaje Dr Hoseah akubaliwe ambae nae bila shaka ni kada wa CCM? na kama u kada wa CCM ni tatizo kwa nini wasimpigie kampeni Shehzad Wall. Au kwa nini wasikae kimya tu?

Amandla...
 
wewe endelea kuwa kama kenge mpaka damu itoke masikioni ndio utaelewa,wenzako wamepewa Dolla na Hosea ili wampigie promo ww unabaki kulialia tu hapa
 
Kwa ufupi sana

Dkt. Hosea ni moja kati ya watu wanaogombea urais wa TLS.

Aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa PCCB. Katika uongozi wake serikali enzi Rais Kikwete serikali ilikumbwa na kashfa kubwa kumbwa kama EPA, Kagoda, Richmond nk.

Nimeona baadhi ya viongozi (sio chama) wakimpa promo Dkt. Hosea.

Tunataka kujua ni hao viongozi kwa utashi wao binafsi au ni chama kinamtakatisha?

Kama ni chama je, mnatumia vigezo gani kumtakatisha? Ni lini na wapi amekuwa akisimamia yale ambayo watu wenye uchungu na nchi hii wamekuwa wakisimamia?

Ni wapi na lini amewahi kuzungumzia katiba mpya?

Ni wapi amewahi kuzungumzia sheria za hovyo kandamizi kwa demokrasia?

Ni wapi amewahi kuzungumzia uchaguzi 2020 na wizi wa kura?

Na kama itakuwa utashi wa hao viongozi tunawashauri tu jitunzieni heshima.
Tutashitakiwa MIGA
IMG-20210324-WA0023.jpg
 
CHADEMA sio watu wa kuwaamini hata kidogo. Ni watu maslahi hawajawahi kuwa na uchungu na hili taifa linaloitwa Tanzania
 
Kwa ufupi sana

Dkt. Hosea ni moja kati ya watu wanaogombea urais wa TLS.

Aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa PCCB. Katika uongozi wake serikali enzi Rais Kikwete serikali ilikumbwa na kashfa kubwa kumbwa kama EPA, Kagoda, Richmond nk.

Nimeona baadhi ya viongozi (sio chama) wakimpa promo Dkt. Hosea.

Tunataka kujua ni hao viongozi kwa utashi wao binafsi au ni chama kinamtakatisha?

Kama ni chama je, mnatumia vigezo gani kumtakatisha? Ni lini na wapi amekuwa akisimamia yale ambayo watu wenye uchungu na nchi hii wamekuwa wakisimamia?

Ni wapi na lini amewahi kuzungumzia katiba mpya?

Ni wapi amewahi kuzungumzia sheria za hovyo kandamizi kwa demokrasia?

Ni wapi amewahi kuzungumzia uchaguzi 2020 na wizi wa kura?

Na kama itakuwa utashi wa hao viongozi tunawashauri tu jitunzieni heshima.
Naunga mkono hoja, Hosea hafai bora Flaviana Charles
 
Back
Top Bottom