CHADEMA inaitia hasara Serikali

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Serikali inatakiwa ifike mahali itambue chadema si chama cha kupambana kwa nguvu, Bali ni chama kinacho hitaji mapambano ya kisiasa zaidi, Tujikumbushe kidogo chadema inavyo itia hasara serikali.

1. Chadema imewahi kuyaweka magari ya police barabarani, ndege za kivita angani, na kuamrisha vikosi vyake vya ulinzi na usalama kufanya kufanya mazoezi, usafi, etc na mwisho vikosi vikaambiwa ukuta umaahirishwa.

2. Kuna wabunge wamewahi kukamatwa na kusafirishwa wengine kwa ndege, magari wakifikishwa Dar wanapata dhamana wanakua huru na kesi wanashinda.

3. Wakati serikali inatumia nguvu nyingi kwa lengo la kuua chadema , bila kujua wanafanya kampeni za kukipaisha chama cha demokrasia na mqendeleo bila kujua. Mfano toka aingie madarakani chadema imekua inapata umaarufu kila kukicha na kupata ofa kibao za promo bila gharama yoyote.

4. Chadema imesababisha lipumba ambaye wala siyo mwajiriwa kulipwa pesa nyingi ,kupewa ulinzi kila anako tembelea, kualikwa kwenye matukio mbalimbali etc , ili tuu chadema itengane na CUF.

Fedha ambazo zinatumika kukimbizana na chadema ,tunaomba serikali ifanyie kazi nyingine kama kuwapa wanafunzi mikopo, madawa , kuajiri walimu, madakari etc.

Mwisho nimpongeze anaye run mikakati ya chadema. big up.
 
Nafikiri ndiyo maana afrika tunakuwa nyuma kwenye maendeleo kwa kutumia muda mwingi katika mambo kama hayo.
 
CCM ni sikio la kufa, hata ukiwashauri utaambulia matusi na kejeli. Na bahati mbaya zaidi wamepata M/kiti ambaye hajui mchezo mzima wa siasa za bongo, yeye anadhani kutumia nguvu ndio njia pekee. Amekutana na vichwa Chadema(wabunifu) wenye mbinu lukuki za kucheza na siasa, ukiwazuia huku wanatokea kule.

Awamu hii ndio awamu Lumumba watapata tabu kuliko awamu zote.
 
Kuna kaniambia Chadema wamejumlisha kura za Lowassa Million Sita na za Followers 2.8 Million za Wema sasa wanashangilia ushindi wa 2020!
nani kwa kwambia kura wanapiga malaika. wafuasi wa wema sepetu ndio wapifa kura, 2015 wema sepetu ameisaidia sana ccm kwa kuwashawishi wafuasi wake wampigie magufuli. hili tetemeko tumelileta wenyewe ccm na lazima lipasue misingi ya Lumumba. nasikia kunatokota baada ya kuonekana mamluki wa mkubwa wanataka kuchukua chama.
 
Kuna kaniambia Chadema wamejumlisha kura za Lowassa Million Sita na za Followers 2.8 Million za Wema sasa wanashangilia ushindi wa 2020!

Tunatumia Mahakama kufanya Kampeni.Wapeleekeni Wabunge wetu na siye.ndiyo tunaanza siasa hapo hapo.

Badilikeni CCM, shida siyo CDM shida ulaji wa CCM umepitiliza.Maendeleo hakuna kutwa kucha kukimbizana na Wapinzani. Mnawalipa mabilioni akina Prof Lipumba ili kuvuruga Upinzani unafanya kazi bure.
 
Tunaipenda CCM sio kwa Ubora au utendaji wake Bali kwa udhaifu wa Wapinzani
 
Tunatumia Mahakama kufanya Kampeni.Wapeleekeni Wabunge wetu na siye.ndiyo tunaanza siasa hapo hapo.

Badilikeni CCM, shida siyo CDM shida ulaji wa CCM umepitiliza.Maendeleo hakuna kutwa kucha kukimbizana na Wapinzani. Mnawalipa mabilioni akina Prof Lipumba ili kuvuruga Upinzani unafanya kazi bure.
umanigusa sana mkuu, pesa anayo lipwa lipumba ingeweza kusomesha wanafunzi zaidi ya 1000 chuo kikuu.
 
katika muda wote wa kampeni sikuwahi kusikia kutoka kwa mgombea wa ccm hoja ya kupambana na kufuta vyama vya upinzani na hicho ndio kilinifanya niwapigie ccm kura. sasa kwakuwa wamepoteza dira na sasa wamejikita katika kuminya demokrasia, na kuua upinzani badala ya viwanda naanza kudai kura yangu!
 
safi sana.
 
FB_IMG_1488016871499.jpg
FB_IMG_1488016869170.jpg
FB_IMG_1488016865543.jpg

Baada ya kusikia lowassa Leo anatia timu uwanja wa taifa.. haaaaa
 
Usiloiju ccm wanfitna sana na hamjazibaini bado,,mnachukulia juu juu ila ccm wanaanzisha janga nanyi bila kujua kichwa kichwa mnaingia.. Hapo ndio mnapigwa bao
 
Back
Top Bottom