CHADEMA inaendeshwa "kimagumashi"... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA inaendeshwa "kimagumashi"...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Aug 5, 2012.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hivi karibuni umeibuka mtindo wa CHADEMA kufungua matawi nje ya nchi. Tumesikia mgombea Urais mtarajiwa mh. Zitto Kabwe akishirikiana na mbunge wa Tanzania anayeishi Marekani mh. Leticia Nyerere wakifungua tawi Washington DC. Tawi hili la Washington DC baadae tuliona limepewa zawadi ya gari na mwanachama mkereketwa! Leo kumekuwa na taarifa ya aliyevuliwa ubunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuwa Uingereza kwa ajili ya ufunguzi wa matawi saba ya CHADEMA.

  Ni dhahiri kuwa CHADEMA wameiga utaratibu huo kutoka CCM. Hata hivyo, tofauti na CCM, katika kufanya hivyo CHADEMA imeanzisha utaratibu huo "kimagumashi".

  Kabla CCM haijaanza kufungua matawi nje ya nchi kitu cha kwanza kilikuwa ni kufanya marekebisho ya katiba ili ufunguaji wa matawi hayo ufanyike kwa kufuata katiba ya chama. Ndio maana katika katiba ya CCM sehemu ya tatu, Fungu la kwanza, 22 (1) (i-ii) kuhusu mashina ya chama, inaeleza kuwa kutakuwa na mashina ya ndani ya nchi na nje ya nchi. Katika fungu la pili, 31 (1) (d), imeelezwa kuwa kutakuwa na matawi ya nje ya nchi. Na imeelezwa bayana kuwa matawi hayo yatafunguliwa kwa indhini ya Katibu Mkuu wa chama. Ndani ya katiba ya CCM vikao vyote vya mashina na matawi ya nje ya nchi vimeelezwa kuwa vinafuata utaratubu upi wa uongozi.

  Kwa upande wa CHADEMA, Katiba ya chama sura ya saba 7.2.1 inasema tawi litaundwa katika kila eneo la kijiji, mtaa au Shehiya ya kiutawala katika mamlaka za serikali za mitaa. Hata hivyo kinyume na katiba hii, katika mazingira ya "kimagumashi", viongozi wa CHADEMA wameanza kufungua matawi nje ya nchi! Haieleweki nani anatoa idhini ya matawi hayo kufunguliwa! Haieleweki matawi hayo yanamlolongo gani wa kiuongozi (wanareport kwa nani). Haieleweki nafasi ya viongozi wa matawi hayo katika uongozi wa chama! Kila anayeamua ananyanyuka na kwenda kufungua tawi nchi anayotaka, kwenye marafiki zake, kwa sababu zake!

  Hata hivyo kwa vile mashabiki wa CHADEMA hawajajenga utaratibu wa kuhoji pale viongozi wao wanapoonekana kufanya "magumashi", mashabiki hao wamekuwa wakifurahia tu ufunguzi huu wa matawi.

  Kuna taarifa kwamba kitendo cha Lema kwenda kufungua matawi Uingereza ni kwa ajili ya kumuwahi Zitto asiende pia kuweka kambi yake huko kama alivyofanya Marekani, lakini swali ni je, Zitto na Lema katika huku kuwahiana kwao wanafuata utaratibu upi kikatiba? Haya "magumashi" yao yanakipeleka wapi chama?

  Mimi bado najiuliza, hawa watu wako serious na uongozi wa nchi yetu? Mbona maneno yao na matendo yao havifanani hata kidogo?
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Jumapili njema...
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  noted for further use
   
 6. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 180
  hongera sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah, wengine huwa wanaenda huko kufanya dili la kuibia nchi, hivi unadhani hatukuoni jinsi ulivyo na hofu kuhusu CDM, mimi sijali nani atakuwa mtawala wa kesho, ninachojua ni kuwa nchi kamwe haitapata rais ambaye ni MGANDA, MRUNDI, MKENYA, MDRC,NK; daima atakuwa ni MTANZANIA bila kujali chama, fikiria kupata mtu bora sio chama bora.

  kama ingekuwa ni chama hapa BONGO kuna chama kina sera nzuri kuliko maelezo, njoo kwenye utekelezaji babaaaaaaaa heeeeee!!!!!!!!!!!!!! yaani weee achaaaaaaaaa tu!
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,730
  Trophy Points: 280
  Kazi unayo ifanya ina kuzidi uzito lazima uanguke!
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kama matawi ya Chadema nje ya Tanzania, hayatambuliki kwenye katiba ya chama kuna hoja kubwa ya kujadili. Chama kikianza puuzo kwa katiba iliyojiwekea yenyewe, kinatupa masuali iwapo kitaheshimu katiba ya nchi.
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ni kweli. Tatizo lililopo kama unavyoona mpaka mkurugenzi wa CHADEMA Molemo anaacha kujadili hoja anajadili watu. Hiki ndicho chama kinachotaka watanzania waamini kuwa kinaheshima uongozi wa kisheria na kufuata kanuni!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Wanachofanya mashabiki wa CHADEMA ni kubuni mbinu mbalimbali za kuwatisha na kuzogoa watu ili wasijisikie huru kusema maovu katika chama hicho. Wangekuwa na dola ni dhahiri wangetumia nguvu za dola kufanya hivyo. Hamuonyeshi mfano mzuri. Badala ya kujadili hoja, mnafanya viroja!
  Watanzania wanawaangalia na matokeo yake mtayaona tu.
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Swali ni je, kwanini ufunguzi wa matawi ya CHADEMA nje ya nchi hauheshimu katiba ya chama?
  Mpaka sasa hakuna aliyetoa jibu!
   
 12. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,276
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Sasa wewe ya chadema yanakuhusu nini? Kwako ccm kuna matatizo chungu mbovu,badala ya kuumiza kichwa jinsi ya kurekebisha mapungufu yenu,tayari umeamia chadema.watu wengine ovyo.
   
 13. k

  kibugumo JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mbona CCM inalaani rushwa na kwenye katiba ya TANU inasema RUSHWA ni ADUI WA HAKI NA SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA,lakini sijui ndio wanakula matapishi yao wenyewe,wao rushwa kila mahali wanafisadi nchi hawana hofu ya kuvimbiwa.Hebu tujifunze haya.
  >kidogo chenye kutosha ni bora kuliko kingi kinachobakia.
  >ujinga usio hasara ni bora kuliko elimu isiyo faida.
  >njaa siyo ua ni bora kuliko shibe inayovimbisha.
  >masikini aliye kinai ni bora kuliko tajiri mwenye tamaa.
  Tumuombe mungu atuepushe na hayo.
   
 14. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,450
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mkuu kuna mambo ya msingi zaidi katika katiba ya CCM ambayo hayafuatwi na katiba haijabadilishwa.

  mfano:


  4. IMANI YA CCM.
  Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:
  (1) Binadamu wote ni sawa.
  (2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
  (3) Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.

  Sidhani kama bado CCM inaamini hayo. (1) na (2) kutokana na matabaka yanayojengwa na chama, ambayo ndiyo yanachangia hata migomo ya madaktari na walimu n.k., na kutokana na jinsi wanavyobagua watu wenye itikadi tofauti za kisiasa.

  Hiyo (3) ndiyo kichekesho kabisa.

  5. MADHUMUNI YA CCM.
  Kwa hiyo Malengo na Madhumuni ya CCM yatakuwa yafuatayo:-
  (3) Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.
  (9) Kuona kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia na ya kijamaa.
  (16) Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu na/au upendeleo.

  17. SIFA ZA UONGOZI
  Pamoja na kutimiza masharti ya Uanachama kama yalivyoelezwa katika Katiba, Kiongozi sharti pia awe na sifa zifuatazo:-
  (1) Awe ni mtu aliyetosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa.
  (2) Awe ni mtu anayependa kueneza matunda ya Uhuru kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo
  ya Taifa kwa jumla.
  (3) Awe na sifa nyingine kama zilivyowekwa katika Kanuni zinazohusika (ZIPI?).

  18. MIIKO YA UONGOZI
  Ni mwiko kwa kiongozi:-
  (1) Kutumia madaraka aliyopewa ama kwa ajili ya manufaa yake binafsi au kwa upendeleo, au kwa namna yoyote
  ambayo ni kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo. (UFISADI)
  (2) Kupokea mapato ya kificho, kutoa au kupokea rushwa, kushiriki katika mambo yoyote ya magendo au mambo mengine yaliyo kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo. (UFISADI)
  (3) Miiko mingine ya Viongozi itakuwa kama ilivyowekwa katika Kanuni zinazohusika.

  na kadhalika.

  Haya ni machache tu ambayo ni contradiction na namna CCM ilivyo na inavyoendeshwa kwa sasa.


  Sasa kama chama chako hata imani na madhumuni yaliyomo kwenye katiba yamepitwa na wakati, mambo hayo ya kufungua matawi mbona ni madogo sana. Kama kweli una nia ya kuhakikisha chama kinafanya kila kitu kadiri ya katiba yake, anzia CCM tena kwenye mambo ya msingi zaidi.

  TOA BORITI JICHONI KWAKO KWANZA! Ndipo uone kibanzi kwenye jicho la ndugu yako.
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo hii ndio justification ya viongozi wa CHADEMA kutokufuata katiba ya chama chao!!!
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Aliyekufundusha hayo kakurithisha umasikini, pole sana...
   
 17. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,450
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mkuu, wewe umeileta mada hii hapa kwa kukerwa na kutofuata katiba. Mambo uliyoleta ni mepesi sana kulinganisha na mambo yasiyofuatwa na CCM yaliyo katika katiba yao.

  Hoj ni kuwa kama unakerwa na tabia hiyo kwa CDM, anzia kwako mwenyewe (CCM) kwenye mambo ya msingi zaidi.

  Unapoanza kutupa mawe angalia kama uko ndani ya nyumba ya kioo!

  Vinginevyo ni siasa za maji taka!!
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mkuu, huu ujumbe ungempa Mbowe na vijana wake nadhani ungewafaa sana, maana wao wako mstari wa mbele kuongea makosa ya wenzao. Kumbe wanatakiwa waanze kwanza kujikosoa wenyewe na tabia yao ya kutokuheshimu katiba ya chama chao. Asante sana kwa busara mkuu. Point yako ni babkubwa...
   
 19. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,450
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nadhani ujumbe huu unawafaa CCM ambao wanakosoa vyama vya siasa kwa malengo ya propaganda tu.

  Wao wenyewe wanaacha mambo ya msingi zaidi kama imani, madhumuni, miiko ya uongozi, na hawaoni kama wana wajibu wa kujikosoa.

  Kama thread hii ungeandika "Vyama vya Siasa vyaendeshwa "Kimangumashi" na kutolea mfano vyama mbali mbali, ikiwemo CCM ningeona kama una nia kweli ya kukosoa.
   
 20. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kuna uhusiano gani ya topic na kauli yako kuwa CHADEMA wamezoea kubebwa na kupakatwa? Explain that if you can!
   
Loading...