CHADEMA inaendeshwa "kimagumashi"...

Kuna uhusiano gani ya topic na kauli yako kuwa CHADEMA wamezoea kubebwa na kupakatwa? Explain that if you can!

Mtoboasiri, usitokwe na povu mdomoni. Fuatilia vizuri uone kama kuna mahali nimeandika neno kubebwa au kupakatwa. Haya magumashi mbona mmezoea sana, yaani mpaka hapa unataka kuniingizia maneno mdomoni!!!
 
Mtoboasiri, usitokwe na povu mdomoni. Fuatilia vizuri uone kama kuna mahali nimeandika neno kubebwa au kupakatwa. Haya magumashi mbona mmezoea sana, yaani mpaka hapa unataka kuniingizia maneno mdomoni!!!

Sijawahi kutokwa na povu na sitokwi leo. Tatizo lenu mnaanzisha uzi halafu mnarudi kwa ID nyingine na kuji-support. Matokeo yake ndiyo hayo ya kujikuta ukijibu kwa ID tofauti.

Kama si wewe ulieandika hicho, ilikuwaje ukamjibia alieandika hivyo? Kwa sababu nilichokijibu hapa KIPO!
 
Haya yote ni matatizo ya njaa!! Kama isingekuwa njaa, watu wana kazi, wako busy wala kusingekuwepo na mtiririko wa mada za kipuuzi namna hii!!

Inakuwaje mtu uhoji ufunguzi wa matawi nje lakini HUHOJI kuhusu chama kuwa na katibu mwenezi HASIE NA KADI YA CHAMA!!?
 
​mbowe chadema ataicha akiondoka lakini ccm inaondoka na kikwete
Mkuu, huu ujumbe ungempa Mbowe na vijana wake nadhani ungewafaa sana, maana wao wako mstari wa mbele kuongea makosa ya wenzao. Kumbe wanatakiwa waanze kwanza kujikosoa wenyewe na tabia yao ya kutokuheshimu katiba ya chama chao. Asante sana kwa busara mkuu. Point yako ni babkubwa...
 
mwisho wa siku Rais lzima ATOKE TZ. sotuwaache tuone. kama vipi hta SAU na NRA nitawapigia kura nyie tapeni tu acheni kujenga hoja na sera nzuri za vyama kaeni mkikosoana kila iitwapo leo.

siku hizi wataanznia wameamka sana hawaangalii msemaji wala mkosoaji sana bali nani mwenye sera nzuri na wanaye mtaka. tena kwa hali livyo ccm na cdm mnaweza msirudi wala msishike madaraka ktk nchi hii kwa maneno yenu ya kipuuzi.
 
mwisho wa siku Rais lzima ATOKE TZ. sotuwaache tuone. kama vipi hta SAU na NRA nitawapigia kura nyie tapeni tu acheni kujenga hoja na sera nzuri za vyama kaeni mkikosoana kila iitwapo leo.

siku hizi wataanznia wameamka sana hawaangalii msemaji wala mkosoaji sana bali nani mwenye sera nzuri na wanaye mtaka. tena kwa hali livyo ccm na cdm mnaweza msirudi wala msishike madaraka ktk nchi hii kwa maneno yenu ya kipuuzi.

Asante sana kwa maneno ya busara...
 
mwisho wa siku Rais lzima ATOKE TZ. sotuwaache tuone. kama vipi hta SAU na NRA nitawapigia kura nyie tapeni tu acheni kujenga hoja na sera nzuri za vyama kaeni mkikosoana kila iitwapo leo.

siku hizi wataanznia wameamka sana hawaangalii msemaji wala mkosoaji sana bali nani mwenye sera nzuri na wanaye mtaka. tena kwa hali livyo ccm na cdm mnaweza msirudi wala msishike madaraka ktk nchi hii kwa maneno yenu ya kipuuzi.
Hizo sera Nzuri za CCM zimetufikisha wapi kwa miaka 50 tunataka wachapakazi na waaminifu acha longolongo za kimagamba
 
ZeMarcopolo

kuna mtu alisema, akili za darasani na za maisha ni tofauti........ mkuu huna upeo hata wa basic knowledge!!! huna wisdom wala uwezo wa analysis ya chochote zaidi ya kuhangaika kutafuta kofia ya ccm. vyama vya siasa vya nchi haviwezi kutofautiana mno kwani political system na context ni ileile... labda pia uangalie kinachoendelea kwa both parties aborad, their approach towards establishment/revitalizing their matawis etc.

hebu fuatilia genesis ya chadema ujue michango ya akina balali na wasomi wengine na walianzia wapi

maybe hujui maana ya magumashi.... na labda ungerejea vita ya siasa kwenye vyuo na ujiangalie wewe ungechambuaje

hizi skolashipu za kindugu zinatufanya kuwa kama prostitutes waliopewa vocha za kuingia free kambi za jeshi!!!
 
Last edited by a moderator:
Hizo sera Nzuri za CCM zimetufikisha wapi kwa miaka 50 tunataka wachapakazi na waaminifu acha longolongo za kimagamba

nitake radhi mkuu sjawah kuwa ccm wala cdm na siyo shabiki wa mipasho yenu kama waimba taarabu siku hizi tumeamka kiakili hatuangalii eti chama cha nyerere wala chama cha wasema sana tunataka sera. ndio maana nasema hata SAU na NRA nitawapigia kura. ninyi mmekuwa mnaboa sana kila siku lazima mje na vijembe badala ya kunadi sera na kufanya kwa vitendo yale ambayo tunayataka.

kama siyo mchapa kazi hata iweje hatukupi kura uwe unatoka cdm ama ccm and 2015 you will leave to see manake ni bora hata amgombea binafsi akasimama anaweza kuwa muwajibikajiaa mzuri tofauti na hawa wenye wafuasi.
 
Haya CHADEMA, sasa mmeshajua kosa mlilolifanya. Kaeni chini muifanyie marekebisho katiba ili hayo matawi yatambulike.
Msitetee makosa, haitawasaidia na wananchi watakasirishwa na "magumashi".
Mbowe, baada ya operation sangara ya Morogoro itisha kikao cha dharura cha marekebisho ya katiba ili aibu hii isiendelee kuwepo.
 
tukubali tukatae, hapo kuna hoja ya kujibiwa japokuwa mtoa mada kaja kishabik sana.
 
MPASUKO mkubwa ccm, Juhudi za Kimataifa zinahitajika kukinusuru!

Hali ndani ya ccm imezidi kuwa mbaya na ambayo haijawahi kutokea tangu kuundwa kwa chama hiki tangu mwaka 1977,

Taarifa za ndani na zakuaminika zinasema mpasuko wenye kutishia hata usalama wa nchi yetu,umeanzaa baada ya Lowassa kulazimishwa na wanausalama kuhudhuria UGAWAJI wa ng'ombe pale Monduli ulioratibiwa na kusimamiwa na Rais Jakaya Kikwete!

Kimsingi inasemekana Lowasa alishaapa kutokaa meza moja na JK, hivyo kitendo cha kulazimishwa kuwepo na kuamuliwa kutoa kauli ya kumsifu jk imemkera sana yeye na wanamtandao wake ndani ya ccm na wamepanga kufanya UASI mkubwa ndai ya CHAMA na ikibidi wanasema (nje ya chama)!

Wakati hilo likijiri kambi ya Samweli Sita nayo imechukizwa sana na hatua ya JK kukaribiana na Lowasa kwani wanasema kitendo cha JK kuwa (maadui) kilikuwa kikiwasaidia wao kujijenga kisiasa na kutimiza malengo yao ya Urais 2015

Hawa nao wanatafakari hatua za kuchukua na inatajwa kuna vikao vya siri vimekuwa vikifanyika Tabora na Masaki vikiratibiwa na wanamtandao wa Sitta!

Kundi lingine ni la Waziri Membe,

Kwanza Membe amekasirishwa sana kuona wanaccm wanamchafua huku mwenyekiti jk akiacha tu hizo rafu bila kupuliza kipyenga, amefika mbali na kusema sasa anajibu mapigo,

Wakati kundi la mwishoo ni la vijana, likiongozwa na Januari Makamba, Emanuel Nchimbi, Nape Nauye nk

Hawa wamestushwa sana na mwenyekiti kuwageuka nakuanza kuwa karibu na Lowasa wakati alishawaahidi kuwa sasa ni zamu ya vijana,

Hili nalo linajiapiza kuwa bora chama kife lakini sio kuongozwa na wazee kwakuwa wameongoza kwa miaka 50 lakini nchi inakuwa kwa kurudi nyuma,

Wakati kundi hili likisema kwa manung'uniko, linaonekana kama linasalitiana kwakuwa baadhi yao wameanza kuingana na kudharauliana hawa wakimtuia lawama Januari na Nape kwa wamekuwa wakijipendekeza kwa Mwenyeti badala ya kujenga umoja wao!

Wadadisi wa siasa za ccm wanasema kuwa hali iliyopo haiwezi kutatulika bila juhudi za vyama marafiki vya nje, kama ANC afrika Kusini, PLO cha Palestina, Frerimo cha Msumbiji,nk

Haya ndugu zangu mungu aepushilie mbali Chama hiki kife bila kurusha miguu maana kitatuingiza kwenye matatizo makubwa!​

Haya ni nyeti zaidi kwa CCM kuliko ya CDM kufungua matawi nje ya nchi kikatiba au kwa kutofuata katiba.

Kama ni umagumashi huu ni zaidi.
 
Sssa rafiki yangu cdm hawawezi kufanya mambo kwa kuiga wanayofanya magamba,nikuulize swali je unaweza ukanipa kifungu chochote ndani ya katiba ya nyinyiem kinachosema mtu akituhumiwa kwa ufisadi anavuliwa gamba ndani ya siku 90? Jambo lolote lenye heri na maendeleo kwa chama kama halijawekwa kwenye katiba likifanywa na mwanachama linachukuliwa kama changamoto yenye faida kwa chama.kilichofanywa na zitto na baadae lema ni changamoto chanya kwa chama na sio magumashi unayouyataja hapo.Zaidi wape hai woooooote hapo jengo la rumumba.
 
Ccm wameshawahi kupewa magari ya kuendeshea mikutano kama chadema tumepewa kuwaelimisha watanzanie walitekwa kwa miaka 50 mikononi mwa majambazi M4C inasambaa nchi nzima ccm inakufa vibaya sana !
 
Hivi karibuni umeibuka mtindo wa CHADEMA kufungua matawi nje ya nchi. Tumesikia mgombea Urais mtarajiwa mh. Zitto Kabwe akishirikiana na mbunge wa Tanzania anayeishi Marekani mh. Leticia Nyerere wakifungua tawi Washington DC. Tawi hili la Washington DC baadae tuliona limepewa zawadi ya gari na mwanachama mkereketwa! Leo kumekuwa na taarifa ya aliyevuliwa ubunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuwa Uingereza kwa ajili ya ufunguzi wa matawi saba ya CHADEMA.

Ni dhahiri kuwa CHADEMA wameiga utaratibu huo kutoka CCM. Hata hivyo, tofauti na CCM, katika kufanya hivyo CHADEMA imeanzisha utaratibu huo "kimagumashi".

Kabla CCM haijaanza kufungua matawi nje ya nchi kitu cha kwanza kilikuwa ni kufanya marekebisho ya katiba ili ufunguaji wa matawi hayo ufanyike kwa kufuata katiba ya chama. Ndio maana katika katiba ya CCM sehemu ya tatu, Fungu la kwanza, 22 (1) (i-ii) kuhusu mashina ya chama, inaeleza kuwa kutakuwa na mashina ya ndani ya nchi na nje ya nchi. Katika fungu la pili, 31 (1) (d), imeelezwa kuwa kutakuwa na matawi ya nje ya nchi. Na imeelezwa bayana kuwa matawi hayo yatafunguliwa kwa indhini ya Katibu Mkuu wa chama. Ndani ya katiba ya CCM vikao vyote vya mashina na matawi ya nje ya nchi vimeelezwa kuwa vinafuata utaratubu upi wa uongozi.

Kwa upande wa CHADEMA, Katiba ya chama sura ya saba 7.2.1 inasema tawi litaundwa katika kila eneo la kijiji, mtaa au Shehiya ya kiutawala katika mamlaka za serikali za mitaa. Hata hivyo kinyume na katiba hii, katika mazingira ya "kimagumashi", viongozi wa CHADEMA wameanza kufungua matawi nje ya nchi! Haieleweki nani anatoa idhini ya matawi hayo kufunguliwa! Haieleweki matawi hayo yanamlolongo gani wa kiuongozi (wanareport kwa nani). Haieleweki nafasi ya viongozi wa matawi hayo katika uongozi wa chama! Kila anayeamua ananyanyuka na kwenda kufungua tawi nchi anayotaka, kwenye marafiki zake, kwa sababu zake!

Hata hivyo kwa vile mashabiki wa CHADEMA hawajajenga utaratibu wa kuhoji pale viongozi wao wanapoonekana kufanya "magumashi", mashabiki hao wamekuwa wakifurahia tu ufunguzi huu wa matawi.

Kuna taarifa kwamba kitendo cha Lema kwenda kufungua matawi Uingereza ni kwa ajili ya kumuwahi Zitto asiende pia kuweka kambi yake huko kama alivyofanya Marekani, lakini swali ni je, Zitto na Lema katika huku kuwahiana kwao wanafuata utaratibu upi kikatiba? Haya "magumashi" yao yanakipeleka wapi chama?

Mimi bado najiuliza, hawa watu wako serious na uongozi wa nchi yetu? Mbona maneno yao na matendo yao havifanani hata kidogo?


Kwani CCM haina Uwalakini? Too Much expectations and criticizer at the same time of CHADEMA...

Waacheni Wana Mipango yao na Wamehakikisha kuwa WIZI kama wa CCM wa MCHANA ndio MWISHO...

Kwanini Unahangaika na Matatizo ya CHADEMA; wakati ya CCM ni Makubwa? Mfano Mdogo ni Sophia Simba na

Mama Kilango... Huo ni Mdogo tu... Wewe sijui source zako ni zipi kuhusu LEMA na ZITTO...

Haukumbuki...:sleepy: Tawi la CCM DC Kikwete alipokwenda walipachikana tu... Mh. Balozi aliyajua hayo... Wanachama

Hawakujua chochote... Angalia CHAMA CHAKO KWANZA kina RUTBA NYINGI TU....
 
a spin doctor at work! keep twisting the truth." If fools went not to market , bad wares would not be sold"
 
wakati tunaenda mwishoni mwa chaguzi za msingi,ghafla tunapata taarifa kwamba chaguzi hizo zimesitishwa na sasa zitafanyika tu chaguzi za matawi ambazo zitasimamiwa na makao makuu kinyume na katiba ya chama.

Inavyoonekana chama kinashindwa kuwaamini watu wa mikoa,wilaya na majimbo na kutaka wao kama viongozi wa makao makuu wafanye wenyewe kila kitu hata ktk ngazi za chini kabisa, kwa hali hii program nyingine za chama kitaifa zinaweza kukwama kutokana na makao makuu kuwa waroho wa kukumbatia majukumu ambayo hata ktk katiba yamegawanywa.

Wakati huo huo wamesimamisha ruzuku kwa muda wa miezi sita,hii ina maana shughuli za uenezi wa chama nchi nzima zitafanywa na makao makuu pekee,kwa hali hii tuna dhamira ya kweli kuchukua nchi au tunapanga programu ili viongozi wa kitaifa wanufaike na ruzuku? Wanajifanya ma star wa kihindi kila kitu wanajua wao.

Naomba doctor slaa aje atolee maelezo swala hili kama ana dhamira safi na chama.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom