CHADEMA inaendeshwa "kimagumashi"...

mm huwa nashiriki ktk kuandaa katiba za vyama na makampuni, ninajua huwa inawekwa open handed clause ili kujumuisha masuala ambayo hayakutajwa moja kwa moja ktk Katiba. kipengele hicho huwezesha kampuni/chama kufanya jambo lolote hata kama halijatajwa katika katiba ilimradi tu jambo hilo lina lengo la kuleta faida kwa chama/kampuni husika. Hivyo ninachosema nina uhakika nacho ndio maana nimeomba u-attach katiba ya sasa ya cdm ili tuipitie tuone endapo haina vipengele/kipengele cha jinsi hiyo. mm ninayekuleza ni mtaalamu katika masuala haya ndiyo maana nimeomba nakala ya katiba nikijua nikiiipata nitafungua eneo gani ambalo huwa tunaweka katika uandishi wa katiba.

natumai nimeeleweka vizuri

Kabla hujabisha unatakiwa kwanza uitafute katika inayojadiliwa uisome, halafu uje na hiyo clause inayoruhusu. Ukitumia nadharia kuna siku utafungwa kwa kosa lisilokuhusu, kwa kutetea mambo usiyojua undani wake.
 
Kama matawi ya Chadema nje ya Tanzania, hayatambuliki kwenye katiba ya chama kuna hoja kubwa ya kujadili. Chama kikianza puuzo kwa katiba iliyojiwekea yenyewe, kinatupa masuali iwapo kitaheshimu katiba ya nchi.

Ni propaganda tu ndugu yangu. sidhani kama ni issue kihivyo. kuna chama fulani hicho kinachotajwa kuigwa strategy yake kimeona pamoja na kufanya hivyo mwitikio wa watu kule nje ni mdogo sana ( huwa tunaona picha). sasa nadhani baada ya kuona hicho kinachotajwa kuiga kinapata mwitikio mkubwa, ndipo maneno yanaanza. Kuna timu moja ilifungwa kombe la Kagame hivi karibuni, kocha alipoulizwa sababu ya msingi ya kufungwa kule akasema eti " Oh, unajua, sisi tulikuwa tunacheza mipira ya chini sasa wao (wapinzani) wakaiga mpira wetu, so wakatufunga...). Mh, sasa kama hiyo ni strategy yenu, iwaje mpate mashaka kuona wapinzani wenu wameiga, SI ITAKUWA MUDA MZURI KUWAFUNGA MAGOLI MENGI CAUSE WANAIGA STRATEGY AMBAYO NYIE MNAIJUA NA KUIMUDU VIZURI ZAIDI ? Najaribu kuliona kwa mtazamo mwingine, hasa nikiamini kuwa mtoa mada, LABDA linamsumbua hilo la hicho chama kingine kufungua matawi nje.
 
Una kipengele unachojua kimeruhusu au unatumia nadharia tu? Ongea kwa evidence...

mm huwa nashiriki ktk kuandaa katiba za vyama na makampuni, ninajua huwa inawekwa open handed clause ili kujumuisha masuala ambayo hayakutajwa moja kwa moja ktk Katiba. kipengele hicho huwezesha kampuni/chama kufanya jambo lolote hata kama halijatajwa katika katiba ilimradi tu jambo hilo lina lengo la kuleta faida kwa chama/kampuni husika. Hivyo ninachosema nina uhakika nacho ndio maana nimeomba u-attach katiba ya sasa ya cdm ili tuipitie tuone endapo haina vipengele/kipengele cha jinsi hiyo. mm ninayekuleza ni mtaalamu katika masuala haya ndiyo maana nimeomba nakala ya katiba nikijua nikiiipata nitafungua eneo gani ambalo huwa tunaweka katika uandishi wa katiba. Ukiona tunaomba document lengo lake ni kujengana na sio kushabikia au kumuonea mtu '// let justice be done even if heaven falls//

natumai nimeeleweka vizuri
 
Hivi karibuni umeibuka mtindo wa CHADEMA kufungua matawi nje ya nchi. Tumesikia mgombea Urais mtarajiwa mh. Zitto Kabwe akishirikiana na mbunge wa Tanzania anayeishi Marekani mh. Leticia Nyerere wakifungua tawi Washington DC. Tawi hili la Washington DC baadae tuliona limepewa zawadi ya gari na mwanachama mkereketwa! Leo kumekuwa na taarifa ya aliyevuliwa ubunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuwa Uingereza kwa ajili ya ufunguzi wa matawi saba ya CHADEMA.

Ni dhahiri kuwa CHADEMA wameiga utaratibu huo kutoka CCM. Hata hivyo, tofauti na CCM, katika kufanya hivyo CHADEMA imeanzisha utaratibu huo "kimagumashi".

Kabla CCM haijaanza kufungua matawi nje ya nchi kitu cha kwanza kilikuwa ni kufanya marekebisho ya katiba ili ufunguaji wa matawi hayo ufanyike kwa kufuata katiba ya chama. Ndio maana katika katiba ya CCM sehemu ya tatu, Fungu la kwanza, 22 (1) (i-ii) kuhusu mashina ya chama, inaeleza kuwa kutakuwa na mashina ya ndani ya nchi na nje ya nchi. Katika fungu la pili, 31 (1) (d), imeelezwa kuwa kutakuwa na matawi ya nje ya nchi. Na imeelezwa bayana kuwa matawi hayo yatafunguliwa kwa indhini ya Katibu Mkuu wa chama. Ndani ya katiba ya CCM vikao vyote vya mashina na matawi ya nje ya nchi vimeelezwa kuwa vinafuata utaratubu upi wa uongozi.

Kwa upande wa CHADEMA, Katiba ya chama sura ya saba 7.2.1 inasema tawi litaundwa katika kila eneo la kijiji, mtaa au Shehiya ya kiutawala katika mamlaka za serikali za mitaa. Hata hivyo kinyume na katiba hii, katika mazingira ya "kimagumashi", viongozi wa CHADEMA wameanza kufungua matawi nje ya nchi! Haieleweki nani anatoa idhini ya matawi hayo kufunguliwa! Haieleweki matawi hayo yanamlolongo gani wa kiuongozi (wanareport kwa nani). Haieleweki nafasi ya viongozi wa matawi hayo katika uongozi wa chama! Kila anayeamua ananyanyuka na kwenda kufungua tawi nchi anayotaka, kwenye marafiki zake, kwa sababu zake!

Hata hivyo kwa vile mashabiki wa CHADEMA hawajajenga utaratibu wa kuhoji pale viongozi wao wanapoonekana kufanya "magumashi", mashabiki hao wamekuwa wakifurahia tu ufunguzi huu wa matawi.

Kuna taarifa kwamba kitendo cha Lema kwenda kufungua matawi Uingereza ni kwa ajili ya kumuwahi Zitto asiende pia kuweka kambi yake huko kama alivyofanya Marekani, lakini swali ni je, Zitto na Lema katika huku kuwahiana kwao wanafuata utaratibu upi kikatiba? Haya "magumashi" yao yanakipeleka wapi chama?

Mimi bado najiuliza, hawa watu wako serious na uongozi wa nchi yetu? Mbona maneno yao na matendo yao havifanani hata kidogo?
arifu aiseee.....umeanza ku develop makambasios zemacophyta mazee.....nimeamini ukiingia gambani mnajivika upuyuyu aiseee.....
 
Hebu funguka vizuri mkuu, maana unajicontradict so tatizo ni ufunguzi wa matawi, au Lema kumuwahi Zitto?
 
Swali ni je, kwanini ufunguzi wa matawi ya CHADEMA nje ya nchi hauheshimu katiba ya chama?
Mpaka sasa hakuna aliyetoa jibu!
"Katiba ya chama sura ya saba 7.2.1 inasema tawi litaundwa katika kila eneo la kijiji, mtaa au Shehiya ya kiutawala katika mamlaka za serikali za mitaa". Sasa wewe gari aina ya ZeMarcopolo, hivi unadhani Uingereza au USA hakuna mtaa au mamlaka za serikali za mitaa? Au mpaka iandikwe "ndani ya nchi" ndio uelewe?! Umekariri eehhhh??????????? Hoja DHAIFU kama alivyo M/Kiti wa Mabwepande!!!!!
 
Swali gumu THANA HILI
Katiba ya chama sura ya saba 7.2.1 inasema tawi litaundwa katika kila eneo la kijiji, mtaa au Shehiya ya kiutawala katika mamlaka za serikali za mitaa. Hivi nyie Magamba, mmekariri eeeeehhh? Au mpaka iandikwe "nje ya nchi" ndio muelewe? Kwani USA, Uingereza, n.k. hakuna mitaa/serikali za mitaa? Mbona Katiba iko wazi? Yaani mna Magamba hadi kwenye akili zenu? Duh!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom