MoureenAbel
Member
- Sep 24, 2021
- 29
- 43
Ili kuweza kukitoa chama tawala madarakani, ni wazi kuwa panahitaji chama ambacho kitakuwa mbadala wake, chenye nguvu kama au walau kukaribia nguvu chama tawala. Hali inapokuwa kinyume na hapo, ni wazi kwamba itakuwa vigumu sana kukitoa chama tawala madarakani kwa sababu hilo linawakatisha wananchi tamaa.
Hii ndio hali iliyopo Tanzania kwa sasa. CHADEMA inatamani sana kuiondoa CCM madarakani, lakini ni wazi kwa uwezo wa CHADEMA ulivyo mdogo, tamanio hili litendelea kuwa ndoto hadi pale watakapoamua kubadilika.
CHADEMA imekuwa ikiruka na kila mjadala unaokuja mitandaoni, viongozi wake wamekuwa ni watu wa kushikilia kila kibaya kinachoichafua serikali, badala ya kutumia nguvu na uwezo wao kujenga chama kiwafikie wananchi zaidi, kitoe sera mbadala ili wananchi wakifahamu na wajue kwamba wana mbadala.
Leo CHADEMA inamkumbatia Polepole na kumuona kama shujaa, wakati miezi kadhaa nyuma walikuwa wanamuona kama sehemu ya watesi, likiji la Tanzania kunyimwa mikopo wanaruka nalo, la katiba mpya wanalo, tozo wanalo, umeme wanalo, EWURA wanalo. Yani hata wananchi wanashindwa kuelewa hawa watu wana sera gani.
Suala sio kuruka na kila hoja au mjadala,andaeni sera itakayoonekana kuwa ni mbadala wa kinachopelelea haya yote kutokea.