SI KWELI PreGE2025 CHADEMA imetuma maombi kushiriki uchaguzi

SI KWELI PreGE2025 CHADEMA imetuma maombi kushiriki uchaguzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Heche kweli kichekesho! Kila siku makelele kama generator ya kijijini, kumbe walikuwa wanapiga porojo tu! Walisema hawashiriki uchaguzi, leo wanatuma maombi kwa mbwembwe. Wanafiki wakuu, walitaka huruma kumbe walikuwa wanatafuta nafasi! Acheni maigizo, wananchi si wajinga.

Heche Kushiriki uchaguzi july 02, 2025.jpg
 
Tunachokijua
John Heche makamu mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) alizungumza na wananchi Juni 30, 2025. Katika mkutano huo Heche alizungumzia masuala tofauti ikiwemo suala la kuhitaji mabadiliko ya uchaguzi.

Madai

Juni 30, 2025 kumekuwa na grafiki inayosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikiwemo X huku ikiwa na utambulisho wa chombo cha habari cha Jambo TV. Grafiki hiyo imeambatana na picha ya John Heche na ujumbe unaosomeka “HECHE: CHADEMA TUMESHATUMA MAOMBI YA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA MSAJILI”

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli. Katika hotuba aliyoitoa John Heche Juni 30, 2025, Makamu huyo alizungumza mambo mbalimbali yanayoeneldela nchini ikiwemo kupotea kwa watu, kutekwa na mwenenndo wa hali ya uchumi.

Ufuatiliaji wa kina uliofanywa na JamiiCheck kwa kufuatilia hotuba hiyo imebaini kuwa maneno hayo ya kuwa CHADEMA wameshatuma maombi ya kushiriki uchaguzi mkuu wa kwa msajili wa vyama.

Mbali na mambo mengine Heche alibainisha kuwa serikali inatamani viongozi wa chama hicho waende kusujudu kwao lakini wao wamekataa. Pia amesisitiza kuwa wamekataa kushiriki katika uchaguzi usio sawa na wa haki

“Tumekataa kuwa sehemu ya uchaguzi wenye unajisi. Tunaisihi serikali na tunaendelea kuisihi serikali ifanye mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi” - John Heche

April 12 Kaimu Katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika kupitia ukurasa wake wa X alisema kuwa hatoenda kusaini fomu za maadili ya uchaguzi wakihimiza mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi, jambo ambalo liliwanyima wao sifa za kushiriki uchaguzi mkuu 2025.

JamiiCheck imefuatilia pia na kubaini kuwa grafiki zinazotumika kusambaza taarifa hizo hazijatolewa wala kuchapishwa na Jambo TV katika kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii hivyo ni za kughushi.
Kichekesho ni wewe ambaye huna uhakika halafu unaleta hapa!!!
View attachment 3390334
Heche kweli kichekesho! Kila siku makelele kama generator ya kijijini, kumbe walikuwa wanapiga porojo tu! Walisema hawashiriki uchaguzi, leo wanatuma maombi kwa mbwembwe. Wanafiki wakuu, walitaka huruma kumbe walikuwa wanatafuta nafasi! Acheni maigizo, wananchi si wajinga.
 
View attachment 3390334
Heche kweli kichekesho! Kila siku makelele kama generator ya kijijini, kumbe walikuwa wanapiga porojo tu! Walisema hawashiriki uchaguzi, leo wanatuma maombi kwa mbwembwe. Wanafiki wakuu, walitaka huruma kumbe walikuwa wanatafuta nafasi! Acheni maigizo, wananchi si wajinga.
No refoms no election haimanishi hatutashiriki uchaguzi mkuu. Elewa vitu kabla ya kukurupuka.
 
View attachment 3390334
Heche kweli kichekesho! Kila siku makelele kama generator ya kijijini, kumbe walikuwa wanapiga porojo tu! Walisema hawashiriki uchaguzi, leo wanatuma maombi kwa mbwembwe. Wanafiki wakuu, walitaka huruma kumbe walikuwa wanatafuta nafasi! Acheni maigizo, wananchi si wajinga.
View attachment 3390334
Heche kweli kichekesho! Kila siku makelele kama generator ya kijijini, kumbe walikuwa wanapiga porojo tu! Walisema hawashiriki uchaguzi, leo wanatuma maombi kwa mbwembwe. Wanafiki wakuu, walitaka huruma kumbe walikuwa wanatafuta nafasi! Acheni maigizo, wananchi si wajinga.

Hiyo habari umeitengeneza mwenyewe au kuna mwendawazimu mwenzako amekutengenezea?

Mods, tafadhali ondeeni hii takataka. Na mleta mada hii ya uwongo awajibishwe. Hii mleta mada ameitengeneza ili kuharibu heshima ya JF.

Hiyo habari haipo Jambo TV.
 
Inawezekana ni kutokana na shinikizo, CCM kuwaambia ili tusionekane tumeamriwa kuwashirikisha uchaguzi, basi ombeni kushiriki. Hizi zinaweza kuwa negotitions zinazoendelea nyuma ya pazia kutokana na shinikozo la EU na USA.
 
Hiyo habari umeitengeneza mwenyewe au kuna mwendawazimu mwenzako amekutengenezea?

Mods, tafadhali ondeeni hii takataka. Na mleta mada hii ya uwongo awajibishwe. Hii mleta mada ameitengeneza ili kuharibu heshima ya JF.

Hiyo habari haipo Jambo TV.
Sijatengeneza, nimeikuta Twitter, na ndiyo maana nimeweka kiulizo (?) kwenye post yangu
 
Ndiyo maana kichwa cha habari kina question mark (?). Maana nimeikuta Twitter
Kumbe huna uhakila lakini umeanza kwa kumuona Heche ni kichekesho!!?
Ulienda shule kusomea ujinga!!??
Ukilaza ni janga.
 
Baada tu ya bunge kuvunjwa NO REFORM NO ELECTION kuna namna inakosa nguvu sitashangaa kuona CHADEMA wakishiriki uchaguzi japo sina uhakika na chanzo cha habari
 
Back
Top Bottom