Ungejaribu kusoma vizuri mada yangu na kuielewa, inaelekea bado hujaielewa vinginevyo usingeniweka moja kwa moja upande wa hasi badala ya upande wa chanya.
Asante kwa mtazamo wako, lakini ungetambua kwanza kwamba mada hii inavyoendana na kichwa cha habari haihusiani na mfafanikio ya Chadema bali udhaifu kutokana ya ahadi yao ya kufanya jiji la Mwanza kuwa kielelezo cha uongozi bora unaotakiwa nchini.
Asante kwa mwono wako, ila kwa sasa hatuna muda wa kuendelea kujadili madhaifu ya CCM kwa sababu kila kukicha tunayaona na kuyajadili na katu hawabadiliki na ndiyo hali inazidi kuwa mbaya zaidi.
Chadema kwa vile wanaonekana kuwa ndio tegemeo la wengi kuokoa jahazi lisizame ndio maana tuko makini kuangalia mwenendo wao pale wanapoonekana kuteleza warudi kwenye mstari. Yaliyotokea Mwanza si jambo la kunyamazia, ni kosa la kiufundi na kisayansi katika mwenendo wa kujijenga kisiasa.
Ukweli huuma, hakuna sababu ya kufunikafunika ukweli kwani mficha ukweli huumbuka hadharani. Wenye moyo wa uzalendo wa kweli kwa nchi yetu tutaungana kuijenga Chadema kwa kusifia wanapofanikiwa na kuwashutumu wanapoleteza. Huku ndiko kujengana badala ya kuendeleza mambo ya kulindana kama wafanyavyo wale wa magambani.
Chadema haiwezi kuongoza nchi hii maana majimbo yao yoote yako hoi. Arusha ndo pyuuuuuuuu. Ubungo yalaaaaaa kawe ndo kasweeeeeeeee. Yaani shida tupu ngoja 2015 washikishwe adabu na wapiga kura sijui watawaambia nini conservative union
Huu muda uliopoteza hapa nafuu ungechukua jembe ukalime!!Ungejaribu kusoma vizuri mada yangu na kuielewa, inaelekea bado hujaielewa vinginevyo usingeniweka moja kwa moja upande wa hasi badala ya upande wa chanya.
Mkuu hakuna mafanikio bila matatizo especially kama anaehusika ni binadamu. Siipendi ccm na mfumo wake na jinsi ambavyo imeshindwa kusimamia raslimali za taifa na kuacha rushwa kutamalaki,lakini sibezi mafanikio na maendeleo yaliyoletwa na ccm kwa kipindi chote kilichokuwepo madarakani, as a thinker huwezi ukaongelea madhaifu tu pasipo kuhusisha mafanikio. Ni kutokana na kipimo cha ufaulu ndo tunatambua kufeli, huwezi ukaangalia mafanikio exclusively bila kuhusisha matatizo unless you are biased, come again mkuu.
Mimi nitaelewa ukiniambia kuwa CDM wamekosa umeya Mwanza wakiwa na madiwani wote kuficha ukweli wa kuligawa jiji la mwanza ili wapite kwa madiwani wao ni udhaifu wa kwa mtoa hoja nilidhani ungefanya hesabu kuwa idadi ya madiwani wote wa jiji hilo kabla ya kugawanywa ilemela na nyamagana wamefanya uchaguzi wa meya jiji la mwanza na CCM wameshindwa otherwise hujanishawishi hapa.
Pili, Nadhani CDM ndo chama kinachoweza kuiongoza hii nchi, Diwani asipofuata katiba yao hawawezi kumuuacha eti kwa sababu akifukuzwa wataukosa umeya mambo kama haya ndo yamefikisha nchi hapa tulipo, CDM wako tayali kupoteza watu wote kama hawawezi kufuata misingi na katika yao, kule A.town tuliona , mwanza pia kama kuna mtu anataka kufanya hayo mambo kuna usemi wa kwamba utawafukuza wangapi uko CCM tu, huku CDM hakuna kitu kama hicho.
MWISHO CCM WAMESHINDA UMEYA KWA SABABU WALILIGAWA JIJI LA MWANZA NA SIYO KINGINE TUWEWAKWELI KATIKA HILI.
Huu muda uliopoteza hapa nafuu ungechukua jembe ukalime!!
Nakubaliana na mleta mada kwa asilimia kubwa sana, huu ndo ukomavu. Nakubali kabisa kwamba uongozi wa juu ulipaswa kuwa karibu na meya na madiwani wa mwanza kwa sababu ndiko walikosema wanataka kuweka mfano, naamini mtu muhimu zaidi kwenye hili alipaswa kuwa slaa mwenyewe kwa sababu akina mbowe wapo bungeni muda mwingi.
kama viongozi wangekuwa karibu na madiwani naamini wasingefikia mahali pa kumtosa meya wao wenyewe maana wangeweza kurekebishana kabla ya kufika huko kwenye kuaibishana. Kuna miaka miwili mbele kabla ya uchaguzi mkuu, kama hakutakuwa na kukosoana maana yake chama hakitkuwa na wakati wa kujirekebisha, hili litakuwa kosa kubwa sana kwa sababu wakati washabiki wataangalia chama kuna watu wasio na vyama wataangalia uhalisia wa mambo. Na endapo tulikosea na hatukujirekebisha tutarudi kwenye yaleyale ya kuibiwa kura nk.
Ukweli utatuweka huru ndugu zangu
Chadema haiwezi kuongoza nchi hii maana majimbo yao yoote yako hoi. Arusha ndo pyuuuuuuuu. Ubungo yalaaaaaa kawe ndo kasweeeeeeeee. Yaani shida tupu ngoja 2015 washikishwe adabu na wapiga kura sijui watawaambia nini conservative union