CHADEMA imeonyesha udhaifu kuongoza nchi, ijipange upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA imeonyesha udhaifu kuongoza nchi, ijipange upya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Oct 7, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Chadema ilifanikiwa kushika usukani wa kuliongoza jiji la Mwanza, Meya wa jiji akiwa ni wa Chadema. Mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita, Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbroad Slaa alitamka hadharani kwenye vyombo vya habari kwamba wanakusudia Jiji la Mwanza linaloongozwa na Chadema kuwa ndio dira ya mfano wa uongozi uliotukuka ambao wakishika nchi watafanya kweli. Wengi tuliamini na kuwa na matumaini hayo tukifikiria Jiji la Mwanza kuwa dira ya mafanikio Chadema katika kuongoza nchi.

  Je, matumaini hayo yamefifia? Hapana, nadhani wana nafasi ya kujipanga upya, wameteleza kidogo.

  Kosa ambalo viongozi wa juu Chadema wamelifanya ni kutokuwa karibu na uongozi wa halmashari ya jiji la Mwanza ambalo walikalia kiti cha Umeya. Walitakiwa kuwa karibu na kujitahidi kuwapa mbinu na kusaidia kutatua matatizo yaliyokuwa yakijitokeza ili kuleta picha kwa wapiga kura kwamba viongozi wa juu ni wafuatiliaji katika utendaji wa watumishi wa umma.

  Matokeo yamekuwa kinyume cha hayo kwani imefikia Madiwani wa Chadema ndio walifanikisha azima ya kumtosa nje ya kiti cha umeya meya wao. Uongozi wa Juu Chadema ukakurupuka kuwafukuza madiwani wake ambao walitumia haki zao kikatiba bila woga wa sera ya uwajibikaji wa pamoja kichama.

  Jambo la kujiuliza, uongozi wa Chadema kitaifa walikuwa wapi siku zote hadi waje dakika za majeruhi kufukuza madiwani wake? Kama uongozi wa juu Chadema wangekuwa karibu na wadiwani wake matatizo yaliyojitokeza yangetatuliwa mapema na kusingetokea haya ya kufukuzana na kuachia ngazi jiji la Mwanza kurudi mikononi mwa wahasimu wao CCM.

  Makosa yaliyojitokeza Chadema Mwanza:


  • Chadema Taifa kutokuwa karibu kufuatilia maendeleo ya uongozi wao jiji la Mwanza.

  • Chadema kuelekeza nguvu zote kukijenga chama (M4C) na kusahau kulinda ardhi iliyokumbolewa na hivyo adui kuirudisha kwenye himaya yake.
  • Madiwani kukosa uzalendo wa uwajibikaji wa pamoja kwani walikuwa na nafasi ya kumshauri meya wao, kama ilishindikana basi wangeomba uongozi wa juu kuokoa jahazi lisizame.
  • Madiwani wa Chadema walisaliti kuungana na CCM badala ya kuomba Chadama taifa wasaidie kuziba nyufa zilizojitokeza.
  • Kosa la kushindwa kutamalaki jiji la Mwanza ni hoja ya CCM kuonyesha uchaguzi ujao udhaifu wa Chadema kushika dola.

  Binafsi ningependa kuelekeza kosa kwa viongozi wa Chadema taifa badala ya kuwalaumu madiwani wa Mwanza pekee, na pengine uongozi wa CCM mkoa Mwanza unahaki ya kubebeshwa gunia hili la misumari. Mwanza kuna wabunge kadhaa ambao kwa uzoefu wao wa kuwa bungeni wangeweza kuona tatizo hilo mapema na kutafuta njia mwafaka wa kulitatua kuliko kuacha ufa uzidi kupanuka na kufikisha hatua ya sasa.

  Chadema wanatakiwa kuangalia kasoro hii na kuanza kujipanga upya, maana kosa ni kosa, na kurudia kosa ni ni mwanguko. Hata hivyo picha isiyo ya kawaida imetokea kutokana na kauli Dr. Slaa kuwa jiji la Mwanza kuwa kielelezo cha mfano wa mafanikio ya Chadema na sasa kugeuka kuwa kitendawili.
   
 2. N

  Njele JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Una maana hawawezi kuongoza nchi ukilinganisha na wozo wa magamba? Kama siku umeweka mada dhaifu ndio leo, sikutegemea. Ya mwanza ni mbinu za CCM kuiharibia Chadema.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ungejaribu kusoma vizuri mada yangu na kuielewa, inaelekea bado hujaielewa vinginevyo usingeniweka moja kwa moja upande wa hasi badala ya upande wa chanya.
   
 4. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Nimesoma kwa makini but nakuonea huruma kwani umepoteza muda kuandika post ambayo haina point,
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni mategemeo yangu kupata jibu kama hilo, lakini ukweli hautaondoka kwa kutetea udhaifu uliojitokeza.
   
 6. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Usikia moto wa chadema kaa mbali M4C inakwenda kuwafukia hawa wahuni ccm chini..100% tumeshashinda tunasubiri muda ufike kama umetumwa umepotea njia ndugu yangu karibu CDM .
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Jamani tuwe wawazi, Chadema imeteleza, imekosa umakini katika kuhakikisha jiji la Mwanza lililokomboliewa linarudi mikononi mwa CCM chini ya miaka miwili. Walao ingefikisha nusu ya muhula imeshindikana. Nani wa kulaumiwa?
   
 8. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kaandika mambo ambayo yana point ajibiwe tu kwa point hata kama kaandika upumbavu, busara inanituma kuamini kuwa hakuna upumbavu mtupu usio kuwa na chembe kidogo ya kiwango cha hekima ndani yake.

  Cha msingi mleta mada tumuombe aweke na madhaifu ya serikali ya ccm halafu tuweke kwenye mzani. Tena hapa aweke kwenye mzani halmashauri ya wilaya ya Kishapu na ya jiji la Mwanza kwa kuangazia ubadhiru ulio kwisha kutokea! Tusijadili ya kutuumiza vichwa kwenye mawizara na vitalu vya uwindaji.
   
 9. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  nimesoma vizuri na kukuelewa vema,ushauri wako na maoni yako ni ya msingi kwa mstakbali wa ujenzi wa chama na nchi,napenda kukukumbusha kuwa hakuna mafanikio yanayopatikana pasi na kukosea,uzuri tumekuwa na watu mhm kama wewe wenye karama za kuona na kupaza sauti,binafsi nakupongeza kwa ushauri mzuri na wa kujenga,ukweli ni kwamba mtu asiependa kukosolewa anakosa haiba na utashi wa kupewa madaraka na mamlaka ya kuongoza.safi sana candid scope i like you guy!
   
 10. a

  anonyme Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mfumo wa nchi hauruhusu vyama ku thrive hilo ni wazi. Ili tuwe na demokrasia ya kweli tuwe wavumilivu
   
 11. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Wale madiwani waliofukuzwa ndo wa kulaumiwa ndo chadema tumewavua uanachama kwani tulijua walichokuwa wanakifanya but Umeya tumeshapoteza tunatakiwa kusonga mbele syo muda wa kumtafuta mchawi harakati mwanzo mwisho mpaka kieleke M4C..BOABOA MAFISADI WOTE HADI TUNAHAKIKISHA TUNAONGOZA HII NCHI NA NIA ZIMESHAANZA KUONEKANA KUPITIA M4C KUNA HAO WAHUNI WANATUMIA NA CCM ..V4C CUF WANAPOTEZA MUDA WAO KWANI WAMESHACHELEWA M4C IMESHAPITA.
   
 12. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hoja yako ina mashiko, japo mi naona sababu kubwa ya anguko ni zile zababu zako mbili za mwanzo. Na katika hili nadhani Makao Makuu watafakari uwezekano wa kuanzisha idara ya tawala za mikoa (au tuseme majimbo) kichama na iwe bize kisawasawa "kulinda maeneo yaliyotekwa."   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu hoja yako nzito sana ni ya ujenzi wa taifa letu katika mustakabali wetu.
   
 14. N

  NO EXCUSE JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 406
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Umetoa ushauri nzuri ni inabidi ufanyiwe kazi. Chama cha siasa kinaundwa na kuongozwa na watu. Na watu hao huwa na mitizamo na malengo tofauti wanapotaka kuchaguliwa. Kupoteza meya na kisha kufukuza madiwani kuliko sababisha kushindwa uchaguzi wa meya ni sucrifice kubwa sana. Ingekuwa si kwa nia isiyo na shaka ya kuwajibishana bila kujali watapoteza nini. Laiti nchi hii tungaluwa na mfumo wa kuwajibishana tungaluwa kama China, Singapore nk
   
 15. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  So akilini mwenu ni kushinda tu!!! Tanzania bado... i think we do not know what we need.
   
 16. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kuna baadhi ya hoja za msingi katika bandiko lako lakini hitimisho lako umelijenga katika misingi dhaifu mno. Siamini kwamba makosa waliofanya CHADEMA Mwanza ni kigezo sahihi cha kuihukumu Chadema kwa ujumla wake kitaifa,katika andiko lako umeegemea zaidi katika kueleza madhaifu tu yaliyojitokeza na ukaishia kuweka muhuri wa CHADEMA kupoteza dira kitaifa.jaribu kuondoa ukungu wa biasness katika mtazamo wako mkuu, angalia kazi za CHADEMA kwa nafasi zao kisiasa na kama chama cha upinzani ambacho ni dhahiri kinakumbana na fitna nyingi kutoka kwa chama tawala ambacho WATENDAJI wengi wa halmashauri ni watiifu kwake. Pia tazama na time factor. Tuendelee
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kinga ni bora kuliko kuponya, kama tahadhari ingefanyika mapema sitegemei kama hatua ya kufukuza madiwani ingetokea. Huenda madiwani wale walikata tamaa baada ya kuona uvumilivu umeshindikana.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Asante kwa mtazamo wako, lakini ungetambua kwanza kwamba mada hii inavyoendana na kichwa cha habari haihusiani na mfafanikio ya Chadema bali udhaifu kutokana ya ahadi yao ya kufanya jiji la Mwanza kuwa kielelezo cha uongozi bora unaotakiwa nchini.
   
 19. b

  blueray JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mleta mada anajaribu kujenga hoja kwamba mwanza ilitakiwa ipate Maendeleo makubwa kwa sababu imekuwa ikiongozwa Na Chadema lakini imeshindwa: Na hivyo ndivyo itakavyokuwa Chadema ikishika dola!

  kwanza hoja yako umeijenga kwa misingi dhaifu.

  pili, umeshindwa kuzingatia kwamba Chadema sasa hivi haina dola, haina uwezo Wa kukasimu, na hata budget ikishapitishwa Chadema haina uwezo wa kupeleka Pesa kwenye manispaa zikatumike. Pesa wanazopata manispaa zinatoka serikali kuu inayoongozwa Na CCM, wakiamua kuwakwamisha wanawakwamisha.

  Pia ni vizuri ukaelewa hizi Pesa za matumizi kwenye wilaya zinasimamiwa Na wakurugezi ambao ni waajiriwa Wa serikali. hivyo mkurugenzi anaweza kuamua kukwamisha Maendeleo ya mji kwa manufaa ya bosi wake

  katika mazingira haya, Mchango mkubwa wa Meya na Madiwani ni kuhakikisha Pesa iliyopatikana haitumiki vibaya. Ingawa kuna pesa inayopatikana kwa kodi za manispaa Pesa hii ni kidogo
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Asante kwa mwono wako, ila kwa sasa hatuna muda wa kuendelea kujadili madhaifu ya CCM kwa sababu kila kukicha tunayaona na kuyajadili na katu hawabadiliki na ndiyo hali inazidi kuwa mbaya zaidi.

  Chadema kwa vile wanaonekana kuwa ndio tegemeo la wengi kuokoa jahazi lisizame ndio maana tuko makini kuangalia mwenendo wao pale wanapoonekana kuteleza warudi kwenye mstari. Yaliyotokea Mwanza si jambo la kunyamazia, ni kosa la kiufundi na kisayansi katika mwenendo wa kujijenga kisiasa.

  Ukweli huuma, hakuna sababu ya kufunikafunika ukweli kwani mficha ukweli huumbuka hadharani. Wenye moyo wa uzalendo wa kweli kwa nchi yetu tutaungana kuijenga Chadema kwa kusifia wanapofanikiwa na kuwashutumu wanapoleteza. Huku ndiko kujengana badala ya kuendeleza mambo ya kulindana kama wafanyavyo wale wa magambani.
   
Loading...