Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,884
- 6,885
- Thread starter
- #21
Mleta mada anajaribu kujenga hoja kwamba mwanza ilitakiwa ipate Maendeleo makubwa kwa sababu imekuwa ikiongozwa Na Chadema lakini imeshindwa: Na hivyo ndivyo itakavyokuwa Chadema ikishika dola!
kwanza hoja yako umeijenga kwa misingi dhaifu.
pili, umeshindwa kuzingatia kwamba Chadema sasa hivi haina dola, haina uwezo Wa kukasimu, na hata budget ikishapitishwa Chadema haina uwezo wa kupeleka Pesa kwenye manispaa zikatumike. Pesa wanazopata manispaa zinatoka serikali kuu inayoongozwa Na CCM, wakiamua kuwakwamisha wanawakwamisha.
Pia ni vizuri ukaelewa hizi Pesa za matumizi kwenye wilaya zinasimamiwa Na wakurugezi ambao ni waajiriwa Wa serikali. hivyo mkurugenzi anaweza kuamua kukwamisha Maendeleo ya mji kwa manufaa ya bosi wake
katika mazingira haya, Mchango mkubwa wa Meya na Madiwani ni kuhakikisha Pesa iliyopatikana haitumiki vibaya. Ingawa kuna pesa inayopatikana kwa kodi za manispaa Pesa hii ni kidogo
Familia iliyokamilika na kuwa na mshikamano, umoja, ustahimilivu na mwono wa mbali huishi kwa mwendo huo hata wakati wa kipindi cha ukata katika maisha yao. Kilichosababisha jiji la Mwanza kurudi mikononi mwa CCM si ukata wa pesa za maendeleo ingawa inaweza kuwa ni moja ya sababu kati ya nyingi. Kubwa zaidi ninaloona mimi ni follow up.
Ingefaa mmojawapo wa viongozi wa juu Chadema, labda Mnyika ambaye ndiye msemaji angekuja hapa atujibu hili, imekuwaje Madiwani wa Chadema kuwa na kura turufu ya kumwondoa Meya wao wakati walikuwa na nafasi ya kumtahadharisha mambo kabla hayaja haribika au pengine kama maji yalizidi unga, basi wangeyapeleka ngazi ya juu kupata ufumbuzi zaidi kuliko kusubiri moto unaunguza nyumba na kuita zima moto.