CHADEMA imeonyesha udhaifu kuongoza nchi, ijipange upya

Chadema haiwezi kuongoza nchi hii maana majimbo yao yoote yako hoi. Arusha ndo pyuuuuuuuu. Ubungo yalaaaaaa kawe ndo kasweeeeeeeee. Yaani shida tupu ngoja 2015 washikishwe adabu na wapiga kura sijui watawaambia nini conservative union
 
Tumeambiwa leo usanii wa chama fulani cha siasa kuvamia mitandao ya kijamii kugirubu watanzania ili kichaguliwe 2015. Magazeti yameongeza dau hawawezi kuyalipa. Tv ya babu anasema wanampakazia hahaha madaraka matamu eheee
 
Ungejaribu kusoma vizuri mada yangu na kuielewa, inaelekea bado hujaielewa vinginevyo usingeniweka moja kwa moja upande wa hasi badala ya upande wa chanya.

hata mimi sijaona mantiki ya wewe kukirudi chama. Nikuulize, kama viongozi wa juu wa chama wana uwezo wa kufanya mambo kwa maslahi ya chama na Taifa, wao ni nani hadi waweze? Na hawa madiwani na mameya si viongozi katika chama na serikali? Diwani si mtu mdogo. Ni mtendaji muhimu sana katika halmashauri na manispaa na kata watokako. Iweje arubunike tu kienyeji? Eti kisa uongozi wa juu hauko karibu nao. Una uhakika gani? na unaposema m4c ni chama inaonyesha ni jinsi gani unavyokebehi. Ni vyema kung'amua mapandikizi mapema na kuyaondoa kuliko kuhofia kubakiwa na mimea michache. Tutafika
 
Candid: Hoja yako ni ya msingi sana. Kuliko kulindana na kujidanganya kuwa mambo yatakuwa sawa kimuujiza ni vema kujisahihisha mapema kabisa ili makosa yaliyofanyika yasirudiwe. Lakini tukumbuke kuwa wanachama wengi wa CDM wamelelewa katika mazingira ya kimagamba. Wasiwasi wangu ni kuwa pengine wako wenye fikra za kimagamba na wanadhani nafasi walizo nazo ndani ya CDM wanaweza wakaendeleza yale ya CCM bila kuchukuliwa hatua. CDM ijitahidi kuwalea viongozi wake katika kila ngazi kwa kuwapatia elimu na kuwapa nyenzo za utawala bora ili iendelee kujijenga na zaidi kuwa kioo cha jamii kwa maana ya utawala bora uliotukuka.
 
Asante kwa mtazamo wako, lakini ungetambua kwanza kwamba mada hii inavyoendana na kichwa cha habari haihusiani na mfafanikio ya Chadema bali udhaifu kutokana ya ahadi yao ya kufanya jiji la Mwanza kuwa kielelezo cha uongozi bora unaotakiwa nchini.

Mkuu hakuna mafanikio bila matatizo especially kama anaehusika ni binadamu. Siipendi ccm na mfumo wake na jinsi ambavyo imeshindwa kusimamia raslimali za taifa na kuacha rushwa kutamalaki,lakini sibezi mafanikio na maendeleo yaliyoletwa na ccm kwa kipindi chote kilichokuwepo madarakani, as a thinker huwezi ukaongelea madhaifu tu pasipo kuhusisha mafanikio. Ni kutokana na kipimo cha ufaulu ndo tunatambua kufeli, huwezi ukaangalia mafanikio exclusively bila kuhusisha matatizo unless you are biased, come again mkuu.
 
Asante kwa mwono wako, ila kwa sasa hatuna muda wa kuendelea kujadili madhaifu ya CCM kwa sababu kila kukicha tunayaona na kuyajadili na katu hawabadiliki na ndiyo hali inazidi kuwa mbaya zaidi.

Chadema kwa vile wanaonekana kuwa ndio tegemeo la wengi kuokoa jahazi lisizame ndio maana tuko makini kuangalia mwenendo wao pale wanapoonekana kuteleza warudi kwenye mstari. Yaliyotokea Mwanza si jambo la kunyamazia, ni kosa la kiufundi na kisayansi katika mwenendo wa kujijenga kisiasa.

Ukweli huuma, hakuna sababu ya kufunikafunika ukweli kwani mficha ukweli huumbuka hadharani. Wenye moyo wa uzalendo wa kweli kwa nchi yetu tutaungana kuijenga Chadema kwa kusifia wanapofanikiwa na kuwashutumu wanapoleteza. Huku ndiko kujengana badala ya kuendeleza mambo ya kulindana kama wafanyavyo wale wa magambani.

Mimi nitaelewa ukiniambia kuwa CDM wamekosa umeya Mwanza wakiwa na madiwani wote kuficha ukweli wa kuligawa jiji la mwanza ili wapite kwa madiwani wao ni udhaifu wa kwa mtoa hoja nilidhani ungefanya hesabu kuwa idadi ya madiwani wote wa jiji hilo kabla ya kugawanywa ilemela na nyamagana wamefanya uchaguzi wa meya jiji la mwanza na CCM wameshindwa otherwise hujanishawishi hapa.
Pili, Nadhani CDM ndo chama kinachoweza kuiongoza hii nchi, Diwani asipofuata katiba yao hawawezi kumuuacha eti kwa sababu akifukuzwa wataukosa umeya mambo kama haya ndo yamefikisha nchi hapa tulipo, CDM wako tayali kupoteza watu wote kama hawawezi kufuata misingi na katika yao, kule A.town tuliona , mwanza pia kama kuna mtu anataka kufanya hayo mambo kuna usemi wa kwamba utawafukuza wangapi uko CCM tu, huku CDM hakuna kitu kama hicho.
MWISHO CCM WAMESHINDA UMEYA KWA SABABU WALILIGAWA JIJI LA MWANZA NA SIYO KINGINE TUWEWAKWELI KATIKA HILI.
 
Nakubaliana na mleta mada kwa asilimia kubwa sana, huu ndo ukomavu. Nakubali kabisa kwamba uongozi wa juu ulipaswa kuwa karibu na meya na madiwani wa mwanza kwa sababu ndiko walikosema wanataka kuweka mfano, naamini mtu muhimu zaidi kwenye hili alipaswa kuwa slaa mwenyewe kwa sababu akina mbowe wapo bungeni muda mwingi.
kama viongozi wangekuwa karibu na madiwani naamini wasingefikia mahali pa kumtosa meya wao wenyewe maana wangeweza kurekebishana kabla ya kufika huko kwenye kuaibishana. Kuna miaka miwili mbele kabla ya uchaguzi mkuu, kama hakutakuwa na kukosoana maana yake chama hakitkuwa na wakati wa kujirekebisha, hili litakuwa kosa kubwa sana kwa sababu wakati washabiki wataangalia chama kuna watu wasio na vyama wataangalia uhalisia wa mambo. Na endapo tulikosea na hatukujirekebisha tutarudi kwenye yaleyale ya kuibiwa kura nk.
Ukweli utatuweka huru ndugu zangu
 
Lets say Chadema wameshindwa kweli kama unavyotaka tuaminisha.Je inatosha kukupa nguvu ya kusema wakajipange?mangapi CCM wameshindwa na wanaendelea shindwa?Kwa miaka 50+ na bado hawajaweza jipanga.Ipi logic yako?Au wewe ndio wa kujipanga?
 
Chadema haiwezi kuongoza nchi hii maana majimbo yao yoote yako hoi. Arusha ndo pyuuuuuuuu. Ubungo yalaaaaaa kawe ndo kasweeeeeeeee. Yaani shida tupu ngoja 2015 washikishwe adabu na wapiga kura sijui watawaambia nini conservative union

nadhani huu ni utoto, watu wanajadili mambo ya msingi wengine wanajaribu kuweka ushabiki usio na maana, hivi majimbo uliyoyataja unaweza kuyaweka kama mfano wa majimbo yaliyo chini sana kimaendeleo kulinganisha na yepi? Na nadhani wabunge wa majimbo uliyotaja wanawajibika sana bungeni kuzungumzia kero za watu wao kuliko wengine. Tatizo ukiona vumbi ubungo ni ya mnyika ukiona lami ni ya ccm! Huu ni ufinyu wa fikra maana wabunge hawakusanyi kodi labda kama utanihakikishia kama wabunge wa kawe na ubungo nao huwa wana tabia ya kusinzia bungeni
 
Mkuu hakuna mafanikio bila matatizo especially kama anaehusika ni binadamu. Siipendi ccm na mfumo wake na jinsi ambavyo imeshindwa kusimamia raslimali za taifa na kuacha rushwa kutamalaki,lakini sibezi mafanikio na maendeleo yaliyoletwa na ccm kwa kipindi chote kilichokuwepo madarakani, as a thinker huwezi ukaongelea madhaifu tu pasipo kuhusisha mafanikio. Ni kutokana na kipimo cha ufaulu ndo tunatambua kufeli, huwezi ukaangalia mafanikio exclusively bila kuhusisha matatizo unless you are biased, come again mkuu.

Mambo mengi tunajadili, ukifuatilia mtiririko wa mada zangu utaona nadadafula moja baada ya nyingine ili kuweza kujitita vizuri katika jambo tunalojadili. Lengo ni kuleta mafanikio katika malengo ya kujenga taifa si kubomoa. Kilichotokea Mwanza upande wa Chadema si cha kufumbia macho, kuna umuhimu wa kujadili kwani hata kama kuna mbinu za kisiasa chadema nao wawe na mbinu za kisiasa kupambana nazo kwani ndio ushindani wa kisiasa.
 
Mimi nitaelewa ukiniambia kuwa CDM wamekosa umeya Mwanza wakiwa na madiwani wote kuficha ukweli wa kuligawa jiji la mwanza ili wapite kwa madiwani wao ni udhaifu wa kwa mtoa hoja nilidhani ungefanya hesabu kuwa idadi ya madiwani wote wa jiji hilo kabla ya kugawanywa ilemela na nyamagana wamefanya uchaguzi wa meya jiji la mwanza na CCM wameshindwa otherwise hujanishawishi hapa.
Pili, Nadhani CDM ndo chama kinachoweza kuiongoza hii nchi, Diwani asipofuata katiba yao hawawezi kumuuacha eti kwa sababu akifukuzwa wataukosa umeya mambo kama haya ndo yamefikisha nchi hapa tulipo, CDM wako tayali kupoteza watu wote kama hawawezi kufuata misingi na katika yao, kule A.town tuliona , mwanza pia kama kuna mtu anataka kufanya hayo mambo kuna usemi wa kwamba utawafukuza wangapi uko CCM tu, huku CDM hakuna kitu kama hicho.
MWISHO CCM WAMESHINDA UMEYA KWA SABABU WALILIGAWA JIJI LA MWANZA NA SIYO KINGINE TUWEWAKWELI KATIKA HILI.

Tusiangalie hoja ya kugawa jiji tu, kwani hata Chadema walipobaini wangeweza kuhamisha wabunge wakuteuliwa kutoka mkoa mwingine na kuwa wa Manza. Je, unasemaje kuhusu Madiwani kufukuzwa uanachama badala ya kuwapo adhabu nyingine ambayo ni onyo iwapo hilo ni kosa la awali, ni sahihi?
 
Nakubaliana na mleta mada kwa asilimia kubwa sana, huu ndo ukomavu. Nakubali kabisa kwamba uongozi wa juu ulipaswa kuwa karibu na meya na madiwani wa mwanza kwa sababu ndiko walikosema wanataka kuweka mfano, naamini mtu muhimu zaidi kwenye hili alipaswa kuwa slaa mwenyewe kwa sababu akina mbowe wapo bungeni muda mwingi.
kama viongozi wangekuwa karibu na madiwani naamini wasingefikia mahali pa kumtosa meya wao wenyewe maana wangeweza kurekebishana kabla ya kufika huko kwenye kuaibishana. Kuna miaka miwili mbele kabla ya uchaguzi mkuu, kama hakutakuwa na kukosoana maana yake chama hakitkuwa na wakati wa kujirekebisha, hili litakuwa kosa kubwa sana kwa sababu wakati washabiki wataangalia chama kuna watu wasio na vyama wataangalia uhalisia wa mambo. Na endapo tulikosea na hatukujirekebisha tutarudi kwenye yaleyale ya kuibiwa kura nk.
Ukweli utatuweka huru ndugu zangu

Umesoma vizuri hali ilivyo, tunataka wenye mwono kama wako, u mtume wa kufuatwa.
 
Chadema haiwezi kuongoza nchi hii maana majimbo yao yoote yako hoi. Arusha ndo pyuuuuuuuu. Ubungo yalaaaaaa kawe ndo kasweeeeeeeee. Yaani shida tupu ngoja 2015 washikishwe adabu na wapiga kura sijui watawaambia nini conservative union

Jaribu kujibu hoja ya msingi kwa haja pambanuzi badala mtindo wa mipasho haitatujenga, hii nchi yetu sote na kila atakayechukua nchi kufaidika au kutofaidika ni sisi sote.
 
Candid Scope anasisitiza sana tukubali kwamba viongozi wa kitaifa wa CDM wamekosa. Hilo amerudia sana kulisisitiza, na kwamba hii ni ishara ya kutoweza kuongoza serikali (kukamata dola). Anasema tukishakiubali wamekosa basi watajipanga upya.

Hakuna uthibitisho kwamba viongozi wa kitaifa wa Chadema hawakujaribu kushughulikia matatizo ya Mwanza kimya kimya kabla hayajafikia hali mbaya. Ni lazima kuwaadhibu vikali wasaliti. Diwani anayeweza kuungana na CCM ili kuidhoofisha CDM si wa kusahihisha, ni wa kufukuza uanachama.

Candid Scope ameleta mada hii ili kuimarisha CHADEMA? Idoubt that. Kutokana na mada zake nyingine ni mpenda mageuzi, lakini mada yake ya sasa inachangia kudhoofisha wapenda mageuzi. Hatakubali hayo, kwani inaelekea ameamua lazima tukubaliane naye tuwalaumu viongozi wa kitaifa wa CDM.
 
Wanajamvi tunatakiwa kujua kwamba pale Mwanza kulikuwa kuna ushindani mkubwa sana wa kiuongozi kati ya ccm na cdm.Viongozi wa cdm walikuwa wanapambana kuonesha uma kwamba uhalisia wa cdm kuongoza nchi ni upi lakini wakati ccm wenye mkuu wa mkoa, mkurugenzi wa wilaya, mkuu wa wilaya na watendaji wengi wenye uwezo wa kifedha pamoja na madiwana wa walipambana kuonesha cdm haiwezi kuongoza jiji la mwanza na pia kumbuka madiwani wengine ni watu ambao walitoka ccm muda si mrefu kwa hiyo wapo madiwani wa cdm walionunuliwa kumwangushwa mayor na pia ukumbukwe hata kama mayor angebaki asingepata ushirikiano kutoka kwa hawa viongozi wenzake kutoka ccm. Mm nadiriki kusema ccm ni wabaya sana wanaendeleza chuki hadi kwenye utendaji.MM sijui kama cdm walilijua hili lkn kwa sasa watakuwa wamejifunza.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom