CHADEMA imekosa dira na mwelekeo

CHADEMA imekosa dira na mwelekeo

Hii tune ya CHADEMA kukosa dira na mwelekeo haina collabo yake? Maana yake miaka nenda miaka rudi ni hiyohiyo lakini inashindwa kuhit huku CHADEMA kikizidi kuwika na kuchanja mbuga

Kaka yangu na hao wanaojiona ni wazee kwenye siasa sasa hivi wanakimbilia kwenye UBAGUZI wa RANGI,baada ya ule wa UDINI na UKANDA kushindwa
 
hiki chama kilijinasibu kuwa chama cha kupinga ufisadi. baada ya kukumbwa na tamaa kali na kiu ya pesa iliyopindukia kikakumbatia mafisadi akiwemo fisadi Lowassa. hivi sasa chama hicho kimekuwa kama kisu butu.. hakina uwezo wala uthubutu wa kutoka hadharani kukemea ufisadi wala uovu wa aina yoyote kwa sababu chenyewe ndio kinara wa uovu hivyo ni genge la wasakatonge na wahalifu wajasiriamali wa kisiasa.

Jamani, naludia kuwaasa,
WENGINE HAMIENI FACE BOOK, inawezekana michango na utumbo wenu usio weza saidia jamii utahit huko.

Sasa hoja ni ipi, uchaguzi ushaisha ni mda wa TATHIMINI na kujipanga upya.
 
ACT kuwa chama cha upinzani sahau ila labda waungane na magamba 2020 coz gamba linatoka likishatoka wataunda umojawao utaunganisha vyama vya ACT.CCM.ADC. ambapo 2025 zito atagombea ktk umoja wao na AMad rashid atakua mgombea mweza january nape na mwigulu watakuja UKAWA alafu nape atasafisha kauli yake ya goli la mkono mbele ya MAKAMANDA wote wa ukawa
 
Kweli viongozi wa chadema hawana uwezo wa kupinga ufisadi lakini wanachama wa chadema bado wanachukia ufisadi. Chadema inatakiwa isafishwe kwa kuondoa uongozi ulikuwepo madarakani ili chama kijisafishe.
Jifunzeni kwa CCM, wamefanikiwa kuwatowa mafisadi kama lowassa na wenzake, na kufanikiwa kuchukuwa urais na viti vingi vya ubunge. JPM akichukuwa uongozi wa chama mafisadi zaidi wataondolewe kwenye uongozi.
Nashukuru sana wewe ndio unaijua siasa ya Tanzania hao wengine ni ushabiki tu
Cha msingi kama chadema inataka IRUDI vizuri inaibidi ijifunge mkanda kisawasawa kwa kujisafisha na safari hii waondoe ule ukanda ili propaganda zisipate nafasi

Nakuomba kama unaeza andaa post ya nini kifanyike na jinsi ya kujisafisha
By the way nakuunga mkono
 
Mbona Magu kaendelea kuwateua mafisadi kwenye serikali yake? Mf.Yu;le aliyoko pale nishati na madini, aliyekwenda kuwa Naibu kamishina TRA na bado wabunge mafisadi wengi wapo mjengoni na wengi wao watapewa uenyekiti wa kamati za Bunge.
 
Cha msingi kama chadema inataka IRUDI vizuri inaibidi ijifunge mkanda kisawasawa kwa kujisafisha na safari hii waondoe ule ukanda ili propaganda zisipate nafasi

Ukanda utaondokaje wakati Kanda zingine Wanachama wenye uwezo hawajitokezi kugombea? Hivi umejiuliza kwenye mikoa ya Kusini, kati, kanda ya Ziwa ni kiongozi gani ambaye unahisi anaweza kuchukua uongozi wa Juu ndani ya CDM? Nipe mfano kwa kuwataja majina.
Pia niambie kwanini ndani ya CCM mawaziri wakuu wengi wametoka Mkoa wa Arusha kuliko mikoa mingine na mingine haijatoa kabisa? Mfano: Sokoine, Lowasa, Sumaye,Msuya
Pia niambie ni Mbunge gani wa kanda nyingine mwenye influence kubwa ndani ya Mkoa, Jimbo ukiacha wale Wabunge wa Kaskazini?
Niambie ni majimbo gani yaliyopo Tz bara ambako mpinzani ameweza kushinda kwa vipindi vitatu mfululizo ukiacha yale ya kaskazini?
Niambie ni kiongozi gani wa ccm au cdm au cuf ambaye ana nguvu kwenye kanda yake akasimama kwenye kugombea Urais na Mkoa wake acha kanda ikamsapoti kwa kumpa KURA nyingi.
Niambie kwanini wakaskazini wamejaa kwenye Ngazi za Juu za serikali, mashirika ya umma na binafsi Tz nzima kushinda kanda zingine?
Kwanini wanasheria wakubwa na maarufu wengi wanat kaskazini?
Na mengine mengi siwezi kuyaorodhesha hapa.
Hivi unategemea Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CDM atoke Dodoma wakati uyo kiongozi hana uwezo wa kushinda hata Udiwani kwa uchaguzi mmoja? Halafu aende kuwaambia watu wa Moshi mchagueni huyu awe Mbunge wakati yeye mwenyewe ameshindwa nyumbani kwake.
Jamani tuache masihara kuongoza chama cha Upinzani Tanzania na kufikia mafanikio ya CDM au CUF ni kazi kubwa sana nakumbuka OSCAR KAMBONA alijitahidi sana kuijenga TADEA Mkoani Ruvuma lakini hakuthaminiwa na kusapotiwa na wana Ruvuma hakuwahi hata kushinda UDIWANI au ujumbe.
Vyama vya Upinzani kutengeneza Ngome sehemu unayokubalika ni kete Muhimu sana na si CDM tu hata CUF wamejikita Pemba, CDM kaskazini na hata ACT wamejikita pale Kigoma.
Cha msingi ni kuwashauri Wasomi na watu wenye uwezo na ushawishi wajiunge na Vyama vya Upinzani au waanzishe na kutengeneza ngome kwenye maeneo yao wanayokubalika.
 
hiki chama kilijinasibu kuwa chama cha kupinga ufisadi. baada ya kukumbwa na tamaa kali na kiu ya pesa iliyopindukia kikakumbatia mafisadi akiwemo fisadi Lowassa. hivi sasa chama hicho kimekuwa kama kisu butu.. hakina uwezo wala uthubutu wa kutoka hadharani kukemea ufisadi wala uovu wa aina yoyote kwa sababu chenyewe ndio kinara wa uovu hivyo ni genge la wasakatonge na wahalifu wajasiriamali wa kisiasa.
sumu haionjwi. sumu ya kubadili gia angani inaitafuna cdm.
 
ACT ni tawi la CCM,...kwa anayeelewa siasa ya TZ
CDM ndio tawi la CCM....kingunge, Msindai, Mahanga, Masha, Lowasa, Lembeli, Sumaye, Sinare, Bulaya n.k.......hawa wakiamua wanaweza kurudi muda wowote tunduni mwao....

Haya niorodheshee majina ya wanaccm waliopo ACT Wazalendo.
 
hiki chama kilijinasibu kuwa chama cha kupinga ufisadi. baada ya kukumbwa na tamaa kali na kiu ya pesa iliyopindukia kikakumbatia mafisadi akiwemo fisadi Lowassa. hivi sasa chama hicho kimekuwa kama kisu butu.. hakina uwezo wala uthubutu wa kutoka hadharani kukemea ufisadi wala uovu wa aina yoyote kwa sababu chenyewe ndio kinara wa uovu hivyo ni genge la wasakatonge na wahalifu wajasiriamali wa kisiasa.
Yaelekea ccm mmeumia sana lowasa kuhamia chadema .Naomba nikuulize Tanzania nzima fisadi ni lowasa tu? Kwan ccm hakuna mafisadi. Chadema kipo Na kitaendelea kuwepo utakaa sana kusubiria chadema kife naona hiyo itakuwa ndoto ya mchana . Kila cku lowasa fisadi alishawaambia muende mahakamani mkamshtaki kama yy ni fisad sasa unangoja nini?
 
TUNASUBIRI ACT WAZALENDO KUWA CHAMA KIKUU CHA UPINZANI 2020 WAKATI CDM IMEFARIKI
Hakika hizo ni ndoto za Alinacha!!
ACT Wazalendo chini ya Mzito Kabwela- ZZK ni CCM B na ndiyo maana kimepoteza jmaarufu kiasi cha kuambulia Mbunge 1 tu nchi nzima!

ACT huwezi linganixha na CHADEMA hata kwa nyukta moja. Pale hakuna Chama.mazee. Kwa uhakika zaidi linganisha kura alizopata mgombea wa CHADEMA Mh.Lowasa na mgombea wa ACT Anne Mghwira utapata picha halisi!
 
Act ina mwaka mmoja
tayari inaongoza halmashauri
 
hiki chama kilijinasibu kuwa chama cha kupinga ufisadi. baada ya kukumbwa na tamaa kali na kiu ya pesa iliyopindukia kikakumbatia mafisadi akiwemo fisadi Lowassa. hivi sasa chama hicho kimekuwa kama kisu butu.. hakina uwezo wala uthubutu wa kutoka hadharani kukemea ufisadi wala uovu wa aina yoyote kwa sababu chenyewe ndio kinara wa uovu hivyo ni genge la wasakatonge na wahalifu wajasiriamali wa kisiasa.

du,tayari hii ni dalili ya kipindupindu wahi ilala,AMANA
 
Wasira alisema kabla ya 2015 chadema itakufa, matokeo yake kauwawa yeye na binti mdogo kutoka chadema.
 
Wasira alisema kabla ya 2015 chadema itakufa, matokeo yake kauwawa yeye na binti mdogo kutoka chadema.
Wasira ni Mzee above 70 unahangaika nae Wa nini??

Hebu tuambie ni kwa nini Vincent nyerere, wenje ,kiwia wamegaragazwa!?!
 
Back
Top Bottom