Chadema imejaa watu wabunifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema imejaa watu wabunifu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Sep 7, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  • Mfumo wa kuchangisha fedha kwa SMS wazua mjadala  [​IMG]
  MKAKATI mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kuanzisha mfumo wa kiteknolojia kuchangisha fedha na kusajili wanachama, utakaokiwezesha kupata mamilioni ya wanachama kupitia simu zao za mkononi, umekitisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuibua mjadala miongoni mwa watendaji wake.
  Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam, zilisema kuwa mara baada ya CHADEMA kutangaza kuzindua mfumo huo wa kisasa, baadhi ya watendaji wa idara ya uenezi walijadili kwa kina faida za mkakati huo na kukiri kwamba unaweza kukijenga zaidi chama hicho na kukusanya mabilioni ya fedha za kampeni.
  Kwa mujibu wa habari hizo, CCM ilikuwa na mkakati wa aina hiyo ambao ulitarajiwa kuzinduliwa mwakani, miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu, hivyo walikiri kuwa CHADEMA imewazidi ujanja kwa kuwahi kuzindua mpango huo kabla yao.
  “Watendaji wa ofisi ndogo tulijadili sana suala hili, kwa kweli kama mpango huo utafanikiwa kwa wananchi kuunga mkono, hakika CHADEMA haitashikika mwakani,” alisema mmoja wa viongozi wa idara hiyo kwa sharti la kutotaja jina lake.
  Mbali ya watendaji hao, baadhi ya wabunge wa CCM, waliozungumza na Tanzania Daima kuhusu mkakati huo, waliipongeza CHADEMA kwamba imezungukwa na vijana wadogo, lakini wabunifu.
  “CHADEMA ina vijana wadogo, lakini wana akili na wabunifu. Watu wa aina hiyo ndio wanaofaa kukaa makao makuu ya chama chetu, ila tuna bahati mbaya tumezungukwa na wazee, kazi yao ni kupiga majungu kwa Katibu Mkuu Yusuf Makamba muda wote ili awape pesa, hawana kitu kipya cha kubuni, hii ni dunia nyingine, lazima tuwe wabunifu,” alisema mmoja wa wabunge wa CCM kutoka mkoani Mbeya.
  Hivi karibuni, CHADEMA iliweka historia ya kuwa chama cha kwanza si tu hapa nchini, bali pia barani Afrika kwa kuanzisha mfumo huo unaotumiwa na vyama vya siasa katika nchi zilizoendelea za bara la Ulaya na Marekani.
  Mpango huo unaotumia teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama), ulizinduliwa na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe aliyechaguliwa tena kuongoza kwa miaka mingine mitano.
  Mfumo huo ambao unatarajiwa kuanza kazi wiki hii, utamwezesha pia kila mwanachama wa CHADEMA, shabiki na wananchi wote, kukichangia sh 300 kila mwezi, kusaidia harakati zake za kujiimarisha na kukusanya fedha za kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwakani.
  Mbowe ambaye ndiye mwaasisi wa mpango huo, alisema utakiwezesha chama hicho kuwa na oganaizesheni ya kiteknolojia, sambamba na oganaizesheni yake ya sasa ya matawi na vikao vyake vyake vya kichama.
  Alisema ili mtu aweze kuichangia fedha CHADEMA na kuwa mwanachama wa chama hicho kama akipenda, itampasa kutuma ujumbe mfupi wa simu yake ya mkononi (SMS), bila kujali aina ya mtandao anaotumia, wenye neno ‘CHADEMA’, kwenda namba 15710 na baada ya kufanya hivyo, atakuwa akikatwa sh 300 kila mwezi.
  Mbowe alisema baada ya ujumbe huo, mwanaharakati huyo atapewa fursa ya kuwa mwanachama wa CHADEMA kama anapenda na atakuwa akitumiwa taarifa mbalimbali za chama hicho mara kwa mara kupitia simu yake ya mkononi. “Akitaka kuchangia zaidi ya sh 300 ndani ya mwezi mmoja, anapaswa kutuma neno ‘CHADEMA’ mara nyingi atakavyo na kwa kufanya hivyo, atakuwa akikatwa sh 300 kila wakati kadri apendavyo kwa mwezi huo,” alisema Mbowe. Kwa mujibu wa Mbowe, chini ya mpango huo, CHADEMA inataweza kuongeza mamilioni ya wanachama kila mwezi kutoka kwenye wanachama 900,000 iliowaandikisha kwa utaratibu wa kawaida wa kadi za uanachama, kwani imelenga kupata angalau watu milioni tatu watakaokuwa
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 10,648
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  ccm na kauli mbiu ya zidumu fikra za mwenyekiti..........hakuna ubunifu wowote wanahofanya sasa ni kutafuta mchawi anae tishia kuvuruga ULAJI wao,wanahaha kuwashughulikia wapinga ufisadi.Wamechoka kufikiri.Acha ndege walio nje ya tundu(nje ya ccm) waendelee kufurahia uhuru wao wa kufikiri na kuwa wabunifu.......big up kwa chadema na wanachadema
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hakika hizi ni Habari njema kwa wote ambao sio mafisadi kuungiza pesa chafu katika siasa za Tanzania hivyo kuna ulazima wa kuchangia CHADEMA. CCM wanawaza mbinu chafu za ushindi tu na za kishetani kama zile za EPA na madudu mengine
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Je, kuna utaratibu wowote umeandaliwa kwa walio nje ya Tanzania kutumia SMS kuichangia CHADEMA? Naomba mhusika yeyote wa CHADEMA anisaidie jubu, either Mnyika au Zitto, au yeyote.
   
  Last edited: Sep 7, 2009
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Chadema
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Sasa wafikilie namna watakavyokuwa wanatoa report za fedha (mapato na matumizi very simple) kwa njia hii ya mtandao. Itawapa watu imani, kwa mfano wakiwa kila mwezi wanasema tumepokea wanachama kadhaa na sh. kadhaa na tumetumia kadhaa simple like that itawafanya watu wawe na imani na CHADEMA zaidi
   
 7. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakubali wakuu.
  CHADEMA iko vizuri kila idara.
  Cha msingi ni wapiga kura wapenda maendeleo kujiandaa kuipa CHADEMA kile inachostahili katika uchaguzi mkuu ujao.
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,837
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana nina suggest kwamba akina Komu waache kutunza pesa Chadema wawe na accountant ambaye hafanyi kazi ya siasa hata mara moja ila awe mwana chadema anaye kipenda Chama kutunza hesabu.Chadema wanakuwa wanahitaji a full Finance Dept na si mtu mmoja anafanya yote .

  Accountant
  AP /AR
  Kuwe na P & L
  if possible iwe computerised Accounting

  Controller

  nk .

  Watu wa magumashi hapana lete hasabu na taarifa kila mara si dhambi ukiwaaambie wanachama na wapenzi wa Chadema juu ya kiasi kilicho kusanywa na matumizi yake mwa Mwezi .Chama ni mali ya wananchi na viongozi ni dhamana wanapewa .
   
 9. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wanaweza pia kupata wanachama wengi na support zaidi kwa kutumia Facebook na mitandao mingine. Huko, wanaweza kuelezea mambo mengi zaidi na kwa watu wengi zaidi kuhusiana na chama hicho. Wanaweza pia kujenga uhusiano wa karibu na watanzania wanaoitakia mema kwa kujitambulisha kwa ufasaha na kujibu maswali ya watu wanaotaka kuwajua
   
 10. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,708
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  dada yangu wazo lako ni zuri lakini sio kila mwezi, wanatakiwa watoe ya mwaka, kwa ajili kuandaa financial statement ni gharama sana. wakiwa wanatoa financial statement kila mwezi utakuta wanatumia hela/mda nyingi kwenye kuandaa statement kuliko kukuza chama
  statement lazima ihakikiwe na auditors bila hivyo itakuwa haina maana yeyote
  labda kama unataka page moja ambayo itakuwa haina maana yeyote..

  hata hivyo sasa hivi mahesabu yao yatakuwa yanakaguliwa CAG, baada ya kukaguliwa na CAG nadhani wataweza kuyaeka bayana watu wayaone
   
 11. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa. I want to start following them on twitter soon!
   
 12. A

  Audax JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  big up chadema. Wanawaza mbali zaidi ya chama chetu kile.
   
 13. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kaka asante kwa mtazamo wako lakini nikiwa simple member ambaye sijui hayo mabalance sheet wala mafinancial statements, kwangu mimi nahitaji kusikia Zilizokusanywa - Zlizotumika = Balance (zilizobaki -/+) Kwisha. Hizi habari za kufunga mavitabu, sijui ukaguzi wa CAG nk yatafuata baadaye, after all nikionyeshwa wala sitalewa. Hiyo Lugha ya assets na liability mnailewa nyie huko juu, sisi tunajua column mbili tu, mapato matumizi kisha neno jumla na Baki!

  Sidhani kama hakuna Monthly report, how are they organised, that is what i want to hear. I think it is possible to understand how many people are enrolled and registered by the party and how much was contributed they can just diseminate such kind of information through an sms to my Mobile.

  How comes to collect funds should be easy through sms, to provide reports should be the opposite, I can not understand? From mys simple reason if you can get funds through mobile you should aslo be able to give reports by mobile too
   
 14. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,708
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  dada yangu most big companies wanatoa quarterly reports, ninachosema mimi ni time na gharama za kutengeneza report kila mwezi...
  hela tunazochanga ni vizuri zikatumika kupanua na kuendesha chama na sio katika "kupiga mahesabu ya hela zilizokusanywa". ukiwa unatengeneza report kila mwezi utakuta unatupia hela nyingi kutengeneza monthly report na sio kupanua chama..
  I would be happy with annual audited financial statement
  wakikupa mapato na matumizi ya mwezi dada yangu haina maana kwa ajili haujui hiyo hela imetumika kwa nini na nini, ukitaka detailed report gharama zinapanda
  note:I am not one of chadema employees
   
 15. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nina Hakika Sisi Vijana wengi tulio ndani na Tanzania tuna ufahamu jinsi gani ya kuchezea mitandao ya internet na pia kuna page chungu mzima kwa ajili ya kuweka na kutunza taarifa nyingi kwa faida ya CHADEMa na pia itakuwa jambo la busara kama wakiwa kwenye facebook, myspace, hi5 na social network nyingine huko kuna vijana wengi sana na Marafiki wa CHADEMa, CHADEMA tupo pamoja kwa kila kheri katika Taifa letu la Tanzania
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hongera kwa kazi nzuri na Busara zenu wote.. Lazima siku watashinda chaguzi hapa Tanzania
   
 17. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hiki ndicho chama chenye fikra mpya kuikomboa tanzania kutoka katika makucha ya wakoloni weusi,
   
 18. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hiki ndicho chama chenye fikra mpya za kuijenga tanzania mpya, tuwaunge mkono hima
   
 19. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hakika nakubaliana na wewe kwa yote yale na pia zile fikra za wakati ule wa Mwalimu zimehamia zote CHADEMA
   
 20. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mkuu hiyo system unayotumia wewe ni system gani unayohitaji kutengeneza report kwa kutumia pesa? CHADEMA ina wahasibu wataalam, na siku hizi kuna software kibao za kihasibu, kila kitu kipo connected automatically. Ni suala la Click moja unapata Financial Statements. Kama hawataweza kutoa hiyo report ya mwezi basi nikubaliane na wewe kuhusu Quartely report, lakini unaponiambia kuwa it is very expensive to prepare finacial report hapo mkuu siwezi kuafiki kabisa, tena sielewi.

  Kama tunania ya kutengeneza mafisadi wengine ndani ya chama, Financial report sio kitu muhimu. Sisi Bongo lala Tunaweza kwa kutumia Xcell tukaunganisha Petty cash, Invoices, Receipts, n.k kwa click moja nikapata balance sheet, sasa huyu mtaalam wa Mafedha anayesaidiwa na advanced program ya kihasibu kwanini asitoke na report in three days??? Kwanini asifanye bank Reconciliation kwa masaa???

  Tuwasaidie kuwa CHAMA makini, kama tutawashangilia tu bila kuwapa tahadhari watatumbukia shimoni. Haya malalamiko ya pesa zinatumika makao makuu tusingekuwa tunayasikia, malalamiko kuwa pesa zinalipa madeni sijui ya M/kiti na helicopter yasingeweza kuwa justifiable. Kwanini hizi Financial reports hazibandikwi kwenye website yao? Mwanakijiji anatoa Finacial report yake kila mwaka sembuse CHAMA khaaaa!

  Mkuu mimi nilitoa Ushauri wa Bure, na ukitoa ushauri sio lazima uchukuliwe na wewe sio kiongozi wa CHADEMA kwa hiyo hatuna haja ya kubishana sana, Tufunge mjadala, Hongera CHADEMA kwa hatua mliyopiga, Lakini ukikusanya cha mtu kumbuka kumpa taarifa umekitumiaje!
   
  Last edited: Sep 8, 2009
Loading...