Chadema imefanikiwa kutoa somo la uraia nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema imefanikiwa kutoa somo la uraia nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 8, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kwa mtazamo wa haraka na ninavyoona kada mbalimbali zinavyoamka kudai haki zao za msingi na jinsi serikali haikujipanga kufanya mambo kwa utaratibu unaweza kuaminika na kukubalika ni dhahiri elimu ya uraia ya Chadema imewafungua akili wengi. Serikali ijue sasa wananchi wameanza kuelewa nini serikali inatakiwa iwafanyie na haki zao za msingi haziwezi kuwekea rahani maisha yao kwa ajili ya wachache wanaonufaika na matunda ya mti tunaomwagilia wote.
   
 2. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kaka umeweka kisu kwenye mfupa. U have hit the nail on the head. Tehe tehe tehe. Kitu kingine cha muhimu kabisa ambacho kinapaswa kuendelea kueleweka kwa watu, Watanzania ni juu ya dhana na msingi wa amani na utulivu vinavyoimbwa na watawala kwenye majukwaa, maneno bila vitendo. Sasa wananchi wanaanza kuelewa na wanapaswa kuendelea kuelewa kuwa msingi wa amani na utulivu ni utendekaji wa haki na matumaini waliyonayo wananchi kwa uongoz/viongozi.

  Vinginevyo, tutakuwa tunaelekea kubaya. Walioko madarakani ambao wamejigeuza kuwa watawala badala ya kulongola njia, kama ilivyo mantiki ya uongozi, wanapaswa kujua kuwa umma sasa umeamuka, wanataka kuona uwajibikaji wa serikali na viongozi wake katika kutengeneza fursa za Watanzania kutoa jasho lao na kujienedeleza. Umma umetekeleza wajibu sasa unadai haki. Unataka wajibu na haki viende sambamba na ionekane hivyo. Aluta continua mkuu.

  Ni class struggle ya wazi kabisa. Kupigania haki na wajibu. Panapokuwa na uminywaji wa haki, ukiamua kuwa neutral, umechagua kuwa upande wa mvunja haki na mkandamizaji.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Bado haijafanikiwa hasa katika eneo la madhara ya uhuru wa kutoa taarifa kwa umma kama hauna uhakika nazo. Jf tumekuwa wakati mwingine tunatengeneza taarifa za uongo na kuzirusha humu kwa lengo la kuijeruhi CCM au Chadema lakini kumbe tunaijeruhi nchi yetu. Bado hatuna utaifa.
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nchi ni kubwa kazi hii sio ya muda mfupi hata kama chadema ina lengo hilo. Chadema haijafanikiwa.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  PEOPLEeeeeeeeeeeeeeeeeeees Poweeeeeeeeeeeerrrrr!
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Katika uwanja wa mapambano madhara ya wasiohusika na mapambano hayawezi kuepukika. Watakaofaidi matunda watajua historia ya waliotengeneza njia ya kufikia walipo.
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,783
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Kabisa Mkuu. Hata hivyo, pamoja na CHADEMA kufanya mengi, bado Mkutano wa Septemba 15, 2007, Mwembeyanga, Dar es Salaam utabaki katika historia ya vizazi na vizazi kama mwanzo mpya wa taifa letu. Mkutano huo uliokuja na hitimisho lililoitwa "Orodha ya Aibu - List of Shame" neno kuu likiwa UFISADI kwa kuthubutu kuwataja mafisadi HADHARANI hakika siku hii itabaki katika historia.

  Kama mnakumbuka akina Makamba (former CCM Secretary General) na wenzake wakaibuka wakijidai eti neno UFISADI halikuwa katika KAMUSI YAO (ya CCM) lakini leo hadi Mwenyekiti wao anaimba na kucheza ngoma ya UFISADI; labda wamesharekibisha hiyo kamusi waliyoikana mwanzoni!

  Kwa wale ambao hatukuwepo wakati wa Uhuru wa kwanza wa Mwl. Nyerere (Desemba 9, 1961) angalau Septemba 15, tuliweza kushuhudia Uhuru wa Pili wa kimawazo, kifikra, uthubutu, na mwanzo mpya chini ya Dr. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa Chadema na makamanda wenzake.
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama maandamano yao yanakubalika kwa nini wamesitisha? Si wameona hayaleti manufaa kwao bali ni kujazana na kesi mahakamani?
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Maneno mazito sana mkuu wangu! Tena ya ujenzi.
   
 10. N

  Njele JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naridhia hoja hii na hoja yako kwa kuwa hapo awali kabla Chedema kuwa Chama kikuu cha upinzanii haikutokea hali ya derikali kunyoshewa kidole na wananchi, lakini sasa hivi naona mambo yameanza kuiwia vigumu serikali kuendesha mambo kiulaini kama ilivyozoea.
   
 11. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  dalili za ukimwi tunaambiwa kutoka vidonda midomoni, kuhara, na homa za mara kwa mara na dalili ya mvua wanasema mawingu ,dalili za chadema kufanikiwa wananji kugomea malipo ya dowans, migomo ya wanafunzi migomo ya madaktari wananji kuwatimua wabunge wao hasa wa magamba majimboni wanapopeleka hoja mbalimbali; mkuu haitajiki mizukulu jilala kukufahamisha kuwa hawa jamaa wamefanikiwa sana tena sana tu na baaaaaaado kudadadadeki mtatafuta pa kutokea
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Haswaaa, maana wanavyozidi kukorogana hata mfano wa historia ya nchi yetu haijapata kutokea. Hali hiyo ndiyo iliyonifikirisha kuona kama elimu ya uraia itolewayo na Chadema imeanza kuwaingia watu. Walithubutu kutamka siku za nyuma kwamba Chadema wanafanya nchi isitawalike, hii ni kutokana na kuzoea kuwaendesha watanzania kama gari bovu.
   
 13. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  unajua candid scope mambo yanavyotokea hivi sasa licha ya chadema kutoa elimu ya uraia pia mitendo michafu inayofululiza inayofanywa na hii migamba inaaccerelate hii motion na main problem this people already reach the point of non return they can not, shall not and will not change and by any means we have to chase them out 2015 na hii wakishinda kwa matendo yote waliyofanya tutawawatoa kwa ngumi
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hawajasitisha mkuu. Yako kwenye pause tu. Kikao cha bunge kitakapomalizika yataanza tena: Mwanza, Mbeya, na this time Darisalama.
   
Loading...