CHADEMA imchunguze Mohamed Mtoi

Status
Not open for further replies.

Joseph Ludovick

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
382
Reaction score
506
Mohamed Mtoi, anafahamika sana hapa lakini siyo wengi wanajua historia yake. Kufuatia hayo, yaliyomsibu kwa sababu ya CHADEMA, ni jambo la kuangalia kwa makini sana mintarafu usalama wa chama na viongozi wake.

Nashauri haraka na lazima,idara yetu ya ulinzi na usalama,na inteligensia, ihakikishe Mtoi hakutani na dokta Slaa na Mbowe akiwa peke yake.

Kwasababu ya uharaka na unyeti wa jambo hili,nategemea ujumbe huu utafsiriwe katika proper context, ndiyo maana nimeandika kwa jina langu.

Nimeshauri


 
Mohamed Mtoi ni mwanachama na mtendaji wa chama aliyekabidhiwa majukumu na anayatimiza kadri inavyotakiwa.

Yuko anatimiza majukumu yake kwa chama kama kawaida. Anatimiza wajibu wake kama mwanachama. Anawajibika kama mtendaji kwa kadri ya nafasi yake.

CHADEMA au viongozi wake, hawapangiwi wala kupokea ushauri wa namna ya kusimamia, kuendesha chama au utendaji kazi wa kila siku kutoka kwa CCM na washirika wao (its cronies as I normally write).

Mleta mada anayo fursa nzuri ya kupeleka ushauri wake CCM ambako bila shaka wanamwamini zaidi kama sehemu ya vijana wao.

Mleta mada huyu angeshauriwa atumie fursa aliyonayo ya mawasiliano ya siri na wazi (kama alivyofanya hapa), aungane na wenzake kwenye lile tawi jipya la CCM, kuwapatia ushauri kama huu watu wa Lumumba au pale White House Dodoma.

Awashauri badala ya kufungia magazeti wafanyie kazi facts zinazosemwa na Magazeti mathalani tukio la kutekwa, kuteswa na kutaka kuuwawa kwa Dkt. Ulimboka.

Awashauri kuwa waache kufanya au kupalilia mauaji kisha wanawatuma mawakala wao kusema Ni Chadema.

Alipaswa awe amewashauri 'wenzake' wafanye uchunguzi wa kina na kuchukua hatua kwenye
 
unajua some time we jamaa sikuelewi uko upande upi? upande wa CDM or against CDM
 

Mmh! Ndumira kuwili a k a Msaliti at work...hivi wewe ni Chadema au ni ACT? Alafu hicho ulichoandika mbona hakieleweki?
 
Isee sijaelewa makamanda mna maana gani.
Ngoja aje mwingine huenda ntaelewa vizuri.
 
mwacheni kijana amechanganyikiwa, atakapo kuwa mtu mzima na kuanza kijitambua ataacha ujinga huo anaoufanya, hawezi akawa na akili timamu huyo. haeleweki yuko CDM au CCM, au ndo njaa inamtesa
 

Ahsante sana TumainiMakene...kwa kombora lako hili moja ni jibu tosha kwa mleta mada hii. Am sure hawezi kurudi tena hapa.
 
Last edited by a moderator:
post za kimkakati toka ACT

hii ni ya pili baada ya comment ya jana kwenye uzi wa kum attack Saanane
 

inapendeza kuona mnawajua vizuri viongozi wenu walivyo madikteta
 
post za kimkakati toka ACT

hii ni ya pili baada ya comment ya jana kwenye uzi wa kum attack Saanane
ACT mtawachukua sana lakini kiuhalisia wanawajua vizuri sana viongozi wenu, ni vigumu sana kutoamini yanayosemwa na ACT kuhusu viongozi wa CHADEMA na hasa MBOWE na SLAA
 
Mohamedi Mtoi. Angalia alama za nyakati ndugu yangu. Madam umezungukwa na kina Masawe, Mangi, Mungi na kina John ima ukubaliane na matakwa yao au uitwe Msaliti kama Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Isee sijaelewa makamanda mna maana gani.
Ngoja aje mwingine huenda ntaelewa vizuri.

Mkuu mada haijaletwa na Kamanda, imeletwa na Msaliti mtumishi wa ACT, huu ni ule mwendelezo wa wana genge kujitoa ufahamu
 
CCM wewe, Chadema wewe, ACT wewe...hivi hamuoni kama mnajidharirisha? Chagueni chama kimoja na mtulienacho.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…