wananchi wanachanga mil 300, chadema wanatumia billion 3. We hujiulizi hizo zingine zinatoka wapi? Au wanamajini yanayo leta hela?
Mkurugenzi wa fedha na utawala wa CHADEMA Anthony Komu alikuwa Channel Ten akimchanachana NAPE juu ya tuhuma zake juu ya CHADEMA kupokea fedha kutoka nje na kwamba inafanya usanii katika harambee zake.
Komu anasema ni kweli CHADEMA inashirikiana na KAS shirika la Kijerumani kama wao CCM wanavyoshirikiana na FES shirika la Kijerumani.
Komu anasema CCM wanapokea fedha kutoka NDI kama wao CHADEMA kupitia TCD lakini mpaka leo hii CCM hawajawahi kutoa mrejesho wa fedha hizo kama wao CHADEMA wanavyofanya.
Komu ameweka wazi kuwa CHADEMA inapokea ruzuku ya shilingi milioni 230 kwa mwezi. Ameweka wazi pia mapato ya harambee zote za Arusha, Dar es salaam na michango ya Jangwani.
By
Mdutch
Nape kakurupuka kapiga simu anaambiwa ataje majina ya hao wanaotoa fedha chafu CHADEMA akabwabwaja maneno kama kawaida kwa kushindwa kuwataja.
Mwandishi kamwambia ataje kiasi cha fedha kilichoingia CHADEMA kutoka nje akabwabwaja tena maneno kwa kushindwa kukitaja kiasi chochote.
NAPE kaulizwa aseme vyanzo vya fedha vya CCM kabwabwaja maneno kwa kushindwa kuvisema vyanzo hivyo. Kashindwa kuwataja hata washirika wao wa CHINA na aliposhindiliwa kuwa na ushirikianao na FES ndio akakubali kishingo upande.
By
Mdutch
KOMU kamlima kishoka NAPE kamwambia kama yeye anadhani CHADEMA inapokea fedha chafu kutoka nje basi ni uzembe wa serikali yao dhaifu inayounda serikali yenye mamlaka na BOT inayosimamia benki zote za Tanzania ambamo CHADEMA ina akaunti zake kwa kuitaka itoe hizo taarifa.
Pia Komu kasema TRA ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya kufuatilia vyanzo vya mapato vya CHADEMA na kuvikagua. Kama CCM wanaona kweli kuna fedha chafu zinaingizwa CHADEMA basi Tanzania haina serikali
By
Mdutch
Wachangiaji wamemjia juu bwana mdogo NAPE kwa kumtaka kama moto wa CHADEMA umekuwa mkali kiasi hicho basi na wao wajaribu kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi kama wanauwezo huo ili wakijenge chama chao kinachokufa.
Kijembe kimerushwa kwa NAPE kutoka kwa mchangiaji kuwa ni kwanini CCM waliopokea fedha chafu za EPA, KAGODA na Deep Green mpaka leo wameshindwa kuwachukulia hatua. Fedha hizi zilitumika kuiingiza CCM madarakani mwaka 2005 na 2010.
Komu kaja juu tena kwa kusema kuwa CCM wana vyanzo vingine vya mapato kwa mfano umiliki wa majengo na viwanja vya michezo ambavyo wamevipora kwa kuwa vilijengwa na umma enzi za chama kimoja lakini mpaka leo hiii hawawezi kuweka wazi mapato yao ukiacha yale ya ruzuku.
By
Mdutch
Eti NAPE amedai kuwa hajaona maswali ya wachangiaji kwa kuwa ameshatoka nyumbani kwenda ofisini.
NAPE anarudi tena hewani na kudai kuwa CHADEMA ni dhaifu na haina social base kwa hiyo haihofii CHADEMA. Anajitetea kuwa yeye ni mkweli na ndio maana yuko tayari kukisema hata chama chake.
Analalamika kuwa wanaosema anaiua CCM wanamuonea kwa kuwa anajitahidi kukijenga chama chake. Anaambiwa ataje majina ya watu wanaotoa fedha chafu anacheka cheka anapata kigugumizi.
Anasema kuwa kama CHADEMA wasipochukua hatua za kuweka wazi vyanzo vya fedha zao watachukua hatua anaulizwa ni hatua gani watachukua anashindwa kusema.
Kauli yake hii ya kuonyesha kuihofia CHADEMA ni kwamba eti yeye NAPE anafanya hivi kuikosoa CHADEMA kwa kuwa ni chama kinachotaka kuiongoza nchi na CHADEMA wajisafishe ili nchi yetu isije ikatawaliwa na watu dhaifu.
By
Mdutch
"CCM ni kama panya. Mtu ukiwa hupo nyumbani panya huingia mpaka sebuleni. Ila mwenye nyumba anapokuja panya hukimbia sebuleni na kuingia uvunguni na maeneo mengine ya nyumba. CHADEMA ndio mwenye nyumba na yuko nyumbani kwa hiyo panya wamekimbia sebuleni kuelekea uvunguni.
Kwamba sebule ni majimbo yote ya mjini kama Mwanza, Arusha, Mbeya , Ubungo, Kawe, Moshi, Iringa na sasa CHADEMA inaingia mpaka uvunguni yaani majimbo ya vijijini kumsakanya panya. Operesheni sangara inayoendelea Morogoro na mikoa ya Iringa, Dodoma, na Manyanya kukijenga chama ni sawa na kumtimua panya uvunguni."
Kauli ya kumalizia ya Anthony Komu.