yasin Gahoile
Senior Member
- Apr 4, 2014
- 119
- 20
nlijua tu cdm waropokaj lazma mtukane ila ukwel unawaingia
Anasema walikutana nyumbani kwa mwenyekiti wa CHADEMA wakafanya mkutano wa kilevi. Hapo mbona anaongea kilevi? Pombe za bure Bwana!
Kibanda kawatoa nishai na mikutano yenu ya kilevi.
Kibanda kama siokosei aliwahi kuwa mhariri wa gazeti la tanzania daima, atakuwa nayo mambo mengi sana moyoni, mwacheni aendelee kufunguka tutasikia mengi
Kuwa mhariri wa Tanzania Daima hakumpi nafasi yoyote ya kujua mambo ya Chama.Sidhani kama Mhariri wa Gazeti la UHURU anajua vitu vya ndani au maamuzi ya CCM...........Hivyo statement yako haina ukweli ndani yake................
Inavyoonekana hujui kusudi na kazi za haya magazeti ya uhuru na tanzania daima haya ni magazeti ya chama kwa ajiri ya kujitangaza, wakati mwingine mhariri anahitaji kupata baraka za wamiliki kuhusu kile anachotakiwa kuandika.
Kama huamini umewahi kuona tanzani daima wanaikosoa chadema? Au uhuru wakiinanga ccm?
Tambua upo uhusiano kati ya wahariri na viongozi wa hizo taasisi.
SIjakataa kuhusu kukitangaza chama husikalakini si kujua vitu vya ndani vya chama hicho ninakukatalia.Unaweza ukafanya kazi kwenye ofisi na usijue kinachoendelea kwenye menejimenti
Usijidanganye,siyo kila asemacho Kibanda ni sahihi eti sababu tu alikuwa Mhariri wa Tanzania Daima.Wengi wa waandishi wetu wananunuliwa kirahisi sana,na wako tayari hata kuua mtu kwa kumsingizia jambo kubwa bila ukweli ndani yake,ilimradi apate chochote...........
Naona hatutofautiani sana,
nafikiri tumwache aendelee kufunguka.
Kuhusu uhalali anachozungumza itategemea ataendelea kutuambia nini ili tuweze kuunganisha doti na kuubaini ukweli
Si vizuri kumwita kanunuliwa au kukubali asilimia zote kwamba anachozungumza ni kweli
Jipe mda utabaini ukweli.