CHADEMA hawana chao utawala wa Rais Magufuli

Kwani Shigongo ni mwajiriwa wa CCM?
KWA JINSI JAMAA ANAVYOBEMBELEZA TUMWOMBEE HALAFU MAMBO BADO MAGUMU NAONA HII ITAKUWA NI MAOMBI YA SHIGONGO SIJUI AKIOMBA ATAKUWA ANASEMA NINI SIAMINI MAOMBI YAKE YANASOME KUANZIA KUSHOTO KWENDA KULIA ATAKUWA ANAMWEMBEA MH HUKU AMEKALIA CHUPA YA FANTA
 
CHADEMA kwa sasa wamepoteana.

Hakuna cha Mwenyekiti wala Katibu Mkuu.

Makamanda wao kwa sasa wamefarakana.

Wale nguli wa sheria waliokuwa wanawategemea kwa sasa hawana lolote. Ni baada ya Kisutu Kufumuliwa

Utawala wa Magufuli waliuchukulia poa sana na sasa unawatokea puani.

Mijadala mingi ya wafuasi wa CHADEMA mitandaoni ni ya malalamiko. Hata wale waliokuwa wanajenga hoja kama Malisa Godlisten, Ben Saanane na wengineo wamekata tamaa na sasa wamejiweka pembeni.

Ufipa hakukaliki tena. Kumekuwa ni hame la watoto wa jandoni.

Kelele nyingi kuhusu udikteta wa Rais Magufuli zimezimika mithili ya moto wa njiti ya kiberiti.

Asiyechaguliwa na wanachama na ambaye hakijui chama ndiye anayesimamia harakati za chama kwa sasa

Wale waliokuwa wanajiita CHADEMA Diaspora kwa sasa wameamua kususia chama. Hata yale matawi ya DMV na London kwa sasa yamebaki makumbusho tu.

Yule cha Mdomo na mtukanaji wao Mange Kimambi kwa sasa ameamua kujiweka pembeni kwa kisingizio eti bwana wake kamnyang'anya simu. Wanaona aibu

Ni mwaka mmoja tu wa Magufuli CHADEMA wapo hoi bin taaban. Wapo nyaka nyaka. Hawajiwezi.

Niwakumbushe tu kuwa siasa si mihemko. Siasa ni mikakati na mbinu za medani. CCM tuna mbinu zaidi ya 2000 za kutuwezesha kufanya siasa. Hata hii mbinu ya kuwaacha mjazane mitandaoni nayo ni mbinu. Kupitia humu kila mnachotema kinakuwa na tija kwetu.

Tukutane 2020

Lumumba kuna mambo.

Mchana unaitwa usiku. weupe unaitwa weusi, Ujinga unaitwa ujasiri, MAISHA MAGUMU YANAITWA MAISHA MEPESI.

Dhiki na shida inaitwa furaha na maendeleo. Yaani hata jina Tanzania linaitwa Mtwara
 
CHADEMA kwa sasa wamepoteana.

Hakuna cha Mwenyekiti wala Katibu Mkuu.

Makamanda wao kwa sasa wamefarakana.

Wale nguli wa sheria waliokuwa wanawategemea kwa sasa hawana lolote. Ni baada ya Kisutu Kufumuliwa

Utawala wa Magufuli waliuchukulia poa sana na sasa unawatokea puani.

Mijadala mingi ya wafuasi wa CHADEMA mitandaoni ni ya malalamiko. Hata wale waliokuwa wanajenga hoja kama Malisa Godlisten, Ben Saanane na wengineo wamekata tamaa na sasa wamejiweka pembeni.

Ufipa hakukaliki tena. Kumekuwa ni hame la watoto wa jandoni.

Kelele nyingi kuhusu udikteta wa Rais Magufuli zimezimika mithili ya moto wa njiti ya kiberiti.

Asiyechaguliwa na wanachama na ambaye hakijui chama ndiye anayesimamia harakati za chama kwa sasa

Wale waliokuwa wanajiita CHADEMA Diaspora kwa sasa wameamua kususia chama. Hata yale matawi ya DMV na London kwa sasa yamebaki makumbusho tu.

Yule cha Mdomo na mtukanaji wao Mange Kimambi kwa sasa ameamua kujiweka pembeni kwa kisingizio eti bwana wake kamnyang'anya simu. Wanaona aibu

Ni mwaka mmoja tu wa Magufuli CHADEMA wapo hoi bin taaban. Wapo nyaka nyaka. Hawajiwezi.

Niwakumbushe tu kuwa siasa si mihemko. Siasa ni mikakati na mbinu za medani. CCM tuna mbinu zaidi ya 2000 za kutuwezesha kufanya siasa. Hata hii mbinu ya kuwaacha mjazane mitandaoni nayo ni mbinu. Kupitia humu kila mnachotema kinakuwa na tija kwetu.

Tukutane 2020
Hakika wewe ni mtani wa jadi.
 
Endeleeni kuisoma namba

Ndio tumeanza hivyo. CCM wana bei za mchele wao na Chadema wana zao. CCM wana fursa peke yao za ajira na Chadema hawana.

Mwaka mmoja umekuwa wa korosho na sasa Tanzania inaitwa Mtwara basi matatizo ya Watanzania ndio yamekwisha
 
Ninachoona mimi hata ccm huku mitaani haipo. Imebaki ccm ya Juma kule magogoni tu. Hatuoni hata mikutano ya ndani ya vijiji/kata. Wote kimyaaaaaaaaaaaaaa.
 
CHADEMA kwa sasa wamepoteana.

Hakuna cha Mwenyekiti wala Katibu Mkuu.

Makamanda wao kwa sasa wamefarakana.

Wale nguli wa sheria waliokuwa wanawategemea kwa sasa hawana lolote. Ni baada ya Kisutu Kufumuliwa

Utawala wa Magufuli waliuchukulia poa sana na sasa unawatokea puani.

Mijadala mingi ya wafuasi wa CHADEMA mitandaoni ni ya malalamiko. Hata wale waliokuwa wanajenga hoja kama Malisa Godlisten, Ben Saanane na wengineo wamekata tamaa na sasa wamejiweka pembeni.

Ufipa hakukaliki tena. Kumekuwa ni hame la watoto wa jandoni.

Kelele nyingi kuhusu udikteta wa Rais Magufuli zimezimika mithili ya moto wa njiti ya kiberiti.

Asiyechaguliwa na wanachama na ambaye hakijui chama ndiye anayesimamia harakati za chama kwa sasa

Wale waliokuwa wanajiita CHADEMA Diaspora kwa sasa wameamua kususia chama. Hata yale matawi ya DMV na London kwa sasa yamebaki makumbusho tu.

Yule cha Mdomo na mtukanaji wao Mange Kimambi kwa sasa ameamua kujiweka pembeni kwa kisingizio eti bwana wake kamnyang'anya simu. Wanaona aibu

Ni mwaka mmoja tu wa Magufuli CHADEMA wapo hoi bin taaban. Wapo nyaka nyaka. Hawajiwezi.

Niwakumbushe tu kuwa siasa si mihemko. Siasa ni mikakati na mbinu za medani. CCM tuna mbinu zaidi ya 2000 za kutuwezesha kufanya siasa. Hata hii mbinu ya kuwaacha mjazane mitandaoni nayo ni mbinu. Kupitia humu kila mnachotema kinakuwa na tija kwetu.

Tukutane 2020
Kalipe madeni ya watu kwanza kabla ya kuiongelea Chadema.
Kwa nini huwashauri wamlipe Shigongo? Jamani mali zake zitapigwa mnada kisa aliwakopesha. Halafu hii ni tabia mbaya kula rambi rambi. Mtapata laana bure jamani. Nasikia uchumi umekua na makusanyo yako juu uku mabenki yakifunga biashara na mohoteli kupigwa mnada. Mpaka shule nazo zinapigwa mnada, vipi kulikoni au utasema ni kwa sababu ya Chadema? Kama ni Chadema basi wabaya sana!! Yaani wamepoteana mpaka Benki zinafungwa, wanafunzi wakosa mikopo wakati walisema elimu bure na hakuna mwanafunzi kukosa mikopo? Kupoteana kwa Chadema kumeiyumbisha serikali maana kutumbuana kumezidi na nasikia Board ya TRA imetumbuliwa kwa sababu wamekusanya mapato mengi. Lizaboni huoni kweli kupoteana kwa Chadema kumeifanya nchi hiyumbe
Chadema chadema. Karekebishe mambo yako uko Fisiem ndo uje Chadema
 
Yaani mwaka mmoja tu CHADEMA wapo nyang'anyang'a. Hiyo miaka mingine ndo watazidi kupotea. Ninachokiona hapa ni siasa za chadema Kufanywa na akina Bashe

Wewe Lizabon

Roho yako inakereketwa na mfupa uliomshinda fisi, ukweli unaujuwa namna mtu wenu anavyoiangusha taasisi kwa kasi. Maslahi binafsi unayoyapata kwa kazi yako hapa JF yanakufanya uwe msaliti kwa Watanzania. Ukweli wa dhati unaujuwa nini kinaendelea hapa Tanzania.

Hebu twambie hata Wanafunzi wa Vyuo vikuu nao wanaisoma namba na kwamba wote hao ni CHADEMA ?
 
Kwani na wewe unakubaliana na hoja ya mtu aliyepata asilimia moja ya kura kuibuka mshindi akimshinda yule wa asilimia 84?

Maajabu ya Lumumba yanaendelea.

Kwamba asilimia 1 ishinde 84%. Haya ndio mawazo yao yalivyo. Si mlituaminisha kuwa JPM anaongoza. Kama mlifikiri bangi kuwa ni ugoro mlishapwelewa.

Namba hazisemi uongo. Jamaa anashuka kwa kasi. Tukubaliane wote kuwa kuna baadhi ya mambo alianza vizuri lakini kadiri muda ulivyosonga aliharibu ndani ya muda mfupi.

By the way ajira mpya lini au zoezi la uhakiki linaendelea? na vipi kuhusu kuhamia dodoma mipange ikoje?

Utwambie na lini changamoto ya kupungua mizigo bandarini kuna mpango upi mkakati wa muda mfupi kuimarisha hali?

Twahitaji pia neno "Kutengua' litaacha kutumika lini badala ya kuongeza uweledi wa "Kuteuwa"

Ni hayo hiyo habari ya CHADEMA ni ya kutafuta fungu la leo tu. (Shikamoo Lizabon kwa ubunifu wako)
 
mkuu lizabon. Sina shaka na uwezo wako wa kufikiri kama ni mdogo kiasi hicho cha kuvua akili zako za kupambanua mambo kwa kina na kwa ujenzi wa Taifa letu Pendwa Tanzania.

Usije ukajidanganya na kushabikia mambo kama haya unayo ya shabikia tena kwa ushabiki mbaya kabisa.

Taifa la tanzania kamwe halito jengwa kwa mtazamo wa kushabikia kukomoana.

Taifa litajengwa kwa undugu na mshikamano. Hapa naomba tuweke siasa za vyama pembeni na kuliweka Taifa Mbele.

Ushabiki wa kivyama hautusaidii sisi kama Watanzania.

Kitakacho tusaidia ni undugu na kuheshimiana na kuwajibika kama wanasiasa na wananchi wa Tanzania katika kuijenga nchi yetu Nzuri kabisa Tanzania.

Ni wito wangu kwa wakereketwa, wenye fikra kama zako tena wa Vyama vyote.

Kuanza kuifikiria nchi kwanza na kuishi kwa upendo na kuheshimiana.

Tukijenga Upendo na kuheshimiana Hakika tutakaa Pamoja na kuijenga Nchi Pamoja tena kwa Upendo na Uzalendo Mkubwa.

Mungu Ibarika Tanzania.
 
Mkuu, maana ya jukwaa la siasa ni kufanya siasa. Bila vyama vya siasa hakuna siasa. Mtazamo wangu dhidi ya vyama vya upinzani hautabadilika kamwe. Ni watu walioshindwa na kufilisika kisiasa. Ni genge la walalamikaji na wanung'unikaji
 
Umesema kweli hawanachao kwani hata wakati wanagawana zile bilioni 2 chadema hawakuwepo na hawakupewa.
Wakati wanafunzi wananyimwa mikopo chadema hawakushirikishwa.
Wakati mnakula hela za waathirika wa tetemeko chadema haikuwepo.
Wakati mnamdhurumu shigongo chadema hawakuwepo.
Wakati mnaifilisi nchi chadema hapo.
Hivyo ni kweli chadema haina chao kwa magufuri, yote anapanga yeye na chama chake cha ccm
 
Mkuu, maana ya jukwaa la siasa ni kufanya siasa. Bila vyama vya siasa hakuna siasa. Mtazamo wangu dhidi ya vyama vya upinzani hautabadilika kamwe. Ni watu walioshindwa na kufilisika kisiasa. Ni genge la walalamikaji na wanung'unikaji

Utatumika sana na utabaki benchi siku zote.
 
Huu ni wakati wa kuchapa kazi. Si porojo za kisiasa. Ndo maana hata wazee wetu Mangula na Kinana wapo benchi. Tunatekeleza kwanza ilani yetu. Mtusamehe tu kwani kwa hii miaka iliyobaki hatutakuwa na mzaha
Mbona wewe ndio unafanya porojo za siasa kila kukicha .......bandiko si umeanzisha wewe ..?..Mbona sikuelewi mkuu .....
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Mbona wewe ndio unafanya porojo za siasa kila kukicha .......bandiko si umeanzisha wewe ..?..Mbona sikuelewi mkuu .....

Ana mfadhaiko wa kutoswa katika teuzi mbali mbali yupo yupo tu hajitambui ndiyo maana anajichanganya sana kwenye mabandiko yake.
 
CHADEMA kwa sasa wamepoteana.

Hakuna cha Mwenyekiti wala Katibu Mkuu.

Makamanda wao kwa sasa wamefarakana.

Wale nguli wa sheria waliokuwa wanawategemea kwa sasa hawana lolote. Ni baada ya Kisutu Kufumuliwa

Utawala wa Magufuli waliuchukulia poa sana na sasa unawatokea puani.

Mijadala mingi ya wafuasi wa CHADEMA mitandaoni ni ya malalamiko. Hata wale waliokuwa wanajenga hoja kama Malisa Godlisten, Ben Saanane na wengineo wamekata tamaa na sasa wamejiweka pembeni.

Ufipa hakukaliki tena. Kumekuwa ni hame la watoto wa jandoni.

Kelele nyingi kuhusu udikteta wa Rais Magufuli zimezimika mithili ya moto wa njiti ya kiberiti.

Asiyechaguliwa na wanachama na ambaye hakijui chama ndiye anayesimamia harakati za chama kwa sasa

Wale waliokuwa wanajiita CHADEMA Diaspora kwa sasa wameamua kususia chama. Hata yale matawi ya DMV na London kwa sasa yamebaki makumbusho tu.

Yule cha Mdomo na mtukanaji wao Mange Kimambi kwa sasa ameamua kujiweka pembeni kwa kisingizio eti bwana wake kamnyang'anya simu. Wanaona aibu

Ni mwaka mmoja tu wa Magufuli CHADEMA wapo hoi bin taaban. Wapo nyaka nyaka. Hawajiwezi.

Niwakumbushe tu kuwa siasa si mihemko. Siasa ni mikakati na mbinu za medani. CCM tuna mbinu zaidi ya 2000 za kutuwezesha kufanya siasa. Hata hii mbinu ya kuwaacha mjazane mitandaoni nayo ni mbinu. Kupitia humu kila mnachotema kinakuwa na tija kwetu.

Tukutane 2020
Nimependa hapo pa kisutu kufumuliwa...ha ha haaa ngome kwishney daah..
 
Back
Top Bottom