CHADEMA hawako makini kabisa

CHADEMA hawako makini kabisa

hizi ni hujuma za ccm

NOOOOOO huu ni ujin.ga kabisa na upu.uzi wa hawa viongozi wa CHADEMA.
Yaani viongozi walio wengi huku ngazi za chini wapo wapo tu kama maz.uzu.

INAKERA SANA...
 
hivi makoa makuu wanafanya kazi gani?ok tuna matawi nchi nzima ni kazi ya mako makuu kujua wana vitu vya muhimu kama mihuri na vitu vya muhimu,naomba mtu awajibike hapo
 
bwana mdiliko nakubaliana na hoja yako lakini angalia hata wewe mwenyewe haupo makini pia. Inashauriwa kabla hujatuma bandiko ufanye kwanza editting kuona makosa na ommissions na sio kila jambo unaweza ku abriviate kama ulivyoandika knda kwa maana ya kanda. Makosa kama hayo ndiyo yanayoigharimu chadema leo kwa kufikiri wanaweza kupiga kwenye fomu ya mgombea wao mhuri unaosomeka cdn, cdm, ukawa au cuf na ikakubaliwa na tume ya uchaguzi. Mara nyingi nimeandika kuipigia kelele chadema kuhusu umakini wao na uzembe mdogo mdogo unaokiathiri chama hata kama kinakubalika. Hawajali semina kwa viongozi wao wa ngazi za chini. Sasa kweli mgombea wa chadema fomu ipigwe mhuri wa cuf ina maana hilo tawi halina mhuri? Hivi chadema makao makuu hawawezi kutengeneza mihuri yenye nembo ya chama na kuacha sehemu ya kujaza tawi, kijiji au kitongoji ambayo inaweza kujazwa na kalamu na m/kiti wa eneo linalohusika kuliko kumwachia kila mmoja kujitengenezea anavyoona? Hivi wenyeviti na makatibu wa wilaya wa chadema hawakagui matawi na kuona mihuri waliyo nayo? Mapingamizi yanayohusu wagombea wa chadema nchi nzima ni maelfu na msitegemee huruma yoyote katika rufani ni kwamba jihesabuni wameondolewa. Yote hayo ni kukosa umakini kwa chadema mbona hatuyasikii kwenye vyama vingine vya upinzani? Huu ni uchaguzi wa ngazi ya chini sana lakini muhimu je uchaguzi mkuu tutegemee nini?.

kwa upu.uzi wa hawa viongozi wa chadema ujinga huu huu utajirudia mwakani na wagombea wetu utasikia wameenguliwa tena. Hovyo kabisa hawa viongozi, wetu wanakera sana.
 
Hilo ni KOSA kubwa lisilokubalika katika utetezi wowote ule MUHURI WA CHAMA (party property) kuandikwa CDM, badala ya CHADEMA!

Tusitetee uzembe kwa kuwa CCM nao wanafanya uzembe.
 
hivi makoa makuu wanafanya kazi gani?ok tuna matawi nchi nzima ni kazi ya mako makuu kujua wana vitu vya muhimu kama mihuri na vitu vya muhimu,naomba mtu awajibike hapo
Hizi lugha za kipole katika misimamo imara ndo zinafanya tuonekane mapoyoyo! Utaombaje mtu awajibike? Sema NATAKA mtu awajibike haraka sana!
 
Back
Top Bottom