Uchaguzi Serikali za Mitaa: Ushauri kwa Viongozi wa CHADEMA ngazi ya Kata na Mitaa

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,041
1,160
UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MCHANGANUO WA RATIBA NA USHAURI KWA VIONGOZI WATENDAJI Wa KATA-CHADEMA.

A: SEHEMU YA KWANZA
RATIBA NA UANDIKISHWAJI WA WAPIGA KURA

1. Kuanzia tar 23/11/2014 litaanza zoezi la uandikishaji na uhakiki wa orodha ya majina ya wapiga kura mpaka Tar 29/11/2014.

2. Tarehe 04/12 hadi Tarehe 08/12/2014 ni siku za kutoa na kusikiliza pingamizi.

3. Tusisahau kuweka mawakala wa kusimamia hili zoezi la kuandikisha wapiga kura ili ccm wasiweze kuandikisha hata wasioishi kwenye mtaa/kijiji au kitongoji husika.

4. Bila kusahau kila mtaa/kata iwe na mhuri wake please wasitutafutie sababu ya pingamizi. Hii ni muhimu sana.

5. Ni siku saba tu za kujiandikisha.

6. Vongozi wa wilaya, kata, vijiji na vitongoji wa Chadema ni muhimu sana kuhakikisha mnahamasisha wananchi wanajiandikisha kuanzia Tarehe 23/11 wasisubili kujiandikisha siku za mwisho kuondoa mikanganyiko inayoweza kusababisha wapiga kura wa Chadema kushindwa kujiandikisha.

7. Ni muhimu pia kulinda usalama wa wagombea wetu, na kuzuia hujuma za kuwafungulia kesi zinazoweza kusababisha wapelekwe polisi kutupotezea muda wa kupiga kampeini.

B: SEHEMU YA PILI

Ndugu viongozi wetu wa Chadema NI MUHIMU SANA HAYA KUYAWEKA TAYARI WAKATI WA MAANDALIZI

1. Orodhesha wagombea wote wa serikali za mitaa katika Jimbo lako.

2. Hakikisha kuwa viongozi wa chama ngazi ya kata au mtaa wametambulishwa ofisi za serikali ngazi husika.

3. Hakikisha kila mtaa/kijiji/kitongoji wameandaa mawakala wa kisimamia zoezi la uandikishaji kuanzia tar23/11- 29/11.

4. Hakikisha kila mgombea ana kanuni ya uchaguzi wa serikali za mitaa na anazielewa.
Au utaratibu wa kuwaelewesha kwa pamoja ufanyike.

5. Hakikisha form za uchaguzi zimefika kila mtaa/kijiji na wagombea ngazi zote wazijaze inavyotakiwa.

6. Hakikisha kila kata iwe na mhuri wake kwa ajili ya kuthibitisha wagombea wetu.

C: KUDHIBITI MBINU ZA WIZI ZA CCM.

1. CCM wanaandikisha wapiga kura zaidi ya mara moja.

KUTATUA: Mawakala wa cdm wawe wenyeji, waaminifu na waadifu na wahakikishe hilo halifanyiki hata kidogo.

2. Ccm kupitia Halmashauri (wasimamizi wa uchaguzi) wanaandaa karatasi za kupigia kura nyingi zaidi kuliko idadi inavyotakiwa na kuwapa wanaccm walio kwenye vituo vya kupigia kura na huzitumia kupiga kura nyingi zaidi fake.

KUTATUA: Mawakala na viongozi wetu wa Chadema kote nchini ni muhimu sana kuelewa hujuma hizi za ccm na wajipange vizuri kuzuia kwa kufanya yafuatayo:

i) kuhakikisha idadi ya karatasi za wapiga kura zinazondaliwa kutumika hazizidi idadi ya wapiga kura walioandikishwa.

ii) mawakala wawe makini sana kupita kawaida kuanzia mwanzo wa zoezi la kupiga kura hadi mgombea wetu atakapotangazwa mshindi.

iii) mawaka wote wakaguliwe mifukoni mwao kuhakikisha hakuna wakala wa ccm aliye na makaratasi ya kupigia kura ya ziada.

iv) wakala yeyote au msimamizi akienda musarani akirudi akaguliwe upya kabla hafanya chochote kituoni kujirisha kuwa hana chochote mfukoni.

V) Atakayekataa kukaguliwa huyo makamanda wale naye sahani moja na kuhakikisha anakaguliwa.

vi) vitu kama kofia, mikoba na nguo zilizokunjwakunjwa au vitu vingine kama hivyo vizuiliwe kabisa kuletwa kituoni. Yaani wapiga kura wadhibitiwe wasithubutu kutumia ujanja wa yaliyotajwa hapo juu kuingiza kura fake kwenye kituo cha kupigia kura.

vii) Wakati msimamizi anataka kufungua masanduku ya kura zilizopigwa mawakala wahakikishe eneo husika hakuna karatasi yoyote na msimamizi awe amefanyiwa uchunguzi kuwa hafanyi udanganyifu wowote wakati wa kufungua na kumwaga kura chini tayari kwa kuhesabu. Kuna wizi unaweza kufanyika hapo na wazimizi ambao ni mawakala No.1 wa ccm ambao huisaidia ccm kuiba kura.

viii) Tusiamini mtu yeyote asiye mwanachama mwaminifu na wa uhakika kuwa analinda Chadema kwa akili na nguvu zake zote.

ix) wakati wa kuandikisha wawepo na no ya idadi ya waliondikishwa rekodi ichukuliwe kila siku ili kuzuia uchakachuaji kufanyika usiku.

Na kila siku kabla ya zoezi la kuandikisha wapiga kura kuendelea, ni lazima mawakala wajiridhishe kuwa idadi iko sahihi kwa wawakirishi wa vyama vyote. Iwapo kuna uchakachuaji, zoezi la kuandikisha lisiendelee kabla mwandikaji hajaondoa majina yaliyotiliwa shaka.

x). wakati wa kupiga kura, lazima idadi ya wapigakura ijulikane kabla ya kuanza kupiga.

xi) wakati huu RB wetu wasiowajua tuwachomeke kwenye vikao vya ccm walete mipango yote wanayoifanya ccm.

xii) Chadema tuhakikishe mamluki yeyote hapati nafasi hata kidogo kujua ni nini Chadema tunapanga na mbinu zetu ni zipi.

UTARATIBU WA KUKAGUA
i) Mhusika/anayetakiwa kukaguliwa atoe mifuko nje yeye mwenyewe kama ni mwanaume mwanaume mwenzie amkague vizuri kwa kwa utaratibu huo kutumia busara, umakini na bila shuruti iwapo mkaguliwa ni mstaarabu.

ii) Iwapo ni mwanamke akaguliwe na mwanamke mwenzake kwa utaratibu sawa na wanaume kwa uangalizi wa kamanda aliyeandaliwa kuchunguza uharamia wa ccm ktk kituo cha kupigia kura.

Kwa tafsiri hiyo, ni muhimu makamanda kuwa karibu na kituo cha kupigia kura ili waweze kukabiriana na majukumu hayo au vingivevyo itakavyotakiwa na mratibu wa uchaguzi wa CHADEMA wa kitongoji husika.

KUMBUKA
a). Mawakala wa Chadema kuwa makini na matumizi ya simu ya mawakala wa ccm.

b). Viongozi wasiandae mawakala dhaifu wasioweza kujisimamia kwa nguvu na busara zote kuzuia uharamia wa ccm.

c) Uzembe wowote usifanyike kuanzia asubuhi hadi jioni wagombea wa Chadema watakapotangazwa washindi.

d) Dharura yoyote kwa mawakala wa Chadema kutoka kwenye vituo vya kupigia kura isiruhusiwe kwani siku ya kupiga kura ni siku ya kupambana ili kuvuna mavuno kazi ya makamanda wa chama waliyoifanya kwa kipindi cha miaka 5.

Hili lipewe uzito mkubwa sana na waratibu wa uchaguzi wa Chadema ngazi zote bila mzaha wowote.

D. IBARA MUHIMU ZA SHERIA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
KWA KUANZIA

1.Ibara ya 20 (5), (6), na (7), msimamizi wa uchaguzi kuhitaji kitambulisho cha mpiga kura.

2. Ibara 19
Tahadhari inatakiwa kuchukuliwa kuzuia shari isiyo ya lazima.

Ccm wakipata kosa dogo watalitumia kuengua wagombea wa Chadema/ Ukawa.

3. Ibara ya 20 (11) namna walemavu na wasiojua kusoma watakavyopiga kura.

Ccm wakipata nafasi hii wanaitumia kuhujumu. Mawakala wanatakiwa kudhibiti kila kura isihujumiwe.

4. Ibara ya 22(2)
Mambo ambayo msimamizi wa uchaguzi anayotakiwa kufanya kabla ya kuchaguzi.
i). Kuhakiki idadi ya wapiga kura.
ii) atahesabu idadi ya karatasi za kupigia kura ambazo hazikutumika na kuziweka ktk bahasha maalumu.

iii) atakagua lakiri na kuona kama imefungwa au haijafunguliwa.

Mambo hayo yakibezwa/kuzembea kuwa makini nayo na mawakala wa Chadema itapelekea kuhujumiwa.

5. Ibara ya 26.
Matendo yasiyobatilisha matokeo. Kifungu hiki kipo kwa masilahi ya ccm.

Kisomwe na kueleweka ili tujipange kuzuia makosa.

6. Ibara ya 33:- Ni muhimu kuitumia vizuri nafasi ya watazamaji wa ndani kulinda kura za Chadema.

7. Ibara ya 34(1). Makosa ya uchaguzi.

Tutaendelea kupambana na CCM kwa kila hali.
 
naomba kuuliza wale hawakupiga kura 2010 kwa sababu mbalimbali labda umri au kutojiandikisha kwenye daftrari je itakuwaje,wataandikisha wapiga kura wapya au ni walewale wa zamani kama kawaida yao?
 
naomba kuuliza wale hawakupiga kura 2010 kwa sababu mbalimbali labda umri au kutojiandikisha kwenye daftrari je itakuwaje,wataandikisha wapiga kura wapya au ni walewale wa zamani kama kawaida yao?

Wataandikishwa kwa upya mkuu.... Cha msingi wahamasishe wote wenye sifa ya kupiga kura kujiandikisha
 
naomba kuuliza wale hawakupiga kura 2010 kwa sababu mbalimbali labda umri au kutojiandikisha kwenye daftrari je itakuwaje,wataandikisha wapiga kura wapya au ni walewale wa zamani kama kawaida yao?

A: SEHEMU YA KWANZA
RATIBA NA UANDIKISHWAJI WA WAPIGA KURA

1. Kuanzia tar 23/11/2014 litaanza zoezi la uandikishaji na uhakiki wa orodha ya majina ya wapiga kura mpaka Tar 29/11/2014.

2. Tarehe 04/12 hadi Tarehe 08/12/2014 ni siku za kutoa na kusikiliza pingamizi.

3. Tusisahau kuweka mawakala wa kusimamia hili zoezi la kuandikisha wapiga kura ili ccm wasiweze kuandikisha hata wasioishi kwenye mtaa/kijiji au kitongoji husika.

4. Bila kusahau kila mtaa/kata iwe na mhuri wake please wasitutafutie sababu ya pingamizi. Hii ni muhimu sana.

5. Ni siku saba tu za kujiandikisha.


6. Vongozi wa wilaya, kata, vijiji na vitongoji wa Chadema ni muhimu sana kuhakikisha mnahamasisha wananchi wanajiandikisha kuanzia Tarehe 23/11 wasisubili kujiandikisha siku za mwisho kuondoa mikanganyiko inayoweza kusababisha wapiga kura wa Chadema kushindwa kujiandikisha.

7. Ni muhimu pia kulinda usalama wa wagombea wetu, na kuzuia hujuma za kuwafungulia kesi zinazoweza kusababisha wapelekwe polisi kutupotezea muda wa kupiga kampeini.

Tutaendelea kupambana na CCM kwa kila hali.


Hivi umesoma kweli au?
 
kura za wizi zinapigwa asubuhi wazee na mashati yao ya mikono mirefu na wamama wamejitanda kanga/mishundi mzigo ndio unaenda kushushwa,
 
Kamanda huu ni ujumbe mzuri kwa manufaa ya chama chetu CDM mimi nashauri jitahidi ufike kwa majatibu wa mitaa, kata, majimbo ili kufanyiwa kazi haraka kwani siku hazigandi tena zifike kwa njia ya barua(karatasi) ili wazisome na kuzisambaza kwa wanachama lkn kwa njia hii ya mitandao ujumbe unaweza ufike lkn sio kila mtu ana cm ya uwezo huu.
 
Mkuu GJHariohay nitafurahi ukinipa utaratibu wa wale wanaoenda kujiandikisha kwa mara ya kwanza. Vitu gani wanatakiwa kuwa navyo. Je wanahitaji barua za mwenyekiti wa nyumba 10, ili kumtambulisha kuwa yeye ni mkazi wa mtaa huo. Hiki kwa wengi ndo huwa kikwazo maana wajumbe wengi huwa ni wa CCM. Vipi kwa wale wageni kwenye mitaa yao. Sehemu hasa ya kuanzia ni wapi ili kuepuka usumbufu wa nenda rudi. Nataka niwastue vijana wangu mtaani kwa ajili ya zoezi hili mapema. Nijulishe tafadhali nikishawakusanya break ya kwanza ni wapi na ni nini wajiandae navyo kwa ajili ya kujiandikisha.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom