CHADEMA hawako makini kabisa

mchambuzixx

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
1,292
1,225
Jamani kuna kitu kimenisikitisha na kimenihuzunisha, hivi hiki chama hakikuwa na uniformity ya mihuri haiwezekani kwa chama makini kama hiki chenye viongozi wa kanda kifanye madudu kama haya.

Kwa mfano Meatu mhuri badala ya kuandikwa CHADEMA unaandika"CDN" pamoja na kujua hila zote za CCM na kujua mapema mitego kama hiyo lkn yamefanyika madudu kama hayo.

Meatu wagombea wote wamepigwa chini kwa kosa hilo inasikitisha kwa kweli kule Same ndio hivyo tena.

Unajiuliza iweje Shinyanga Mjini wajaze vizuri Meatu waboronge? Ina maana kila mtu alikuwa anajijazia anavyojua yeye?

Sijajua hatua gani zimechukuliwa kuwapatia haki wananchi lakini huu ni uzembe mkubwa umefanyika. Mbona CUF hawakufanya madudu haya?

Labda mwenye jibu atatuambia.
 
Gor

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,793
1,195
Watz wengi majizi tu....mihuri utaandikaje cdm?
 
chipolopolo 2

JF-Expert Member
Nov 10, 2014
3,274
2,000
Inamaana hao hao viongozi wa chadema hawajaliona hilo tatizo. Kama ni kweli bas hao viongozi wachukuliwe hatua
 
BigMan

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,096
1,195
Jamani kuna kitu kimenisikitisha na kimenihuzunisha, hivi hiki chama hakikuwa na uniformity ya mihuri haiwezekani kwa chama makini kama hiki chenye viongozi wa kanda kifanye madudu kama haya.

Kwa mfano Meatu mhuri badala ya kuandikwa CHADEMA unaandika"CDN" pamoja na kujua hila zote za CCM na kujua mapema mitego kama hiyo lkn yamefanyika madudu kama hayo.

Meatu wagombea wote wamepigwa chini kwa kosa hilo inasikitisha kwa kweli kule Same ndio hivyo tena.

Unajiuliza iweje Shinyanga Mjini wajaze vizuri Meatu waboronge? Ina maana kila mtu alikuwa anajijazia anavyojua yeye?

Sijajua hatua gani zimechukuliwa kuwapatia haki wananchi lakini huu ni uzembe mkubwa umefanyika. Mbona CUF hawakufanya madudu haya?

Labda mwenye jibu atatuambia.
hilo afadhali katika sehemu nyingine jina la chama limeandikwa vuri lakini kosa katika muhuri huo huo likaongezwa jina la Katibu wa chama ngazi husika lakini katika maeneo mengine pia jina la mgombea na chama ni chadema lakini mhuri umegongwa wa CUF
 
Njota14

Member
Dec 4, 2014
9
0

Kweli cdm hawako makini, haiwezekani chama kinachosema kua mwakani kinachukua nchi halafu kinaachia wagombea wake wanaenguliwa kizembe, sehemu nyingine hawajasimamisha wagombea
 
afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
hilo afadhali katika sehemu nyingine jina la chama limeandikwa vuri lakini kosa katika muhuri huo huo likaongezwa jina la Katibu wa chama ngazi husika lakini katika maeneo mengine pia jina la mgombea na chama ni chadema lakini mhuri umegongwa wa CUF
Njama za viongozi asikudanye mtu kwamba watu wamekosa uelewa kiasi hicho.
 
laiza

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,065
1,195
wenzako wanakomaa dar ili waingie ikulu magogoni wewe unawaletea habari za meatu...kuna ikulu huko?
Jamani kuna kitu kimenisikitisha na kimenihuzunisha, hivi hiki chama hakikuwa na uniformity ya mihuri haiwezekani kwa chama makini kama hiki chenye viongozi wa kanda kifanye madudu kama haya.

Kwa mfano Meatu mhuri badala ya kuandikwa CHADEMA unaandika"CDN" pamoja na kujua hila zote za CCM na kujua mapema mitego kama hiyo lkn yamefanyika madudu kama hayo.

Meatu wagombea wote wamepigwa chini kwa kosa hilo inasikitisha kwa kweli kule Same ndio hivyo tena.

Unajiuliza iweje Shinyanga Mjini wajaze vizuri Meatu waboronge? Ina maana kila mtu alikuwa anajijazia anavyojua yeye?

Sijajua hatua gani zimechukuliwa kuwapatia haki wananchi lakini huu ni uzembe mkubwa umefanyika. Mbona CUF hawakufanya madudu haya?

Labda mwenye jibu atatuambia.
 
Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
4,692
2,000
kuna mwana jf alitaadharisha wiki tatu zilizopita kua ccm wameitega cdm kwenye mihuri nao cha ajabu wamejaa 18 wenyewe wanaham
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,319
2,000
Tumekwisha mjulisha na kumwagiza waziri mkuu awarejeshe wagombea wote wa cdm walioenguliwa kwa sababu za kitoto za mihuri .
 
magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,125
2,000
Kusema kweli hakuna uchaguzi mgumu km wa huu wa serikali za mitaa hata kwa ccm yenyewe! Wagombea wenyewe huwa ni wakuokoteza,na wanaokubali unakuta hawajui chochote kuhusu siasa. Hali km hii ni rahisi kulaumu km hujafanya siasa za huko chini. Hata ccm wanafanya makosa mengi sana km hayo,lkn wao wanapewa taarifa na wasimamizi kabla hawajawekewa pingamizi na wanarekebisha mambo. Kumbuka watendaji wote wa vijiji na kata huwa wanaitwa kwenye vikao vya ccm na kupewa maelekezo. Chadema hata hivyo wanajitahidi sana!
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,030
2,000
Watz wengi majizi tu....mihuri utaandikaje cdm?
Labda mimi niseme KUKOSA umakini kwenye maandishi ni tatizo kubwa sana sana Tanzania. Watu ni wavivu na hawajali wala kijishughulisha kabisa kuhakikisha maandishi yako kama yalivyotakiwa kuwa. Majina ya sehemu, watu, vitu nk watu wanaandika wanavyotaka. Na watu wa aina hiyo ukiwakosoa wanakuwa wakali sana na wanakuwa rahisi kujibu ''mradi umeelewa''. Kwa upande mwingine CCM wanatumia loopholes kama hizi kuwaondoa wagombea wa upinzania kwasababu wanajua kabisa CCM hawakubaliki kabisa. Na mwisho labda niseme sheria za uchaguzi za Tanzania ni sheria mbovu sana zinazotoa mianya ya kuwaondolea wapiga kura haki ya kuchagua mgombea wanayemtaka. Vilevile hizi sheria zinafanya hujuma iwe rahisi kutenda hasa kwa kutumia fedha. Kwanini isiwe huyo msimamizi awe na jukumu la kuhakikisha fomu ipo kamili na sahihi kabla ya kupokea?
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,030
2,000
Kusema kweli hakuna uchaguzi mgumu km wa huu wa serikali za mitaa hata kwa ccm yenyewe! Wagombea wenyewe huwa ni wakuokoteza,na wanaokubali unakuta hawajui chochote kuhusu siasa. Hali km hii ni rahisi kulaumu km hujafanya siasa za huko chini. Hata ccm wanafanya makosa mengi sana km hayo,lkn wao wanapewa taarifa na wasimamizi kabla hawajawekewa pingamizi na wanarekebisha mambo. Kumbuka watendaji wote wa vijiji na kata huwa wanaitwa kwenye vikao vya ccm na kupewa maelekezo. Chadema hata hivyo wanajitahidi sana!
Mkuu sidhani kama wanajitahidi sana kama unavyosema. Suala kama hili la muhuri mbona ni rahisi sana! Makao makuu kwanini wasiwe na jukumu la kutengeneza mihuri na kuisambaza kwa kila wilaya ili kuwe na unique ya aina fulani? Kwanini wasiandae check list ya vitu vyote vinavyotakiwa kutimizwa halafu wazimbaze kila kanda na knda ipeleke wilayani kwa mfano?
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
Jamani kuna kitu kimenisikitisha na kimenihuzunisha, hivi hiki chama hakikuwa na uniformity ya mihuri haiwezekani kwa chama makini kama hiki chenye viongozi wa kanda kifanye madudu kama haya.

Kwa mfano Meatu mhuri badala ya kuandikwa CHADEMA unaandika"CDN" pamoja na kujua hila zote za CCM na kujua mapema mitego kama hiyo lkn yamefanyika madudu kama hayo.

Meatu wagombea wote wamepigwa chini kwa kosa hilo inasikitisha kwa kweli kule Same ndio hivyo tena.

Unajiuliza iweje Shinyanga Mjini wajaze vizuri Meatu waboronge? Ina maana kila mtu alikuwa anajijazia anavyojua yeye?

Sijajua hatua gani zimechukuliwa kuwapatia haki wananchi lakini huu ni uzembe mkubwa umefanyika. Mbona CUF hawakufanya madudu haya?

Labda mwenye jibu atatuambia.
Mimi sijaona sheria inayoongoza uchaguzi huu je ili Mgombea awe sio mgombea halali ni makosa yepi yanayomuondolea sifa naomba utuwekee hapa ili tujue na pia ni vema tukapenda kujua vyama vya siasa hususani vya upinzani ni lini vilipatiwa sheria hizi za huu uchaguzi?
 
majebere

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
4,736
2,000
Kuna walio beba hela kwenye mifuko ya rambo kutoka stanbik na mpaka sasa hawajulikani.wakwenu wapo pia.
 
geraldkowero1

JF-Expert Member
Jul 5, 2014
1,839
1,500
Mkuu sidhani kama wanajitahidi sana kama unavyosema. Suala kama hili la muhuri mbona ni rahisi sana! Makao makuu kwanini wasiwe na jukumu la kutengeneza mihuri na kuisambaza kwa kila wilaya ili kuwe na unique ya aina fulani? Kwanini wasiandae check list ya vitu vyote vinavyotakiwa kutimizwa halafu wazimbaze kila kanda na knda ipeleke wilayani kwa mfano?
Bwana Mdiliko nakubaliana na hoja yako lakini angalia hata wewe mwenyewe haupo makini pia. Inashauriwa kabla hujatuma bandiko ufanye kwanza editting kuona makosa na ommissions na sio kila jambo unaweza ku abriviate kama ulivyoandika knda kwa maana ya kanda. Makosa kama hayo ndiyo yanayoigharimu chadema leo kwa kufikiri wanaweza kupiga kwenye fomu ya mgombea wao mhuri unaosomeka cdn, cdm, ukawa au cuf na ikakubaliwa na tume ya uchaguzi. Mara nyingi nimeandika kuipigia kelele chadema kuhusu umakini wao na uzembe mdogo mdogo unaokiathiri chama hata kama kinakubalika. Hawajali semina kwa viongozi wao wa ngazi za chini. Sasa kweli mgombea wa chadema fomu ipigwe mhuri wa cuf ina maana hilo tawi halina mhuri? Hivi chadema makao makuu hawawezi kutengeneza mihuri yenye nembo ya chama na kuacha sehemu ya kujaza tawi, kijiji au kitongoji ambayo inaweza kujazwa na kalamu na m/kiti wa eneo linalohusika kuliko kumwachia kila mmoja kujitengenezea anavyoona? Hivi wenyeviti na makatibu wa wilaya wa chadema hawakagui matawi na kuona mihuri waliyo nayo? Mapingamizi yanayohusu wagombea wa chadema nchi nzima ni maelfu na msitegemee huruma yoyote katika rufani ni kwamba jihesabuni wameondolewa. Yote hayo ni kukosa umakini kwa chadema mbona hatuyasikii kwenye vyama vingine vya upinzani? Huu ni uchaguzi wa ngazi ya chini sana lakini muhimu je uchaguzi mkuu tutegemee nini?.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom