bullet proof
Member
- Sep 19, 2012
- 57
- 35
CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani na viongozi wake wanajitahidi kusana kuzunguka nchi nzima kufanya harakati mbalimbali za kisiasa kama chama cha upinzani kwa maana ya kujaribu kukosoa na kukejeli hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kupitia chama tawala cha mapinduzi (CCM). Harakati hizi zimeendana na maandamano makubwa ambayo mara kadhaa yamegharimu maisha ya wananchi (vifo).
CHADEMA hufanya harakati hizi zote wakijaribu kuwaaminisha watanzania kuwa wao (CHADEMA) ndio mwarobaini wa matatizo ya watanzania: ujinga, maradhi, umasikini nk. Harakati hizi huzifanya kwa ufundi mzuri saana tu kiasi kwamba kama usipokuwa makini unaweza kuwaamini kwamba kweli ni wakombozi wa taifa hili. Lakini je, kweli CHADEMA kina DHAMIRA na MIKAKATI sahihi ya kulikomboa taifa hili? Au ni ufundi na ujanja ujanja wa kijasiriamali wa kuandika 'mchanganuo' mzuri wa kibiashara ili kujipatia mtaji (kura) halafu wajitengenezee faida binafsi?
Kiukweli kabisa, CHADEMA ni kama NGO ya kutengenea faida binafsi tu na hakina mpango wowote, wa kuaminika, wa kulikomboa taifa hili na uthibitisho wangu ni huu:
KUKWEPA KODI; wakati CHADEMA wanjua kuwa kodi ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato ya serikali ili kuendeshea shughuli mbalimbali za maendeleo, chama hiki kimekuwa mstari wa mbele kukwepa kodi. Viongozi wake wakuu ambao hulipwa fedha nyingi (ujira/mshahar) na ambao unatakiwa kukatwa kodi, wao kwa makusudi kabisa wamasema eti chama hakilipi wafanyakazi wake mishahara kinalipa POSHO! Wanafanya hivi makusudi ili kuepuka makato ya kodi katika mishahara kwani posho huwa hazikatwi kodi. Sasa kwa maoni yangu, huu nao ni ufisadi kama ufisadi mwingine; posho gani ya 1,000,000/=?!!
Dk SLAA NA URAIS NA MALIPO YA UBUNGE: mwaka 2010, akijua kuwa ilikuwa ngumu kumshinda JK katika uchaguzi wa urais, Slaa aligoma kogombea urais kwa kuogopa kukosa MAMILIONI YA SHILINGI ZA UBUNGE! Hivyo akatoa masharti kwa chama chake CHADEMA kuwa ataingia KUJARIBU URAIS lakini chama kimhakikishie kumlipa kila kitu ambacho mbunge atakuwa anapata kama vile na yeye ni mbunge1 Sasa hivi Dk Slaa analipwa na chama chake mshahara wa mbunge,posho, amepewa gari kama mbunge nk. Sasa, kama chama kinachojipambanua kwamba kinataka kuleta mabadiliko nchini, kwanini MASILAHI HAYA BINAFSI yanapewa kipaumbele kiasi hiki? Je, hili halitoshi kumshitua mtu makini kuwa kuna maigizo yanafanyika hapa? na hakuna dhamira ya dhati ya kumkomboa mwananchi?
SUALA LA POSHO ZA WABUNGE: kati ya mambo yaliyomuweka katika wakati mgumu katika chama chake Mh ZITTO ilikuwa suala hili la kupinga sitting allowance za wabunge. ZITTO alisimama kidete na kupinga kabisa posho hizi, hadi leo ni yeye peke yake ZITTO ambaye hachukui posho hizi. Kwa mara ya kwanza niliwaona wabunge wa CHADEMA wakiungana na CCM; walikuwa wakitetea posho hizi wakati wakijua kuwa kama posho hizi zingefutwa na fedha hizi zinaongezwa kwenye maendeleo angalau kitu kingfanyika katika kwakomboa wananchi dhidi ya umasikini.
Haya, pamoja na mambo mengine mengi tu, yatoshe kutushitua watanzania kuwa tunaimbishwa wimbo ambao hatujui kiitikio chake! Watanzania hasa vijana wenzangu, tuache ushabiki huu wa kisiasa bila kujua kuwa baadhi ya wanasiasa wana ajenda zao za siri ili hututumia sisi kama ngazi tu kufikia malengo yao ya kisiasa.
......................................Mungu ibariki Tanzania na watu wake..............................