Chadema hamjui mnazidiwa na mzee wa mpako

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Kama imeshindikana kuwa na redio au gazeti basi nunueni vipindi kwenye tv na redio na andaeni vipeperushi, cd na vijarida vya habari zinazowahusu. Watu hawakuelewa kwanini mlitoka bungeni mara mbili. Kwa hili la kujitangaza mnazidiwa hadi na MZEE WA MPAKO. Habari za kuhusu chadema kunasemu hazifiki kabisa. Zinafika propaganda tu kuwa ni chama cha vurugu udini na ukabila na watu wanahamini hayo. Napenda kuona chadema inafanya kazi kisayansi zaidi.

Kuanzia kubuni sera kujitangaza na kupigania haki. Mazungunzo yenu na JK KUHUSU KATIBA yasiwafunge mdomo. Mlikuwa kimiya mgomo wa madaktari. Mko kimiya madai ya walimu. Mko kimiya madai ya wafanyakazi. Kwa chadema imara hatutaitaji wanaharakti wala hasasi za kiraia.

TUNAOMBA TUMWONE SLAA ANAHUTUBIA TAIFA HATA KILA MWEZI KWENYE TV REDIO NA CD KUPITIA MKUTANO WA HADHARA NA KUONESHA MBINU MBADALA za kuokoa taifa. Ahutubie ikitokea sintofahamu yoyote inaohusu chama na taifa na si kuacha tbc ipige propaganga. Tujue uelekeo wa chama na kadharika.

SIAMINI KAMA HAMNA FEDHA. INAMAANA MNAWEZA MKAWA MNAZIDIWA KIPATO NA MZEE WA MPAKO. Weka kipindi maalumu tuone na hojazenu ata mnazozitoa bungeni msitegemee magezeti pekee watu bush hawawaelewi
 
Vyama vya Upinzani Tanzania havipewi nafasi sawa katika vyombo vya habari isipokuwa pale inapotokea habari mbaya au ya kuuzwa. Kwa mfano kila Hotuba ya rais kila mwezi inatakiwa viongozi wa vyama vya Upinzani wawe ktk studio za vyombo vya habari wafuatie kutoa maoni yao juu ya hotuba ya rais. Hakuna mtu anapenda sana kusikiliza siasa na hotuba isipokuwa za JK panapotokea tukio..

Inatakiwa pia wachambuzi wa mambo ya Siasa au Uchumi washirikishwe lakini tumekumbwa sana na utamaduni wa Muziki na Sanaa kiasi kwamba Taarifa za habari hazina mshiko..TV zoote na redio nchini zinapeperusha muda mrefu mziki kuliko taarifa, magazeti yote yanauza zaidi kwa udaku..hatuna chombo kama CNN, BBC, RT au CBC ni muziki kwa kwenda mbele hivyo tusipende sana kuwalaumu viongozi wa vyama kwa sababu mapenzi ya wananchi ni muziki na CCM huwapiga bao vyama vingine wanaposhirikisha wanamuziki ktk majukwaa yao ya uchaguzi..

Hivyo vijiji ambavyo unasema Chadema hawafiki hata CCM hawafiki lakini wanavijiji wanaposikia Sugu atakuwepo viwanja vya majani ya Chai basi watu hutoka vijijini kwenda kumsikiliza Sugu, wakifika Uwanjani wanakutana na kofia na T-shirt na burudani kwa kwenda mbele utadhani sherehe za Uhuru, wataacha vipi kuipenda CCM..
 
Kila mwanachama ana haki ya kutoa maoni yake mazuri kwa utaratibu unaofaa.
Sasa wewe unasubiri nini kutoa maoni hayo kwa uongozi?

Wazo zuri ila umewakilisha kama mipasho.
 
Kwani we hukufuatilia star tv meru? Ila pia huwezi ishi kwa mkate tu cdm ilipofika haijapigiwa promo ivyo itasambaa kama ilivyosambaa.cdm is just lik da brand
 
Kaka Mkandala,
Umeongea vizuri sana, lakini Chadema na hata vyama vingine vya upinzani inawapasa kulifanyia hili kazi, wajaribu kununua airtime labda ya saa moja kila wiki, wajaribu kuuza sera zao humo na kuelezea/kuyafafanua maswala yote yenye utata katika vyama vyao na hata serikali kwa ujumla wake

kuna Tatizo kubwa la umeme, sasa kama Chadema wakitoa misimamo yao Arumelu, watu wa Kigoma na sehemu zingine hawawezi kulipata hilo kikamilifu, lakini swala kama hilo sensitive ilipaswa lisemwe kwenye kipindi maalum na chama kama Chadema waelezee wakipewa madaraka watalitatuaje hilo tatizo
 
Mzee wa UPAKO anatumia miujiza aliyoshushiwa usimfananishe na wanasiasa matapeli, wanaohubiri wasioyatenda. Wanatumia helcopter wakati wanafunzi hawana madawati mashuleni.
 
Kaka Mkandala,
Umeongea vizuri sana, lakini Chadema na hata vyama vingine vya upinzani inawapasa kulifanyia hili kazi, wajaribu kununua airtime labda ya saa moja kila wiki, wajaribu kuuza sera zao humo na kuelezea/kuyafafanua maswala yote yenye utata katika vyama vyao na hata serikali kwa ujumla wake

kuna Tatizo kubwa la umeme, sasa kama Chadema wakitoa misimamo yao Arumelu, watu wa Kigoma na sehemu zingine hawawezi kulipata hilo kikamilifu, lakini swala kama hilo sensitive ilipaswa lisemwe kwenye kipindi maalum na chama kama Chadema waelezee wakipewa madaraka watalitatuaje hilo tatizo

Wakinunua airtime mfanyakazi wa ndani atalipwa na nini? hebu muwe wakweli jamani, chama kina majukumu mengi sana na ni muhumu ku-prioritize kila jambo. kwa sasa hili halipo katika list ya yaliomuhimu.
 
CDM inaendeshwa na nguvu ya umma,mzee wa upako ni freemanson pia mzee wa mapooooda na pia ni gamba! Ila good idea cdm kujitangaza zaidi sru tv etc
 
Acha upumbavu hapa tunazungumzia mambo ya vyama na siyo mambo ya nyumbani kwako.....
 
Wakinunua airtime mfanyakazi wa ndani atalipwa na nini? hebu muwe wakweli jamani, chama kina majukumu mengi sana na ni muhumu ku-prioritize kila jambo. kwa sasa hili halipo katika list ya yaliomuhimu.


Mfanyakazi wa ndani ndio nini?

Mkuu wala hufanani na unachoongea
 
Lusekelo ela za CHUMA ULETE na MAGAMBA,chadema tutajitangaza kwa kupitia M4C.ila changia chama.wasiliana kiongozi wa cdm
 
Kaka Mkandala,
Umeongea vizuri sana, lakini Chadema na hata vyama vingine vya upinzani inawapasa kulifanyia hili kazi, wajaribu kununua airtime labda ya saa moja kila wiki, wajaribu kuuza sera zao humo na kuelezea/kuyafafanua maswala yote yenye utata katika vyama vyao na hata serikali kwa ujumla wake

kuna Tatizo kubwa la umeme, sasa kama Chadema wakitoa misimamo yao Arumelu, watu wa Kigoma na sehemu zingine hawawezi kulipata hilo kikamilifu, lakini swala kama hilo sensitive ilipaswa lisemwe kwenye kipindi maalum na chama kama Chadema waelezee wakipewa madaraka watalitatuaje hilo tatizo
Mzingira kaka mazingira yanatukwaza kwa mengi. Chadema hawawezi kununua airtime ikiwa TV station wanaona haitauza matangazo maana ndio tegemeo kubwa sana la biashara hizi za habari.
Kikubwa ni kuwatazama watu wanataka nini na bila shaka sisi na muziki tumelogwa hivyo ukiwapelekea mwanamziki tuseme kesho Chadema wapeleke Twanga pepeta Arumeru, watu watatoka Arusha Mjini kwenda kuwaona Twanga Pepeta.. na hapo ndipo utakapo wakamata lakini kuwa na kipindi ktk TV uzungumzie siasa tuu na uchumi watu watakichoka mapema. Hapa JF pekee ukiandika makala ndefu inawachosha watu maana kusoma sii utamaduni wetu. Nimeambiwa sana nibadilishe na kuna ukweli mkubwa sana lakini kweli itawasaidia Watanzania ambao hawataki kusoma au ni kuwalemaza zaidi?..
 
Hayo yote ni mawazo mazuri Mkuu.. Ila ni kawaida wananchi wanapoanza kuchoka na maisha mabovu sio tv wala radio zinazowastua na kuwafanya wang'amue chama tawala ndo kinawapa hayo maisha mabovu na kinawapeleka kuzimu huku chama cha upinzani kinataka kuwarudishia uhai wao.. Huu mwamko unaouona sasa umechangiwa na maisha mabovu zaidi kuliko media..
 
Wachangiaji wengi mnamawazo yaliyonifumbua mengi ila nachoamini ni kwamba
1. Wengi nnatafuta sababu ya cdm kushindwa na si kushinda.
Yani hawawezi kwasabu. Hilo si sahihi
2. CCM Wana redio gazeti na Angalia TBC na yenyewe yao tu. Vikianza vikao vya bunge wanaoitwa asubui tbc sasa ni CCM AU CUF kuwakaanga chadema.
Tunachoambulia kuhusu chadema ni vichwa vya habari kwenye magazeti.
"chadema walipuka"
"SLAA AMLIPUA JK"
"TUNDULISU AMVAA SPIKA"
WAOMBE UFADHILI NDANI NA NJE. Wanunue airtime kwaajiri ya kufafanua hoja muhimu na hasa bunge likianza. Watumie vipeperushi majarida na redio. Vijijini hawafiki. UNAJUA KWANINI MWAKA 2010 ZAIDI YA 50% HAWAKUPIGA KURA. Sababu moja tu. Wanechoka uongo wa wanaccm na hawajui lolote kuhusu chadema. Nipinge kama uko kijijini. AKUNA CHA FREEMASON WALANINI GIZA HALIWEZI KUFUNIKA NURU
 
Kama imeshindikana kuwa na redio au gazeti basi nunueni vipindi kwenye tv na redio na andaeni vipeperushi, cd na vijarida vya habari zinazowahusu. Watu hawakuelewa kwanini mlitoka bungeni mara mbili. Kwa hili la kujitangaza mnazidiwa hadi na MZEE WA MPAKO. Habari za kuhusu chadema kunasemu hazifiki kabisa. Zinafika propaganda tu kuwa ni chama cha vurugu udini na ukabila na watu wanahamini hayo. Napenda kuona chadema inafanya kazi kisayansi zaidi. Kuanzia kubuni sera kujitangaza na kupigania haki. Mazungunzo yenu na JK KUHUSU KATIBA yasiwafunge mdomo. Mlikuwa kimiya mgomo wa madaktari. Mko kimiya madai ya walimu. Mko kimiya madai ya wafanyakazi. Kwa chadema imara hatutaitIaji wanaharakti wala hasasi za kiraia. TUNAOMBA TUMWONE SLAA ANAHUTUBIA TAIFA ATA KILAMWEZI KWENYE TV REDIO NA CD KUPITIA MKUTANO WA HADHARA NA KUONESHA MBINU MBADALA za kuokoa taifa. Ahutubie ikitokea sintofahamu yoyote inaohusu chama na taifa na si kuacha tbc ipige propaganga. Tujue uelekeo wa chama na kadharika. SIAMINI KAMA HAMNA FEDHA. INAMAANA MNAWEZA MKAWA MNAZIDIWA KIPATO NA MZEE WA MPAKO. Weka kipindi maalumu tuone na hojazenu ata mnazozitoa bungeni msitegemee magezeti pekee watu bush hawawaelewi

Pamoja na longo longo zote ulizoongea umeshindwa kutambua kuwa CDM siyo NGO inayotoka kwenye makao makuu yake na kwenda kujitangaza kwa walengwa. Ni chama cha siasa chenye wanachama kila sehemu na pana mahitaji tofauti tofauti kulingana na mahala husika pamoja na mazingira yake. Ni jukumu la kila mtu mahali alipo kushiriki kwa namna yoyote awezavyo kulingana na mazingira aliyomo kwenye juhudi za kuleta mabadiliko ya kweli. CDM jukumu lao ni kuratibu na kuunganisha juhudi za wapiganani wa maeneo mbalimbali. Kama wewe hapo ulipo umejikalia tu unasubiri cdm tv au dr slaa aje kwenye maeneo yako au atoe tamko, basi utasubiri sana!!!
 
Bado naumizwa sana. Tumeshindwa kuona mikutano ya M4C Live. Jamani ata recorded. IVI hamna fedha. Nakili kuwa mnanguvu sana mijijini na mfano Jf lakini vijijini bado
 
Back
Top Bottom