kwa kitendo chenu cha kuweka madaraka pembeni na kuweka nidhamu kwanza mmeonyesha mfano mzuri wa
kuigwa siyo ndani ya Tanzania bali hata africa nzima. hongereni kwa kutafuna mfupa uliomshinda fisi(CCM) pamoja na kuwa ni chama tawala kikiwa kinashikirianafasi mbalimbali ndani ya Nchi na kina miaka zaidi ya 30 toka kuanzishwa kwake lakini kimeendelea kukumbatia majambazi kwa ajili ya kuweka madaraka mbele. tumejionea wakishindwa kuwatimua na kuwachukulia hatua hata
viongozi wabunge na mawaziri wala rushwa na wengine wakipandishwa na vyeo hata baada ya kupata kashfa chungu nzima za kuwaibia wananchi mfano mzuri ni chenge,Lowassa,vullu, beth machangu, mke wa sitta, Rostam ........
kinachonifanya niwavulie kofia ni mlikuwa na uwezo wa kuendelea kushikilia umeya kwa kukubali kukumbatia uozo kama CCM inavyofanya ambayo imechangia kurudisha nchi nyuma lakini nawapeni hongera sana kwa kuchagua discipline kwanza kwa maslahi ya nchi badala ya nafasi ya umeya. mmeonyesha mfano mzuri wa kuwa mchezaji hata ukiwa mzuri kiasi gani kama huna nidhamu hufai, uongozi wa namna hii ktk vyama vya siasa ni mchache sana siyo Tanzania hata bara la africa.