Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtoa uzi laiti Dr Slaa angejua unapatikana wapi angekufuata akunyanganye na kadi yenyewe ya CDM.
Kwa leo hili nalo ni neno la mtu mwenye fikra mtambuka, wengi hawaelewi. Dr alijua kuna uwezekano wa kupoteza umea, lakini nidhamu kwanza. Tukianza vibaya katika hili CDM haitakuwa na sababu ya kuchukua nchi. Big up CDM.kwa kitendo chenu cha kuweka madaraka pembeni na kuweka nidhamu kwanza mmeonyesha mfano mzuri wa
kuigwa siyo ndani ya Tanzania bali hata africa nzima. hongereni kwa kutafuna mfupa uliomshinda fisi(CCM) pamoja na kuwa ni chama tawala kikiwa kinashikirianafasi mbalimbali ndani ya Nchi na kina miaka zaidi ya 30 toka kuanzishwa kwake lakini kimeendelea kukumbatia majambazi kwa ajili ya kuweka madaraka mbele. tumejionea wakishindwa kuwatimua na kuwachukulia hatua hata
viongozi wabunge na mawaziri wala rushwa na wengine wakipandishwa na vyeo hata baada ya kupata kashfa chungu nzima za kuwaibia wananchi mfano mzuri ni chenge,Lowassa,vullu, beth machangu, mke wa sitta, Rostam ........
kinachonifanya niwavulie kofia ni mlikuwa na uwezo wa kuendelea kushikilia umeya kwa kukubali kukumbatia uozo kama CCM inavyofanya ambayo imechangia kurudisha nchi nyuma lakini nawapeni hongera sana kwa kuchagua discipline kwanza kwa maslahi ya nchi badala ya nafasi ya umeya. mmeonyesha mfano mzuri wa kuwa mchezaji hata ukiwa mzuri kiasi gani kama huna nidhamu hufai, uongozi wa namna hii ktk vyama vya siasa ni mchache sana siyo Tanzania hata bara la africa.
Wanatumia kanuni ya idadi ya bora madiwani na bora meya. CCM hovyo kabisa.siku moja nilikuwa naangalia TV wkt wa bunge nilitamani kulia machozi niliposikia mbunge mzima wa ccm akisema kuwa lilikuwa ni kosa kwa Bunge kuunda tume ya mwakyembe ya kuchunguza richmond kwani imekiabisha chama(CCM) ina maana kiumbe kama huyu hafai kuwa mbunge kwani ameweka mbele maslahi ya chama badala ya nchi yake.
chadema inabidi mtembee kifua mbele na tukio la mwanza mlichukulie kama BADGE OF HONOR Kwamba hamtakubali kukumbatia wezi, wavivu, viongozi wasio na maadili kwa kuogopa vyeo vyao bali kuwashugulikia bila kujali vyeo vyao na mfano mzuri ni Mwanza na kwy harakati zote za M4C litajwe kama mfano hai wa kuweka mbele nidhamu badala ya wadhifa.