CHADEMA + CUF: Maandamano ya kitaifa

CHADEMA + CUF: Maandamano ya kitaifa

Nadhani serikali imezidisha matumizi ya mabavu sasa!
 
Kila kiashilia kinaonyesha machafuko makubwa yaja Tanzania!
 
Ipo haja yakufanya hivyo tena kwa haraka tunawaachia mno -c'mong guys!!

Alliance on common issues make sense
 
hilo haliwezekani .kwanza CUF zanzibar(wapemba) wamesharidhika na vipunje vichache vya mchele walivyorushiwa na ccm na wamesahau kabisa upande wa bara which means that akina lipumba wanatumika kama maboya tu ya kuvukia mto.wamegawana vyeo serikalini,lipumba kaachwa peke yake so ushirikiano na chadema is just adream.namshauri prof lipumba atoke cuf ajiunge na chadema kama alivyofanya prof safari.wananchi tunamkubali ila chama sicho!urojo mwingi....................
 
mimi naona CUF wasubiri kwanza jamani, CDM tuko kwenye vita nzito isiyohitaji mamluki hata kidogo, sina imani nao coz wao ni CCM B. now wanataka kuja huku wametumwa na nani? Rostam, Chenge au Lowasa? watueleze kabisa wanakuja kwa hisani ya nani kutoka CCM?
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo [Chadema] na Chama cha Wananchi [CUF] vimepanga kufanya maandamano mkoani Kigoma na Dar es Salaam kupinga kunyanyaswa kwa viongozi wake kunakofanywa na Jeshi la Polisi nchini.
Mkoani Kigoma Juni 11 nmwaka huu,Chadema watafanya maandamano ya amani kupinga unyanyasaji huo

Huku CUF imepanga kufanya maandamano yake Juni 12 mkoani Dar es Salaam kulaani kitendo cha Mahakama ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kumnyima dhamana Mbunge wa Viti maalum wa chama hicho, Magdalena Sakaya, na viongozi wengine wa kitaifa.

Upande wa Chadema wanapinga kupinga wka dhamana kwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alivyokamatwa na kupelekwa Arusha chini ya ulinzi mkali kama mhalifu wakati ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Chama hicho kimechukulia kitendo hicho kama ni udhalilishaji kwa kiongozi huyo na chama kwa ujumla na kuidhalilisha serikali

Pia maandamano hayo yana lengo la kuishinikiza serikali kutekeleza ahadi zake ilizotoa kwa muda mrefu mikoani hususani mkoa wa Kigoma na kuleta mabadiliko mikoani.

Maandamano ua CUF yataanza Ubungo na kuishia Manzese viwanja vya Bakhresa ambako utafanyika mkutano wa hadhara.
Mbali na lengo la kunyimwa dhamana kwa mbunge huyo pia CUF inafanya maandamano hayo kwa lengo la kupinga unyanyasaji unaofanywa na jeshi hilo
 
Sasa maandamano yatakosa radha na msisimko kama hata tunaandamana kwa issues za kawaida
 
1. Source?
2. Wana CDM tunasubili tamko rasmi kutoka kwa viongozi wetu. Tunafahamu kuwa kukamatwa kwa mbowe kulikuwa kwa kisiasa zaidi kuliko kwa kimahakama
 
Hayo maandamano kwa CDM haya tija yoyote, labda kama mnataka kuendelea kushuka chat! Tafuteni njia nyingine.
 
Mtu ana kula posho saba saba,we unaenda kuungua jua. Kwa hili hapana.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
AZMA YA KUTOSITISHA MAAANDAMANO YA KUPINGA MAUAJI YANAYOFANYWA NA POLISI
Imetolewa na Julius MtatiroNaibu Katibu Mkuu-Chama Cha Wananchi CUF – Tanzania Bara10/6/2011Chama Cha wananchi CUF kinasisitiza kuwa maandamano ya kupinga vitendo vya kinyama vya mauaji vinavyofanywa na jeshi la polisi dhidi ya wananchi wasioikuwa na hatia nchini yatakayofanyika tarehe 12/6/2011 yako palepale licha ya jeshi la polisi kupinga kwa sababu zisizokuwa na mashiko wala mantiki ya kikatiba. Kwa nini tutaandamana1. Tamko la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu la mwaka 1945, (The UN declaration of Human Rights of 1945) ambalo Tanzania ikiwa ni mjumbe rasmi wa Umoja wa Mataifa imeridhia,linatoa haki ya kuandamana ikiwa watu au chama kinataka kuonesha hisia zake kwa jamii husika ni muhimu kwa watanzania wote. 2. Katiba yetu ya jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, ambayo tayari ina viraka zaidi 14 inatoa haki kwa Raia wa Tanzania vikundi au taasisi kutoa mawazo au hisia zao ibara ya 20 kifungu 1 3. CUF ni chama chama siasa chenye kauli mbiu HAKI SAWA KWA WOTE, hivyo basi kitendo walichofanya Polisi cha kufyatua risasi ni cha kinyama kilichokatisha haki ya kuishi ya mtanzania mwenzetu huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora, CUF, tutaandamana ili kupinga kitindo hicho na vitendo kama hivyo. Tutaandamana ili polisi wote waliohusika katika mauaji ya wananchi wasio na hatia wafikishwe mahakamani na wachukuliwe hatua za kisheria. 4. Moja ya malengo ya kuanzishwa kwa chama cha wananchi (CUF) ni pamoja na kuwaunganisha watanzania, kukataa aina yoyote ya uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi, na uadhalilishaji wa kisiasa au wa kiuchumi. Hivyo basi CUF kama chama chenye usajili wa kudumu nchini, kilichosajiliwa kutokana na malengo yake, kinacho haki na wajibu wa kuungana na wananchi kupinga unyanyasaji na uonevu unaofanywa na jeshi la polisi nchini. 5.Kifungu cha 43(1) cha sheria za Polisi na Polisi Wasaidizi sura ya 322 kama ilivyoandikwa upya mwaka 2002 kinaeleza kuwa waandamanaji wanapaswa kutoa taarifa ya maandamano kwa ofisa wa Polisi masaa 48 kabla ya maandamano. Aidha kifungu cha 43 (3) kinaeleza kuwa Ofisa wa polisi hawezi kukataza maandamano chini ya kifungu cha 43(2); isipokuwa iwapo atajiridhisha kuwa mkusanyiko huo utasababisha uvunjifu wa amani au kuathiri usalama wa nchi au kuvunja utulivu wa nchi au kutumika kwa malengo yasiyo halali. Kwa manti hiyo kukataza maandamano bila Polisi kusema maandamano ya CUF yatavuruga vipi amani ni uzembe wa dhahiri na kamwe chama hakiwezi kusitisha maandamano kwa kutekeleza uzembe.6.Hoja ya Kova kwamba maandamanao ya CUF kesi za Urambo na Nyamongo zimeshafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria haina mashiko ya kwani kesi zote hizo si za mauaji bali ni kesi kukuasanyika kinyume na sheria.HIVYO CUF TUTAANDAMANA NA KUJARIBU KUTUZUIA NI KUVUNJA AMANI YA NCHI.NGUVU ZA POLISI KUTUZUIA ZITUMIKE KUTULINDA.
WOTE TUNAWAALIKA KATIKA MAANDAMANO.
HAKI SAWA KWA WOTE.
Julius Mtatiro,
10/06/2011
 
hivi wanaandamana dar pekeyake, vpi urambo kwenyewe au hawana wanachama..chadema tuwaunge mkono siku ya maandamano yao
 
Huko kwengine hakuna vyombo vya habari vya tv vya kuuzia sura.
 
Pole sana Mtatilo. Huwa najiuliza sana nini hasa malengo ya Mtatilo (ya kisiasa)kujiunga na CUF hasa baada ya kumaliza chuo (akiwa amejitengenezea jina kitaifa) pale Mlimani.
Pamoja na hayo yote vitendo vya polisi kuuwa raia ni vya kishenzi na havikubaliki hata kidogo.
Wito wangu ni chama makini cha upinzani kianzishe hoja ya kudai uwazi katika hii sheria ya polisi kutozuia maandamano ya wanachi tunapodai haki kwanza ndo tuanze kuandamana kwa issue nyingine. Tofauti na hapo mi naona tukiandamana tutaendelea kupigwa virungu, mabomu ya machozi, kuwekwa ndani na hata kuuwawa zaidi na hawa polisi vilaza.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
AZMA YA KUTOSITISHA MAAANDAMANO YA KUPINGA MAUAJI YANAYOFANYWA NA POLISI
Imetolewa na Julius MtatiroNaibu Katibu Mkuu-Chama Cha Wananchi CUF – Tanzania Bara10/6/2011Chama Cha wananchi CUF kinasisitiza kuwa maandamano ya kupinga vitendo vya kinyama vya mauaji vinavyofanywa na jeshi la polisi dhidi ya wananchi wasioikuwa na hatia nchini yatakayofanyika tarehe 12/6/2011 yako palepale licha ya jeshi la polisi kupinga kwa sababu zisizokuwa na mashiko wala mantiki ya kikatiba.Kwa nini tutaandamana1. Tamko la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu la mwaka 1945, (The UN declaration of Human Rights of 1945) ambalo Tanzania ikiwa ni mjumbe rasmi wa Umoja wa Mataifa imeridhia,linatoa haki ya kuandamana ikiwa watu au chama kinataka kuonesha hisia zake kwa jamii husika ni muhimu kwa watanzania wote.2. Katiba yetu ya jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, ambayo tayari ina viraka zaidi 14 inatoa haki kwa Raia wa Tanzania vikundi au taasisi kutoa mawazo au hisia zao ibara ya 20 kifungu 13. CUF ni chama chama siasa chenye kauli mbiu HAKI SAWA KWA WOTE, hivyo basi kitendo walichofanya Polisi cha kufyatua risasi ni cha kinyama kilichokatisha haki ya kuishi ya mtanzania mwenzetu huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora, CUF, tutaandamana ili kupinga kitindo hicho na vitendo kama hivyo. Tutaandamana ili polisi wote waliohusika katika mauaji ya wananchi wasio na hatia wafikishwe mahakamani na wachukuliwe hatua za kisheria.4. Moja ya malengo ya kuanzishwa kwa chama cha wananchi (CUF) ni pamoja na kuwaunganisha watanzania, kukataa aina yoyote ya uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi, na uadhalilishaji wa kisiasa au wa kiuchumi. Hivyo basi CUF kama chama chenye usajili wa kudumu nchini, kilichosajiliwa kutokana na malengo yake, kinacho haki na wajibu wa kuungana na wananchi kupinga unyanyasaji na uonevu unaofanywa na jeshi la polisi nchini.5.Kifungu cha 43(1) cha sheria za Polisi na Polisi Wasaidizi sura ya 322 kama ilivyoandikwa upya mwaka 2002 kinaeleza kuwa waandamanaji wanapaswa kutoa taarifa ya maandamano kwa ofisa wa Polisi masaa 48 kabla ya maandamano. Aidha kifungu cha 43 (3) kinaeleza kuwa Ofisa wa polisi hawezi kukataza maandamano chini ya kifungu cha 43(2); isipokuwa iwapo atajiridhisha kuwa mkusanyiko huo utasababisha uvunjifu wa amani au kuathiri usalama wa nchi au kuvunja utulivu wa nchi au kutumika kwa malengo yasiyo halali. Kwa manti hiyo kukataza maandamano bila Polisi kusema maandamano ya CUF yatavuruga vipi amani ni uzembe wa dhahiri na kamwe chama hakiwezi kusitisha maandamano kwa kutekeleza uzembe.6.Hoja ya Kova kwamba maandamanao ya CUF kesi za Urambo na Nyamongo zimeshafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria haina mashiko ya kwani kesi zote hizo si za mauaji bali ni kesi kukuasanyika kinyume na sheria.HIVYO CUF TUTAANDAMANA NA KUJARIBU KUTUZUIA NI KUVUNJA AMANI YA NCHI.NGUVU ZA POLISI KUTUZUIA ZITUMIKE KUTULINDA.
WOTE TUNAWAALIKA KATIKA MAANDAMANO.HAKI SAWA KWA WOTE.
Julius Mtatiro,
10/06/2011
Ninaunga mkono maandamano hayo na tena kauli ya mwisho rangi nyekundu ina mantiki kubwa mno.Ifike mahali tusisubiri wala kukubali uongo na visingizio vya kupinga maandamano.Vyama vyote vya upinzani na wanaharakati wote tushiriki maandamano
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar-es- salaam Suleiman Kova ameyapiga marufuku maandamano ya CUF yaliyopangwa kufanyika kesho kutwa Dar kwa sababu jeshi la polisi litakuwa lina mapokezi ya ugeni wa kitaifa na kimataifa kwa hiyo hawatakuwa na idadi ya polisi wa kutosha kusimamia maandamano hayo, wakati huo huo Naibu katibu mkuu CUF Bw.Julis Mtatiro amesema maandamano yao yako pale pale.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar-es- salaam Alfred Tibaigana ameyapiga marufuku maandamano ya CUF yaliyopangwa kufanyika kesho kutwa Dar kwa sababu jeshi la polisi litakuwa lina mapokezi ya ugeni wa kitaifa na kimataifa kwa hiyo hawatakuwa na idadi ya polisi wa kutosha kusimamia maandamano hayo, wakati huo huo Naibu katibu mkuu CUF Bw.Julis Mtatiro amesema maandamano yao yako pale pale.

Mkuu vipi tena? Tibaigana karudi tena kwenye utumishi wa jeshi la Polisi?
 
Back
Top Bottom