CHADEMA chazoa viti Mbeya vijijini, CCM hoi

Weraweraaaaaaaa!!Dalili ya mvua ni mawingu. Hakika wananchi wameanza kuelimika,Natamani 2015 umefike hata kesho.Wananchi wamechoka na kejeri za Chama Cha Mafisadi,mara tunajivua gamba,mara posho za wabunge ziongezwe eti maisha Dodoma yamepanda, wakati pale kuna wafanyakazi hawajaongezewa chochote, wananchi wa kawaida wanaishi bila matumaini ya kuamka,inakuwa heri ya jana kuliko leo.
CDM hongera saaaana na kaza kamba, songa mbele mpaka vijiji vyote,2015 ni yetu,Chama kilicho makini ndicho kitaikomboa Tanzania kutoka utumwani
 
Watu kwa kukuza mambo yaani kupata viti vinne tena vya vijijini ndio kuzoa viti?
 
Jana usiku nimesikiliza radio Five ya Arusha, wametangaza vitongoji vinne na kijiji kimoja vyote vimecukuliwa na CCM, Kumbe kulikuwa na vitongoji 18. Radio five hawatundei haki wananchi kwa kutupa habari vipandevipande tena za upande mmoja. Inamaana huyo Enerst Mdee( Mtoa taarifa) wao wa huko Mbeya, jana alipata matokeo ya vitongoji vyenye ushindi wa CCM peke yake ?

ndio kawaida yao mkuu,walitaka mkate tamaa.
 
Watu kwa kukuza mambo yaani kupata viti vinne tena vya vijijini ndio kuzoa viti?
Siku zote strategy ya ushindi wa CCM wanajua ni vijijini kule ambapo watu si waelewa kama mlivyofanya Igunga. Sasa watu wamefunguka macho sijui 2015 itakuweje maana dalili za mvua ni mawingu!!!!!!! Hongela CDM Mbeya vijijini hawa ni wetu mbona!!!!!!!!

 
tuwe tunapeana habari za kweli ja
mani.cdm wamepata vitongoji 2 na ccm 2.kwann tunapotosha?
 
tuwe tunapeana habari za kweli ja
mani.cdm wamepata vitongoji 2 na ccm 2.kwann tunapotosha?

naomba nikusaidie ili uwasaidie pia waliokutuma-chadema imeshinda vijiji vifuatavyo mageuzi,mshikamano,ndola na tunduma.Kwa upande wa vitongoji Chadema imeshinda vitongoji vya zahanati,kilimani,amani,chemichemi,mzalendo,maendeleo,muungano,upendo na kanani.Kwa upande wa ccm baadhi ya vitongoji ilivyoshinda ni vitongoji vya umoja,zedi,chunyaroad,mapogoro,mbugani na mji mkongwe.
 
tuwe tunapeana habari za kweli ja
mani.cdm wamepata vitongoji 2 na ccm 2.kwann tunapotosha?

huwa hatuokoti habari kama nyie mnavyofanya kwani mbali ya kuripotiwa kwa kirefu kwenye gazeti la nipashe jana lakini pia nimezungumza na mwenyekiti wa chadema kata ya Nsalala ndugu Stephano Mwasenga.
 
Back
Top Bottom