CHADEMA Chama la Wana na Kishindo Kimya Kingi!

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,822
Chadema kama taasisi inaendesha shughuli zake ofisini kwa mipangilio yake bila kusukumwa, kuchagizwa, kushinikizwa wala kushawishiwa na yeyeto.

Tulipo sasa mwenyekiti mheshimiwa Mbowe (mola amjalie salama) yuko nyuma ya nondo chini ya watesi wake ambao wangependa kuona Chadema ikisambaratika "forth with."

IMG_20210729_192941_480.jpg

Chadema kama watoto yatima nafasi yao ndani ya nchi wanaijua pasi na shaka. Wanayajua machungu yao. Wanayajua magumu yao. Wanajua hawana Mama, mjomba wala shangazi. Wanazijua hali zao.

IMG_20210704_051559_619.jpg

Wanajua hawana pa kukimbilia. Wanajua vyote jua na mvua vi juu ya vichwa vyao. Wanajua mtaji wa wao ni nguvu zao wenyewe. Wanajua silaha na ngao yao ni umoja na wingi wao.

Wamedhamiria kuzipambania hali zao na kwa hilo halipo linalo wasimamisha.

Kwamba watesi wa Mbowe wangependa ikiwezekana kumfutilia mbali Mbowe, kuifutilia mbali Chadema, kwani nani asiyelijua hilo? Kwamba sasa ndiyo wameikaribia adhimu yao hiyo? Thubutu!

Mbona itakuwa ni kujilisha upepo mchana kweupe?

Kutwa kucha kutengeneza chokochoko. Mara Mbowe katelekezwa jela, Mbowe ka "boogie step," Mbowe mwenyekiti wa maisha, Mbowe hana uungwaji mkono, kufanyike uchaguzi Chadema, kuwe na katiba mpya Chadema, nk, khaaaaaa!

Hivi hamna vyama vyenu? Au kwanini msianzishe vyama mkajiwekea hizo katiba zilizo bora kabisa kuliko zote duniani na ikibidi kuliko hata za huko mbinguni mliko na malaika viongozi?

Kila mtu, si johnthebaptist, USSR nk, ana lake alimradi wasikie kuna mipango gani. Wakudadavuwa naye bila shaka ni yulee..ee, fungeni milango anakuja!

Kweli kimya kingi kina mshindo mkuu.

Chadema iko salama na hali ni shwari.

Babu Loliondo katutangulia, tusifanye ajizi tupate "jab" zetu kama kipaumbele.

Maisha yetu na ya watu wengine ni ya muhimu zaidi kuliko vyote na muda wenyewe ni mchache.

Ninawasilisha.
 
Chadema lazima iangaliwe kwa jicho la tatu, kama mwenyekiti wa chama alikuwa Katili wa kupanga mauaji ya watu wengine, je hao walio chini yake na wafuasi aliwafundisha kitu gani kama sio uhalifu na ujambazi?! inawezekana sio wote lkn baadhi yao lazima wafuatiliwe ili kubaini matendo yao na wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Tunamshauri Msajili wa Vyama vya siasa afute huu mkusanyiko wa wahalifu walio jificha kwenye mwamvuli wa chama cha kisiasa.
Amani ya nchi yetu lazima italindwa kwa gharama yoyote ile, hatuko kuona kikundi cha watu wachache kinajaribu kuchezea amani ya nchi yetu.

kamwe hato chekewa mtu yeyote.
 
Wewe ni shetani na wewe na familia yako mlaaniwe!
Chadema lazima iangaliwe kwa jicho la tatu, kama mwenyekiti wa chama alikuwa Katili wa kupanga mauaji ya watu wengine, je hao walio chini yake na wafuasi aliwafundisha kitu gani kama sio uhalifu na ujambazi?! inawezekana sio wote lkn baadhi yao lazima wafuatiliwe ili kubaini matendo yao na wachukuliwe hatua kali za kisheria...
Kama Mungu aishivyo,Kama Mungu alivyo muondoa Magufuli mtesi kama wewe na afanye hivyo kwenu wote
 
Hata Kaburu wa Afrika kusini alikuwa na kauli za kipumbavu kama zako kuhusu kina Mandela na jamaa zao. Hata hivyo nisiache kukwambia:

Habari ndiyo hiyo.
 
Wewe ni shetani na wewe na familia yako mlaaniwe!

Kama Mungu aishivyo,Kama Mungu alivyo muondoa Magufuli mtesi kama wewe na afanye hivyo kwenu wote

Wanakereka mno kuona Chadema ni unshaken. Wanakereka mno kufahamu kuwa Chadema hufanya hesabu zake zote kabla ya jambo lolote:

Kwamba tulipo hata ingekuwa je tungekuwa bado tuko imara inawauma mno.

Chadema ni chama la Wana si hao wengine.

Kimya chake kina mshindo mkuu!
 
Chadema lazima iangaliwe kwa jicho la tatu, kama mwenyekiti wa chama alikuwa Katili wa kupanga mauaji ya watu wengine, je hao walio chini yake na wafuasi aliwafundisha kitu gani kama sio uhalifu na ujambazi?! inawezekana sio wote lkn baadhi yao lazima wafuatiliwe ili kubaini matendo yao na wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Tunamshauri Msajili wa Vyama vya siasa afute huu mkusanyiko wa wahalifu walio jificha kwenye mwamvuli wa chama cha kisiasa.
Amani ya nchi yetu lazima italindwa kwa gharama yoyote ile, hatuko kuona kikundi cha watu wachache kinajaribu kuchezea amani ya nchi yetu.

kamwe hatochekewa mtu yeyote.
 
Ongezeni na la 4 matatu hayatoshi. Usiache kumkumbusha Msajili na wote wanao husika kuhusu hili:

Sasa hivi tuko huku pia:

Habari ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom