CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!.

CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!.

Wanabodi
Declaration of interest. Paskali sio mwanachama, mfuasi, mshabiki wa chama chochote cha siasa, bali ni Mtanzania Mzalendo wa nchi yake anayetanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kutoa mawazo, maoni na mapendekezo yake freely kwa ukweli daima bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani au utamuumiza nani, kwa sababu ukweli ni ukweli tuu na utasisima mpaka mwisho.

Naomba kukiri kupandisha bandiko hili kutokana na bandiko hili

Kiukweli kama hili litafanyika, Chadema kitakuwa ni chama cha ajabu sana! . Kinapeleka mahakamani issue ndogo ambayo sio issue kabisa ya kisheria bali ni kikanuni tuu!, lakini kumetokea very serious issues za kukanyagwa kwa katiba ambako ndiko haswa kungehitaji legal interpretation Chadema inakupiga kwa kuunda UKUTA na kuhamashisha mandam ano na mikutano nchi mzima!.

Spika is right, kati ya wabunge 9, watatu ni wanawake. CCM ina nafasi 6 imepeleka wanawake 6 na wanaume 6. Opposition wana nafasi 3, walipaswa kupeleka wagombea angalau 6 ambapo 3 wanaume, 3 wanawake.

Hata kama kati ya nafasi 9 za Tanzania wanawake ni watatu na tayari CCM inao wanawake watatu, wanaochagua wabunge wa EALA ni Bunge la JMT na sio CCM, hivyo hiyo haki ya female represention lazima ionekana kwa vyama vyote ili wabunge wa Bunge la JMT wawe na choice to choose from all parties na sio kulazimishwa kuwakumbatia wagombea wa CCM.

Nadhani Chadema wanamtegemea sana Lisu kwenye legal interpretation, yes Lisu ni mwanasheria mzuri, nguli na mbobezi ila sio mzuri saana kivile kwenye kanuni, udhaifu wa Lisu ulionekana wakati wa muswada wa katiba aliwaingiza chaka opposition wote kama nilivyo eleza hapa
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Hivyo kama ndiye aliyewashauri Chadema waende mahakamani kupinga uchaguzi wa EALA wakati uchaguzi ni leo, the anawaingiza tena chaka.

The best thing to do kwa Chadema ni kufuata tuu sheria, taratibu na kanuni, kwa Chadema kurekebisha makosa katika muda waliopewa.

Japo ni kweli Mahakama ndio chombo rasmi cha kutoa legal interpretation nchini Tanzania hivyo Chadema kinaitumia haki hiyo, kwanza wakamilishe taratibu na kanuni za kibunge kwa kufuata maelekezo ya Spika wakati wakijaribu kusimamisha uchaguzi huo mahakamani, kwa sababu uwepo wa wagombea kutoka Chadema sio prerequisite ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Mahakama haitausimamisha uchaguzi huo kwa respect ya the principles of separation of powers kutoingilia Mhimili wa Bunge, na hata wakiusimamisha , bado uchaguzi utafanyi kwa Mhimili wa Bunge hautakubali kuingiliwa na Mahakama, hivyo Chadema wata loose big time.

Hawajifunzi kwa CUF ambao ni loosers, CUF walipotangaza kususia uchaguzi wa marudio Zanzibar walidhani uchaguzi ungeshindikana, amini usiamini saa hizi Maalim anajuta, anautamani hata ule umakamo! .

Kiukweli Chadema ni chama cha ajabu sana, kinakimbilia mahakani kutafuta legal redress kwenye trivia issue ndogo tuu za kanuni, halafu very serious issues kama kuvunjwa kwa katiba na rais wa JMT, wao ndio wana deal nayo kwa kuunda UKUTA na kupanga maandamano na mikutano nchi nzima?!.

Katiba imetoa uhuru kwa vyama vya siasa kukutana na kufanya mikutano ya kisiasa. Ametokea mtu aliyeapa kuilinda katiba lakini akaikanyaga. This is very serious allegations ambazo ndizo zingehitaji haswa a legal redress, kutoka kwa mabingwa na wabobezi wa sheria.

Nilijitahidi kutafuta Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!

Chadema walipounda UKUTA kupinga udikiteta, niliwauliza hivi katiba ikikiukwa solution yake ni kufanya maandamano na mikutano? .Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Mwaka 2014 wakati tukisubiria uchaguzi wa 2015, niliwahi kutoa ushauri wa bure kwa Chadema kuhusu udikiteta CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!
Halafu watu kama hawa ndio watujie ile 2020 kuwaomba Watanzania wawakabidhi nchi?!.

Pia nilishauri
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Uchaguzi wa Mwaka 2015 Chadema ilikuwa ina stand better chances kuchukua nchi only if Chadema wangezitia hili
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni .....!

Hivyo wote wenye matumaini ya mageuzi Tanzania, wana very high expectations na Chadema, as a leeder on opposition atakaye kwenda kuipumzisha CCM, lakini unfortunately and very sad kwa nchi yetu Tanzania, Chadema ina wa let down kwa issues kama hizi za kijinga kijinga zinazoipotezea muda Chadema kushinda mahakamani kufunga na kufungua, 2020 hiyo hapo.

CCM iliishachokwa siku nyingi, kuna watu kibao wangependa kuipiga chini CCM hata kesho, wakiwemo CCM wenyewe, tatizo ni waikabidhi nchi kwa nani? .

Tanzania bado hatuna kabisa a serious opposition ya kuiangusha CCM 2020, hivyo kwa Watanzania wengi hata 2020 wataingia kwenye uchaguzi wakiwa faced na two choices, in between the two devils, you choose the lesser! .

Niliwahi kusema mahali kuwa CCM ni li zimwi na Watanzania wengi wanajua wakiwemo wana CCM wenyewe, lakini unapokuwa faced na mazimwi mawili, unachagua zimwi likujualo, better a devil you know than you don't know, sasa kama mambo ya Chadema ndio kama haya kwenye mambo madogo madogo, tutegemee nini 2020? .
Nawatakia Bunge jema.
Jumanne njema.
Paskali
Tatizo kubwa mtu akishazoea MAKESI KESI, basi hata jambo ambalo ni la kimsingi yeye ni kwenda mahakamani tu kufanya KESI.
Kwa lugha nyingine mtu huyo hu enjoy MAKESI.
Prerequisite ya kiongozi mzuri ni UTULIVU before he acts or reacts for that matter.Na si KUKURUPUKA na kukimbiza mambo. Acha tusubiri kesi!
 
Mkuu Pascal Kusema ukweli kabisa, Mimi Ni mshabiki wako Mkubwa, ila Kuna kipindi unapungukiwa hekima, Na kipindi hiki nadhani Ni zaidi.
Huwezi wapangia watu wenye mrengo Wao namna ya kuendesha mambo Yao kwa kadiri wanavyoona Wao, provided hawa athiri haki za watu wengine.
Na ukiangalia kwa Makini, Chadema wana set trend ya kutaka Kila jamboo lenye utata litafsiriwe kisheria.... Itatisaidia Sana huko tuoendako.

Ni mwehu Tu anaeweza kukwambia Jirani yake mbona unakula ugali samaki wakati Kuna maziwa Na Nyama kwenye friji....
Utainekana wa hovyo Sana,.... Unakaribia hapo.
Mwehu ni yule anayeambiwa "upo uchi" na yeye anadhani anaonewa wivu. Bwana Paskali acha hawa wafu wazike wafu wenzao.
 
Unajua sometimes tunatakiwa kuweka ushabiki pembeni na tuwe very reasonable japo ni wapinzani..Mbowe kawapatajepataje hawa watu wawili?Unajua Mbowe ana mapungufu tena Makubwa sana! Ukweli lazima usemwe hata ktk mambo ya ubunge viti maalum mafigisu kibaoo..! Mbowe jitathmini bwana watu wengine ambao tuwashabiki wa chama chako sio wakufata mkumbo kwa kila kitu twajitambua tena sana! Jiongeze!
 
Yoyote aliyewashauri CDM waende mahakamani ni aina ya watu wale wagomvi wagomvi kila kitu lazima abishane na kupinga pinga tu.
Kanuni zinasema at least 1/3 , kwa hesabu rahisi tu inamaanisha jinsia yoyote isisizidi 2/3 wala kupungua 1/3. Kama CDM wakiweka 50-50 watakuwa wametimiza sharti hili ila wao wanazidi kushupaza shingo, acha waende kuaibika huko mahakamani.

1/3 _< jinsia yoyote _< 2/3
 
Mkuu adui Namba moja katika taifa hili ni CCM.
Tusiwategemee sana hawa CHADEMA, ila tupambane kila ulipo kwa nafasi yako ikiwezekana tukawatumia tu CDM kama daraja la kuing'oa CCM kama adui namba moja, tupaze sauti lengo likiwa moja kuing'oa CCM.. CCM ikishajiendea ni rahisi kudeal na haya matatizo mengine ambayo yatakuwa hata mizizi hayana au bado kukomaa..
inaonekana una makengeza ya akili hivi kati ya cdm na ccm nani adui wenu namba moja? eti tuitumie cdm kuondokana na ccm una mawazo ya kipumbavu kabisa, pelekeni daftari la mahudhurio la wapiga kura tatizo liko wapi?
 
PASCAL MAYALA KWA KI KWETU MAANA YAKE NI NJAAA.

i hope wazaz hawakukosea kukupa hili jina maana linasadifu yanayoendelea kwako sasa hivi

Yeye anaitwa Pascal na Baba yake anaitwa Mayalla, sasa aliekuja na jina la Mayalla si anatakiwa kuwa Babu yake?

Ukishirikisha hiyo grey matter ipo kichwani kwako nadhani utanielewa.
 
Pascal naona umeheuka wewe unaona katiba ndio serious issue? Je CCM walivyogawanya wilaya ya Kinondoni ili wapate meya Kwa figisu


Toka aambiwe jina lake kwa kisukuma maana yake ni njaa amekuwa mtu wa hoyo kabisa huyu mtani wangu. Sijui alikuwa haijui hiyo maana kabla ya hapo?
 
Kama watu mtaacha kutumia MIHEMKO na kuamua kutumia akili hata kwa Dakika Tano Mtaelewa Hoja hii ya mleta HUU UZI. HUWA NASEMA MOJA YA TATIZO KUBWA WALILO NALO VIJANA WA SASA NI KUACHA KABISA KUTUMIA AKILI. WAMEZIPUMZISHA AKILI MPAKA ZIMEKUWA NA KUTU. NEVER USED. WANATUMIA HISIA,ITIKADI,IMANI NA MIHEMKO KUAMUA MAMBO. Vijana wengi wa leo wana ubongo mpya kabisa NEVER USED.
CHADEMA HAITAKUJA KUSHINDA UCHAGUZI BILA MABADILIKO YA KATIBA. HILO WASAHAU NA SIKU WAKISHINDA MIMI NAHAMA TZ NAHAMIA SYRIA KWENYE MAPIGANO AU SOMALIA.

IT WILL NEVER EVER HAPPEN
. katiba ndo msingi mkuu wa mabadiliko na hili kama vyama vingekuwa kweli vina nia njema na nchi hii ndo vingesimamia badala ya kukimbizana na kesi ndogo ndogo zisizo na tija kwa Ukombozi wa Taifa hili. KATIBA MPYA NDIO ITAKAYO OKOA TAIFA HILI.
 
Back
Top Bottom