CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,660
119,278
Wanabodi

Declaration of interest, japo Paskali ni mwanachama, wa chama cha siasa, maoni yangu ni maoni ya Mtanzania Mzalendo wa kweli wa nchi yake anayetanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kutoa mawazo, maoni na mapendekezo yake freely kwa ukweli daima bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani, utamuudhi nani au utamuumiza nani, kwa sababu ukweli ni ukweli tuu lazima usemwe, na siku zote ni ukweli tuu ndio utasisima mpaka mwisho.

Nayaandika haya kwa nía njema ile ile ya kwenye mazuri tupongeze, kwenye mapungufu tukosoe na kwenye mabaya tulaani kwa nia ya kujenga, "constructive criticism", kama tunavyoikosoa serikali yetu kwa lengo la kuisaidia, sisi ambao japo ni wanachama wa chama cha siasa, lakini mawazo yetu sio ya siasa za vyama (partisan politics) pia tutavikosoa vyama vya siasa sio kwa lengo la kubeza, bali kwa lengo la kuvisaidia.

Kati ya udhaifu mkubwa kabisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, na ndio ambao unaifanya Watanzania kushindwa kuiaminia na kuikabidhi ikulu yetu, ni kitendo cha Chadema kupoteza muda mwingi wa thamani, kwa kukumbatia siasa za matukio badala ya siasa za mikakati, kitu kinachoifanya kuendelea kupoteza muda kwa kupiga mark time pale pale ilipo, badala ya kusonga mbele, hali inayopelekea ikulu kuishia kuisikia tuu!.

CCM, iliishachokwa siku nyingi, kama Chadema wangeitumia vizuri advantage ya kuchokwa kwa CCM, zamani cHADEMA ingeishakuwa Ikulu siku nyingi kama ingejikita katika siasa za kweli za kimipango mikakati na sio siasa za matukio na na siasa za maji taka.

Bunge la bajeti linakwenda kuanza ndilo the most serious na longest session ambapo wapinzani makini wenye utayari wa kutawala nchi wanatakiwa kuonyesha uwezo wa kuichallenge serikali kwa bajeti mbadala kwenye kila sekta kuonyesha kuwa Watanzania walifanya makosa sana kuichagua CCM iwapo wangekuwa wao wangefanya hili na lile na nchi yetu ingekuwa mbali ili 2020 Watanzania wawaaminie wawakabidhi nchi, lakini subirini tutaambiana, kama mwanzo wenyewe ndio huu!.

Niliishasema siku nyingi kuwa CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Lakini kwa hii CCM ya Magufuli inavyojipanga, sijui tutarajie nini kwa opposition come 2020. Magufuli is a game changer, amebadili mfumo wa siasa za CCM, hivyo kuelekea 2020, upinzani unakwenda kunyauka sana kama sio kufa kabisa!.

Naomba kukiri kupandisha bandiko hili kutokana na bandiko hili
Ubunge wa EALA: CHADEMA hatukukosea, tutaenda Mahakamani kupinga ...

Kiukweli kama hili litafanyika, Chadema kitakuwa ni chama cha ajabu sana! . Kinapeleka mahakamani issue ndogo ambayo sio issue kabisa ya kisheria bali ni issue ya kikanuni tuu!, lakini kumetokea very serious issues za kisheria kama kukanyagwa kwa katiba kile kipengele cha uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano, ambako ndiko haswa kungehitaji legal interpretation Chadema inakipiga kwa kujenga UKUTA na kuhamashisha mandamano na mikutano nchi mzima, ambapo kwa chama serious, hii ndio issue ya kupeleka mahakamani.

kanuni ya ubunge wa EALA iko wazi kabisa inasema kila chama kiteue wabunge, lakini angalau theluth moja wawe wanawake. Hivyo Spika yuko right kuwazuia Chadema, kati nafasi 9 za wabunge EALA kwa Tanzania, Angalau nafasi 3 lazima zishikwe na wagombea wanawake. Mgawanyo wa jumla wa nafasi hizo ni kwa CCM ina nafasi 6, Chadema ina nafasi 2, na CUF ina nafasi moja. CCM imepeleka wanawake 6 na wanaume 6. Kwenye nafasi 3 za Opposition, nao walipaswa kupeleka wagombea angalau 6 ambapo 3 wanaume, 3 wanawake.

Hata kama kati ya nafasi 9 za Tanzania wanawake ni watatu na tayari CCM inao wanawake watatu, wanaochagua wabunge wa EALA ni Bunge la JMT na sio CCM, hivyo hiyo haki ya female representation lazima ionekana kwa vyama vyote ili wabunge wa Bunge la JMT wawe na choice to choose from all parties na sio kulazimishwa kuwakumbatia wagombea wa CCM.

Nadhani Chadema wanamtegemea sana Lisu kwenye legal interpretation, yes Lisu ni mwanasheria mzuri, nguli na mbobezi ila sio mzuri kwa kila kitu, au ni mzuri saana kivile kwenye kanuni, udhaifu wa Lisu kwenye kanuni, ulionekana wazi wakati wa muswada wa katiba aliwaingiza chaka opposition wote kama nilivyo eleza hapa

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Hivyo kama ndiye aliyewashauri Chadema waende mahakamani kupinga uchaguzi wa EALA wakati uchaguzi ni leo, then anawaingiza tena chaka!.

The best thing to do kwa Chadema ni kufuata tuu sheria, taratibu na kanuni, kwa Chadema kurekebisha makosa katika muda waliopewa.

Japo ni kweli Mahakama ndio chombo rasmi cha kutoa legal interpretation nchini Tanzania hivyo Chadema kinaitumia haki hiyo, kwanza wakamilishe taratibu na kanuni za kibunge kwa kufuata maelekezo ya Spika wakati wakijaribu kusimamisha uchaguzi huo mahakamani, kwa sababu uwepo wa wagombea kutoka Chadema sio prerequisite ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Mahakama haitausimamisha uchaguzi huo kwa respect ya the principles of separation of powers kutoingilia Mhimili wa Bunge, na hata wakiusimamisha , bado uchaguzi utafanyika kwa Mhimili wa Bunge hautakubali kuingiliwa na Mahakama, hivyo Chadema wata loose big time.

Kwa nini Chadema hawajifunzi kwa CUF ambao ni loosers, CUF walipotangaza kususia uchaguzi wa marudio Zanzibar walidhani uchaguzi ungeshindikana, amini usiamini saa hizi Maalim na CUF wanajuta ila hawasemi, kuna mtu anautamani hata ule umakamo tuu!, vingora sio mchezo! .

Kiukweli Chadema ni chama cha ajabu sana, kinakimbilia mahakani kutafuta legal redress kwenye trivia issue ndogo tuu za kanuni, halafu very serious issues kama kuvunjwa kwa katiba na rais wa JMT, wao ndio wana deal nayo kwa kuunda UKUTA na kupanga maandamano na mikutano nchi nzima?!.

Katiba imetoa uhuru kwa vyama vya siasa kukutana na kufanya mikutano ya kisiasa. Ametokea mtu aliyeapa kuilinda katiba lakini akaikanyaga!. To me this is very serious allegations ambazo ndizo zingehitaji haswa a legal redress, kutoka kwa mabingwa na wabobezi wa sheria.

Nilijitahidi kutafuta Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!

Chadema walipounda UKUTA kupinga udikiteta, niliwauliza hivi katiba ikikiukwa solution yake ni kufanya maandamano na mikutano? .Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Mwaka 2014 wakati tukisubiria uchaguzi wa 2015, niliwahi kutoa ushauri wa bure kwa Chadema kuhusu udikiteta CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Halafu watu kama hawa ndio watujie ile 2020 kuwaomba Watanzania wawakabidhi nchi?!.

Pia nilishauri

Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Uchaguzi wa Mwaka 2015 Chadema ilikuwa ina stand better chances kuchukua nchi only if Chadema wangezingatia hili
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni .....!

Hivyo wote wenye matumaini ya mageuzi Tanzania, wana very high expectations na Chadema, as a leader of a serious and strong opposition atakaye kwenda kuipumzisha CCM, lakini unfortunately and very sad kwa nchi yetu Tanzania, Chadema ina wa let down Watanzania kwa issues kama hizi za kijinga kijinga zinazoipotezea muda Chadema kushinda mahakamani kufunga na kufungua, 2020 hiyo hapo.

CCM iliishachokwa siku nyingi, kuna watu kibao wangependa kuipiga chini CCM hata kesho, wakiwemo CCM wenyewe, ila ujio wa Magufuli sasa umegeuza kibao, badala ya CCM kuendelea kuchokwa sasa CCM ndio inaendelea kupendwa, haijalishi kama kupendwa huko ni kupendwa kwa mapenzi ya dhati na huru, au CCM inapendwa kwa kupendeshwa kwa mbinu!, the bottom line is sasa CCM inapendwa!, hivyo Chadema kama ndio hii na ikiendelea hivi, amini nawaambie sijui kama 2020 kuna Chadema au opposition atakayerudi Bungeni!. Watanzania wana kiu sana ya mageuzi, lakini tatizo ni waikabidhi nchi kwa nani?! .

Tanzania bado hatuna kabisa any serious strong opposition ya kuiangusha CCM 2020, hivyo kwa Watanzania wengi hata 2020 wataingia kwenye uchaguzi wakiwa faced na the same two choices, in between the two devils, you choose the lesser!, a devil you know than a devil you don't know!.

Niliwahi kusema mahali kuwa CCM ni li zimwi na Watanzania wengi wanajua wakiwemo wana CCM wenyewe, lakini unapokuwa faced na mazimwi mawili, unachagua zimwi likujualo, better a devil you know than you don't know, sasa kama mambo ya Chadema ndio kama haya kwenye mambo madogo madogo, tutegemee nini 2020? .

Naelewa matokeo ya ukosoaji wowote wa Chadema humu jf, naomba kuwahakikishia Wanachadema kuwa mimi ni miongoni mwa watoaji wa fedha zangu kwenye ruzuku yao hivyo nina haki yote ya kuzungumza lolote kuhusu hatma ya matumizi ya kodi yangu ndio maana nilishauri Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi

Nawatakia Bunge jema.

Jumanne njema.

Paskali
 
Kwa hiyo unaona hakuna umuhimu, kwa chama , kwenda kudahi tafsiri ya kisheria pale wanapoamini hawajatendewa haki.
Jitahidi kuwa mtiifu kutumika kupotosha one day utakuwa mteule.
 
Mkuu hakuna anayetaka kusikia sauti kama hizi.

Mimi naandika kila siku juu ya CHADEMA kutokuwa na uchungu na nchi hii kama CCM au zaidi ya CCM wenyewe tusiowataka.

Issue kama Katiba Mpya na Kudai Tume Huru ya Uchaguzi hawaoni kama ni tatizo kwao mpaka watakapopigwa 2020. Najua watakuja na maneno ya kuibiwa tena!!!

Ila ukweli ni kuwa wamewekeza kwenye mabishano yasiyokuwa hata na documentation.

Mitandao ni ya Watanzania si zaidi ya Laki 7-1.5m. Haiwezi kuitoa CCM yenye ngome ya wakulima 80-90 ya wakulima na masikini.
 
Mkuu Pascal Kusema ukweli kabisa, Mimi Ni mshabiki wako Mkubwa, ila Kuna kipindi unapungukiwa hekima, Na kipindi hiki nadhani Ni zaidi.
Huwezi wapangia watu wenye mrengo Wao namna ya kuendesha mambo Yao kwa kadiri wanavyoona Wao, provided hawa athiri haki za watu wengine.
Na ukiangalia kwa Makini, Chadema wana set trend ya kutaka Kila jamboo lenye utata litafsiriwe kisheria.... Itatisaidia Sana huko tuoendako.

Ni mwehu Tu anaeweza kukwambia Jirani yake mbona unakula ugali samaki wakati Kuna maziwa Na Nyama kwenye friji....
Utainekana wa hovyo Sana,.... Unakaribia hapo.
 
Hayo ni mawazo kama mawazo mengine, na sio lazima kila unachokiwaza kiwe sahihi au sio sahihi lakini mwisho kabisa kila swali lina jibu lake sahihi.

CCM ni Zimwi linalonyonya maendeleo ya nchi hii na kutuchelewesha kufika kwenye maziwa na asali, Kwa sasa tupambane wote kwa nguvu zetu kuliua hili Zimwi haya mengine tuyaache tu akina Mbowe na Lissu waendelee na sinema zao, kwa sasa adui Namba moja ni CCM, tupambane kuliua hili zimwi aka adui namba moja huko baadaye hawa maadui wadogodogo tuachane nao kwanza...
 
Uchanguzi wa EALA utakuwa leo na chadema watakuwa wamepoteza rasmi nafasi zao mbili, kuna ugumu gani kulekebisha makosa na kuendelea na uchaguzi?
Mie nawashangaa nikwann wanalazimishia chaguo la masha na wenje tu?!
kwani ukipeleka majina ya wanachadema wa5 (wakiwemo wanawake) alafu miongoni mwao wakapatikana wa2 kuna tatizo gani?!
hao wanaolazimishiwa kama wangekuwa majembe wangelishinda huko jimboni.....masha mwenyewe wakuja tu kakuta wafia chama ambao leo wanaonekana si chochote ndani ya chama!
 
Mkuu hakuna anayetaka kusikia sauti kama hizi.

Mimi naandika kila siku juu ya CHADEMA kutokuwa na uchungu na nchi hii kama CCM au zaidi ya CCM wenyewe tusiowataka.

Issue kama Katiba Mpya na Kudai Tume Huru ya Uchaguzi hawaoni kama ni tatizo kwao mpaka watakapopigwa 2020. Najua watakuja na maneno ya kuibiwa tena!!!

Ila ukweli ni kuwa wamewekeza kwenye mabishano yasiyokuwa hata na documentation.

Mitandao ni ya Watanzania si zaidi ya Laki 7-1.5m. Haiwezi kuitoa CCM yenye ngome ya wakulima 80-90 ya wakulima na masikini.

Mkuu adui Namba moja katika taifa hili ni CCM.
Tusiwategemee sana hawa CHADEMA, ila tupambane kila ulipo kwa nafasi yako ikiwezekana tukawatumia tu CDM kama daraja la kuing'oa CCM kama adui namba moja, tupaze sauti lengo likiwa moja kuing'oa CCM.. CCM ikishajiendea ni rahisi kudeal na haya matatizo mengine ambayo yatakuwa hata mizizi hayana au bado kukomaa..
 
Kwa hiyo unaona hakuna umuhimu, kwa chama , kwenda kudahi tafsiri ya kisheria pale wanapoamini hawajatendewa haki.
Jitahidi kuwa mtiifu kutumika kupotosha one day utakuwa mteule.
Hiki ndicho kinachoitafuna Chadema. Adui yenu mkubwa sio CCM bali UKWELI..Hamtaki kabisa kuambiwa UKWELI. Na hamtaki kuambiana UKWELI. Hivi ule mtumba mliouita fisadi miaka tisa mfulizo, kisha mkaufanya kuwa mgombea wenu wa urais 2015, UKO WAPI?
 
Unasahau wewe siku ile mna mkutano na waandishi wa habari mliuliza kuhusu katika kwa Magufuli na mkajibiwa kuwa hilo kwake si Kipaombele chake na halipo kwenye ilani yake ya uchaguzi halafu hapa unajifanya kuwananga Chadema kana kwamba wao ndo wanaobeba msalaba wa watanzania wote. Au mwenzetu betri imeisha chaji?
 
Huwezi ukaonyesha akaona shetani anamtoa shetwani ukasema hakuna mapepo tena. Wanachofanya CHADEMA kwa sahizi si tofauti sana na CCM. Inaweza ikawa zaidi ila watu wengi wanamaneno kama yako.

Hata wakiendelea kama hivi hawatafika wanakotaka waende maana wanajichanganya sana. Kwa wenye akili wanaona.
Mkuu adui Namba moja katika taifa hili ni CCM.
Tusiwategemee sana hawa CHADEMA, ila tupambane kila ulipo kwa nafasi yako ikiwezekana tukawatumia tu CDM kama daraja la kuing'oa CCM kama adui namba moja, tupaze sauti lengo likiwa moja kuing'oa CCM.. CCM ikishajiendea ni rahisi kudeal na haya matatizo mengine ambayo yatakuwa hata mizizi hayana au bado kukomaa..
 
Back
Top Bottom