BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,021
- CCM ooha Chadema, taifa linakwenda chini mkuu kuna hoja muhimu za taifa sasa hivi badala ya hizi nyepesi nyepesi!, hivi umesikia kwua kuna wanafunzi wengi wamepasi primary lakini hawana shule za kwenda form one?
Hapa FMES umezungumza point kubwa sana. Inasikitisha kusikia maelfu ya watoto wa Kitanzania ambao wamepasi mitihani yao ya darasa la saba lakini kutokananna upungufu wa madarasa hawataendelea na masomo yao ya secondary. Idadi ya watoto hawa kwa nchi nzima inaweza kuzidi 300,000 hawa no watoto wengi sana kuacha wazagae hivi hivi tu.
Wakati huo huo tunaachia 'wawekezaji' wachukue 97% ya rasilimali zetu!!! Mimi kwa maoni yangu yale mabilioni ya EPA kama kweli yamerudishwa basi yaelekezwe katika kujenga madarasa na kuwaendeleza waalimu katika mikoa yote ya nchi yetu ili tusisikie tena hili la maelfu ya Wanafunzi wa shule za msingi waliopasi wanakosa nafasi za kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa madarasa. Huu ni uzembe wa hali ya juu sana.