Chadema, CCM yametimia

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,573
31,887
Wanabodi..
Mwenendo wa kisiasa, kati ya watani wa jadi CCM na Chedema sasa umeanza kuzua mijadala ndani ya jamii.

Wananchi wanahoji iko wapi kasi na upepo wa mabadiliko ilikuwa nao Chadema mwaka 2010 na mwaka jana ilikoyeyukia.

Huku CCM kilichokuwa kimeanza kudorora sasa kikionekana kupaa zaidi kuliko ilivyotarajiwa na wengi.

Mwamko wa Chadema ulianza kushika kasi mara baada ya Slaa, kuteuliwa kugombea Urais, mwamko huo uliendelea hata baada ya uchaguzi, na hasa baada ya chama hicho kuamua kufanya siasa zake kwa njia ya maandamo mikoa ya Kanda ya Ziwa hadi Nyanda za Juu Kusini.

Wadadisi wa mambo ya kisiasa wameanza kuhoji ni wapi kasi hiyo imeyeyeka ghafla na kukipa nafasi tena CCM kuanza kutamba katika maeneo mbali mbali nchini.

Hali hiyo ya kuanza kudorora kwa Chadema imelezwa pia kukikumba chama cha CUF kupoteza mvuto.

Chadema inatakiwa ibadili sera zake na falsafa mpya za kuendelea kuwashawishi Watanzania.
 
Bado sana mkuu ritz kusema CDM imedorora! kuna mambo mengi yanatisha ndani ya serikali na hakuna dalili za kuyapatia dawa. Watanzania wengi wanataka mabadiliko, na mabadiliko hayaji kama mvua ila kwa mipango yenye akili.
 
uchunguzi wako ni kwa mujibu wa nini? au unasukumwa na unazi wa kupindukia ulionao juu ya CCM?
Mm sijaona huo mwamko watu walionao juu ya CCM!
 
Redet.., Rwekaza Mukandala au Benson Bana....!?

Hii ni hatari kama Tembo amefanana na sungura mpaka
wanasababisha mjadala mkubwa ndani ya jamii.
maana yake nini?....Sungura ataendelea kuwa mkubwa
na Tembo atadumaa.
 
Redet.., Rwekaza Mukandala au Benson Bana....!?

Mkuu Mkeshaji,
Huu ndio ukweli unajua kila siku unapiga kelele za ufisadi ufisadi, zimewachosha watanzania lazima Chadema kama chama ibuni falsafa mpya kutegemea kuhubiri ufisadi kama kete yake haitakisaidia Chadema huko tuendako.
 
uchunguzi wako ni kwa mujibu wa nini? au unasukumwa na unazi wa kupindukia ulionao juu ya CCM?
Mm sijaona huo mwamko watu walionao juu ya CCM!
mkuu usijali hawa magamba walishasema kuwa sisi ni chama cha msimu na hakuna siku waliyosema cdm kinatishia zaidi ya kujipa moyo tuu!
 
Gud analysis mkuu ritz.
Tatizo la mashabiki na wanachama wa CDM hawayaoni haya. Kila siku chama kinazidi kudorora, wanashindwa kwenye chaguzi ndogo mbali mbali kwa tofauti kubwa, lakini halion hili!
Kazi kuimba tu Slaa, Slaa, Slaaa..
 
uchunguzi wako ni kwa mujibu wa nini? au unasukumwa na unazi wa kupindukia ulionao juu ya CCM?
Mm sijaona huo mwamko watu walionao juu ya CCM!
CCM wamekuja na mbinu mpya ambazo JK ametoka nazo uingereza kwa DAVID CAMERON...

Si unajua juzi tu walikuwa pamoja Davos na jana wakawa wote kwa summit ya wasomali. Endeleeni kutamba na mbinu zenu za kikameruuuuuum muwapelekee wana Arumeru.
 
Wanabodi..
Mwenendo wa kisiasa, kati ya watani wa jadi CCM na Chedema sasa umeanza kuzua mijadala ndani ya jamii.

Wananchi wanahoji iko wapi kasi na upepo wa mabadiliko ilikuwa nao Chadema mwaka 2010 na mwaka jana ilikoyeyukia.

Huku CCM kilichokuwa kimeanza kudorora sasa kikionekana kupaa zaidi kuliko ilivyotarajiwa na wengi.

Mwamko wa Chadema ulianza kushika kasi mara baada ya Slaa, kuteuliwa kugombea Urais, mwamko huo uliendelea hata baada ya uchaguzi, na hasa baada ya chama hicho kuamua kufanya siasa zake kwa njia ya maandamo mikoa ya Kanda ya Ziwa hadi Nyanda za Juu Kusini.

Wadadisi wa mambo ya kisiasa wameanza kuhoji ni wapi kasi hiyo imeyeyeka ghafla na kukipa nafasi tena CCM kuanza kutamba katika maeneo mbali mbali nchini.

Hali hiyo ya kuanza kudorora kwa Chadema imelezwa pia kukikumba chama cha CUF kupoteza mvuto.

Chadema inatakiwa ibadili sera zake na falsafa mpya za kuendelea kuwashawishi Watanzania.

Haaahaa kumbe ijumaa imeshafika bwana. Na wadadisi wa mambo ya kibiashara nao wanasemaje? Maana sijawahi kuwaona hao wadadisi wa mambo ya kisiasa. Sijui wanapatikana wapi
 
Ilianza NCCR - Mageuzi ya Mrema wakati huo, Ikaja CUF na sasa CHADEMA. Vyote vinaibuka na kuzama CCM iko pale pale, upinzani wa kibongo bana!
 
kukipa nafasi tena CCM kuanza kutamba katika maeneo mbali mbali nchini.

.

Ungetuelezea hayo maeneo mbalimbali ni yapi? tunategemea hali za kimaisha ziwe bora,bei za bidhaa zishuke,gharama za nishati zishuke,uzalishaji viwandani upande ukienda sambamba na utengenezaji wa ajira mpya nyingi zaidi, miundombinu izidi kuimarika na sio kuhesabu km za lami ambazo hamsaidia mtanzania anayeishi bukyanagandi, CCM ingejisifia kama angalu imeweza kufanya hayo hata kwa aslimia 20 na sio takwimu za kupika...hata hivyo unajua Serikali sikivu iko kama matumizi makubwa kuliko mapato na unajua hili maana yake ni nini..!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom