William Mshumbusi
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 1,792
- 2,421
- Thread starter
-
- #61
William,
inawezekana umeandika kwa jazba au kishabiki tu au hata kwa kutojua, hiyo ndiyo siasa unaangali upenyo unaoweza kuwafanya wananchi wakuelewe na unasimamia hapo na kwa Chadema naona wanafanikiwa, kila likitokea tatizo wanawaeleza wananchi na wananchi wanauona ukweli, huwezi kuwaeleza wanachi maneno tu bila kuwapa mifano. Ufisadi wanona, ndio chanzo cha huduma duni za kijamii, wanafunzi kufeli ni kwa sababu ya uongozi bomu! na mambo mengine mengi!
Kuhusu waziri kujiuzuru huku ni kuwajibika na kwa mtu mwenye busara matokeo mabovu kabisa miaka mitatu mfululizo anaachia ngazi mwenyewe bila hata kusubiri, na hapa ndipo tungepata mahala pa kuanzia kutatua tatizo. waziri amekuwepo kwa muda sasa kwenye wizara hiyo na matokeo mabovu sana katika nchi hii yametokea kipindi chake hivyo hana mbinu za kutatua matatizo ingawa anayajua na dawa yake ni yeye kupisha mtu mwingine mwenye uwezo;
Pia nikukumbushe kwamba Chadema wanafanya uchunguzi na utafiti wa mambo mengi sana na ndio maana wanaibua uvundo mwingi sana serikalini na ndiyo sababu ya nyie kuichukia zaidi Chadema kuliko vyama vingine vyote; wanatafiti wanakuja na tafiti makini bungeni mnazizima! wakienda kuwaeleza wananchi wenye nchi yao mnatumia polisi kuwazima, sasa unataka watumie mbunu zipi!?
Tusiwe Majuha jamani nchi yetu nzuri inateketea chini ya utawala wa ccm na sisi tumekaa kimya tu tukiangalia! kisa mimi ninapata kila kitu sina tatizo! huu ni ubinafsi tu! mamilioni ya watanzania wanaishi kwa shida na taabu wakati nchi yao tajiri sana, nchi inashindwa kutoa huduma bora za kijamii kwa wananchi wake! tukataeni mambo haya ndugu zangu! msikubali kutumiwa na hawa wafujaji wa mali za umma! hivi umeshaona hawa watu wanavyofuja mali za nchi hii! na hapa hatuongelei hao waliojuu tu hata waliochini ni tatizo, 60% ya fedha za serikali zinatumiwa kwa mambo ya hovyo kabisa kwa sababu hakuna mfumo mzuri wa kusimamia fedha na hakuna uwajibikaji, kila kitu ni chini ya kiwango, hatuko makini kuhakikisha fedha yetu inafanya kazi kwa tija na kwa viwango! tunafanya mizaha tu! kila mtu anapiga dili tu! tutabaki nyuma sana!
TUSIWE WABINAFSI TUAMKE TUTETEE JIMII NZIMA YA WATANZANIA.
ujumbe mzuri Je unamfikiaje na mtu asiyejua Jamii folumu na asiyehudhuria mikutano ya hadhara akiamini siasa ni ulongo.
Mbinu duni za kujieneza hizi
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka 2010 mkoani Arusha � Arusha mjiniNdugu yangu hiki chama uwa hakikosolewi na chama cha Mitume.
Ndugu yangu hiki chama uwa hakikosolewi na chama cha Mitume.
William Mshumbusi,badala ya kuilaumu CHADEMA hebu jifikirie umeifanyia nini nchi yako kulingana na maelezo yako.Inawezekana hata kelele hupigi basi nafuu hata CHADEMA wanapiga kelele kumuamsha mwenye nyumba usingizini.
Unaweza ukadhani kelele zipigwazo na CHADEMA hazina msingi lakini isingekuwa kelele hizo basi hata wewe usingekasirika na kutoa ujumbe wako ili tuujadili.
Kwangu mimi upinzani unaweza ukajengwa na kuamua kwa dhati kabisa kwamba tupunguze nguvu ya serikali kwa kubana nafasi za wabunge nyingi ziende kwa upinzani ili ule ujinga wa serikali wa waliokubali wameshinda utakwisha na yote ya ubadhirifu wa mali ya umma utapungua sababu mhimili mmoja wa kuibana serikali utakuwa na nguvu.Lakini kwenye hili vyama vyote vinapigania vipate rais hatutafika kule tunakoenda.
Sisi sote watanzania( mimi,wewe na yule) bila kujali itikadi ya vyama tunajukumu la kuiwezesha nchi yetu kutowachagua wale wote tunaowaona hawafai kuwa viongozi kwa sababu za wizi wa mali ya umma,udini,uwongo,unyanyasaji.na mengineyo.
All in all, mbinu za kuneneza chama siyo effective. Viongozi wasikwepe jukumu kwa kusema eti 'kila mtanzania ajiulize kaifanyia nini nchi' vinginevyo hatuna haja ya kuwa na viongozi. Mikutano ya hadhara sawa ila siyo mwarobaini pekee wa kueneza chama.hapo kwenye red, upo sahihi, kila mtanzania na ajiulize hilo swali! tutapiga hatua badala ya porojo za kila siku!
Chukulia mfano: watu 20 mnamfukuza mwizi, mmoja wenu ana mbio na uwezo wa kumkamata yule mwizi lakin kila akikaribia kumkamata mwizi anapunguza mwendo badala yake anazidisha kelele mwizi, mwizi, mwizi...! Katika hali hiyo ni rahisi kuhisi kuwa huyo na anayemfukuza mwizi na yule mwizi mwenyewe lao moja!mmetuchosha sasa always cdm, cdm.vyama vya siasa vipo 20 na zaidi why cdm, cdm kila mda aaaahhhhhhhhh
kweli vyama uvielewi,una chama sawa,lakini na ww pia ujielewi,umepoteza dira ujui mbele ni wapi na nyuma ni wapi,nchi hii ina vyama zaidi ya 17 ila ww mbaya wako ni chadema tu?bahati mbaya ata hiyo tread yako aijakaa sawa ni vizuri nawe pia ufanye utafiti kabla ya kuleta pumba zako
Nchi hii imejaa mapoyoyo kweli kweli. Unakiambia chama ambacho kiliuza sera za ilani yake na kuporwa ushindi ndo kifanye utafiti ili Maccm wao wabaki wasafirisha meno ya tembo tu!!
Na wakati huo wote huja na jibu rahisi tu: Fulani ajiuzuru! Kana kwamba yeye ndiye kaja na mkosi huo.
chadema inapigia kelele matatizo yaliyoibuliwa tayari hivyo nahofia uwezo wake wa kufanya kazi kisayansi na uchunguzi.
Nataka wabaini vyanzo vya matatizo
Mtume mmoja tu ndie hataki kukosolewa, ukimkosea wafuasi wake watakushikisha adabu!!!
Wengine unawakosoa tu....labda ungesema..hakikosolewi kama mtume fulani!..