CHADEMA bado mko hivi kweli?

CHADEMA bado mko hivi kweli?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Bado mnaruhusu wagombea wa CCM,hadi leo hii,kupita bila kupingwa? Hadi leo hii mnaamini kuwa Makamanda wachache wa mikoani wanaweza kuwabadili wananchi bila nguvu ya pamoja? Bado mnaamini kuwa Nafasi za chini kama Wenyeviti wa Vijiji,Mitaa na Vitongoji na Madiwani hawana maana. Kimsingi,hao ndio wenye watu.CHADEMA, CCM is still strong. Strong shall be defeated by the stronger. Nafasi ya kupata mafanikio ni kubwa sasa kuliko wakati wowote mwingine. Hii ni kwakuwa,wananchi walio wengi sasa wanashiriki siasa za upinzani bila woga. CHADEMA, wakati ni huu! Badilikeni mtuoneshe siasa ya kweli ya ushindani Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mkuu usitoboe siri, chadema hawajui kuwa wenyeviti wa mtaa na vijiji ni watu wa muhimu sana, wewe waache kama walivyo na mawazo yao mgando.
 
cdm inalitambua hilo na ndiyo maana kuna mpango mkakati umefanyika wakuanzisha kanda ili madaraka yarudi chini kwa wananchi wanaoguswa na matatizo moja kwa moja,japo juhudi hizo zinakwamishwa na wakuu wa mikoa na wilaya kwa maagizo ya wakubwa zao.

viongozi wa juu wa cdm wanatambua changamoto zinazowakabiri wagombea wao,hasa wa vijiji na vitongoji pamoja na hayo kila eneo lenye uchaguzi cdm imeweka mgombea tofauti na kipindi cha nyuma hapakuwa na wagombea wengi katika maeneo husika<kama uchaguzi ungekuwa huru nadhani leo tungekuwa tuongea habari nyingine> kikubwa hatukatishwi tamaa na vitisho vya wale wanajifanya wako juu ya sheria na juhudi za cdm hazitakoma leo wala kesho,asante kwa ushauri wako
 
Mkuu ni kweli lakini CCM wana pesa ya kuwarubuni wagombea wa vyama vya upinzani. Ndiyo maana mtaji mkubwa wa CCM bado ni ujinga na umasikini.

Kwa nia njema SIKU NJEMA ZA MUNGU HAZIISHI hila kama hizi zitashindwa na dhamira nzuri ya ukweli na wema.
 
Kwa chadema sio mitaa na kata zote muhimu.

Zipi kata muhimu ambazo wanazipigania kwa nguvu zote.

Hizo nyingine hazina thamani kwao.

Hata kwenye Ubunge, wako wagombea wanaopewa pesa za kampeni na wengine wanachinjiwa baharini.

Au mmesahau story ya pesa zilizotoka Uingereza mwaka 2005 kuisaidia chadema kwenye uchaguzi?
 
Kama hatuta acha kuendekeza njaa zetu CCM watatusumbu...njia wanayo tumia ni fupi sana, 'penye udhia penyeza rupia"
Mfano kama mtoto wako anauwawa na polisi, kwa kuewa pesa kidogo tu unaanza kutetea ujinga!
 
Kuna aliyetaka kugombea kupitia CDM akakataliwa? Mbona mwenzetu hukwenda kusimama au kusimamisha mgombea. jukumu hili ni letu sote, sio Dr Slaa na Mbowe peke yake. Je wewe ni mfia chama?
 
Chadema wao wanataka kata za Arusha tu uko kwingine hawana haja napo walianza Mungu na wanamaliza na Mungu.
 
Kwa chadema sio mitaa na kata zote muhimu.

Zipi kata muhimu ambazo wanazipigania kwa nguvu zote.

Hizo nyingine hazina thamani kwao.

Hata kwenye Ubunge, wako wagombea wanaopewa pesa za kampeni na wengine wanachinjiwa baharini.

Au mmesahau story ya pesa zilizotoka Uingereza mwaka 2005 kuisaidia chadema kwenye uchaguzi?

Bavicha wanajipongeza wamepata 28% Iramba ni mafanikio kwao.
 
Wananikumbusha ile timu iliyokuwa inashangalia kwa kufungwa magoli matano TU. Timu hiyo ilizoea kufungwa 12 na kuendelea.

Hahahahahahahah Bavicha is a ridiculous entity...
 
Kuna aliyetaka kugombea kupitia CDM akakataliwa? Mbona mwenzetu hukwenda kusimama au kusimamisha mgombea. jukumu hili ni letu sote, sio Dr Slaa na Mbowe peke yake. Je wewe ni mfia chama?

Watu hawataki kuombea kwa tiketi ya chama ambacho madhumuni ya kuaznishwa kwake siyo mema.

Vijana waliolaghaika wasiojua kinachoendelea ndio mko mstari wa mbele kushabikia chama msichoelewa mipango yake ya ndani.
 
Bado mnaruhusu wagombea wa CCM,hadi leo hii,kupita bila kupingwa? Hadi leo hii mnaamini kuwa Makamanda wachache wa mikoani wanaweza kuwabadili wananchi bila nguvu ya pamoja? Bado mnaamini kuwa Nafasi za chini kama Wenyeviti wa Vijiji,Mitaa na Vitongoji na Madiwani hawana maana. Kimsingi,hao ndio wenye watu.CHADEMA, CCM is still strong. Strong shall be defeated by the stronger. Nafasi ya kupata mafanikio ni kubwa sasa kuliko wakati wowote mwingine. Hii ni kwakuwa,wananchi walio wengi sasa wanashiriki siasa za upinzani bila woga. CHADEMA, wakati ni huu! Badilikeni mtuoneshe siasa ya kweli ya ushindani Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Hakuna Chama cha Upinzani kinachoweza kuishinda CCM Tanzania 2015 ktka hali ya kawaida ya kupiga Kura, huo ni ukweli mchungu, na ninaweza kwenda mbali hata kama CCM wasiposimamisha mgombea na wakaweka kivuli bado watashinda tu, na anayebisha ni kwamba haelewi jinsi mfumo wa TZ ulivyo na unavyofanya kazi.

CCM ni wajanja sana walikubali tu kuingia Mfumo wa Vyama ili kuonekena kwa Wazungu kwamba kuna vyama vingi, lkn hawakubadilisha mfumo uliokuwepo, ambao ni wa Chama kimoja bado, ukweli tu kwamba Raisi wa Tanzania ni Raisi mpaka pale Raisi mwingine anapoapishwa unafaa kuelezea ugumu wa upinzani kuweza kushinda Uchaguzi, achilia mambo mengine meengi sana ambayo yamejificha!
 
cdm inalitambua hilo na ndiyo maana kuna mpango mkakati umefanyika wakuanzisha kanda ili madaraka yarudi chini kwa wananchi wanaoguswa na matatizo moja kwa moja,japo juhudi hizo zinakwamishwa na wakuu wa mikoa na wilaya kwa maagizo ya wakubwa zao.

viongozi wa juu wa cdm wanatambua changamoto zinazowakabiri wagombea wao,hasa wa vijiji na vitongoji pamoja na hayo kila eneo lenye uchaguzi cdm imeweka mgombea tofauti na kipindi cha nyuma hapakuwa na wagombea wengi katika maeneo husika<kama uchaguzi ungekuwa huru nadhani leo tungekuwa tuongea habari nyingine> kikubwa hatukatishwi tamaa na vitisho vya wale wanajifanya wako juu ya sheria na juhudi za cdm hazitakoma leo wala kesho,asante kwa ushauri wako

Tatizo ni kwamba hao wanaoenda kuwaomba kura hawawezi hata kutamka M4C au peoples power! Shida iko hapo! lakini wanawapa vipeperushi vilivyoandikwa M4C!
 
Watu hawataki kuombea kwa tiketi ya chama ambacho madhumuni ya kuaznishwa kwake siyo mema.

Vijana waliolaghaika wasiojua kinachoendelea ndio mko mstari wa mbele kushabikia chama msichoelewa mipango yake ya ndani.
Wewe ndio hujui kinachoendelea. Mimi sio kijana. Naelewa mipango ya ndani ya CDM. Unamsamea nani?
 
Ungekuwa unajua mipango ya ndani ya chadema ungemjua mmiliki wa nyumba iliyopangishwa na chadema pale Kinondoni. Vilevile ungejua tenda ya magari hya M4C amepewa nani na kwa vigezo gani. Halafu ungefahamu mikutano ya chadema inafanyika kweye hoteli za nani na kwa bill ya shilingi ngapi.

Vilevile ungeona aibu kuja jamvini kuitetea chadema kila kukicha. Umeona Mbowe anaitetea chadema hapa? Yeye ni member hapa lakini nafsi yake inamsuta. Nyinyi msiojua kinachoendelea ndio kutwa mko nyuma ya keyboard kutetea vitu msivyoelewa.
 
ZeMarcopolo wewe siyo chadema, huwezi ukajua huwa tunapanga nini kwenye mikutano yetu ya ndani! Tuna mikakati ya kuchukua dola hilo halina ubishi!
 
Last edited by a moderator:
Tuna mikakati tumejipanga kwenda chini kwa wananchi, lakini msisahau jambo moja muhimu mnapolinganisha uwezo wa vyama, CHADEMA kinategemea ruzuku na michango ya wanachama kujijenga, lakini tunazitumia ipasavyo kujiimarisha na tuna imani mpaka uchaguzi wa 2014 hakutakuwa na kitongoji, kijiji wala mtaa ambao hatutasimamisha wagombea wa chadema. pamoja na hila nyingi za CCM na ujinga ambao bado upo vijijini chadema imeendelea kusimamisha wagombea katika ngazi mbalimbali za uchaguzi na tunashinda na nyingene tunashindwa hii ni dalili nzuri ya kukua kwa chama chetu.
 
ZeMarcopolo wewe siyo chadema, huwezi ukajua huwa tunapanga nini kwenye mikutano yetu ya ndani! Tuna mikakati ya kuchukua dola hilo halina ubishi!

Hahahahahahahaha sawa mkuu.

Zingatieni njia za amani tu.

Tatizo lenu mnajiandaa kuchukua dola bala ya kujifunza kwanza njia za kuiomba dola toka kwa wenye dola.

Tuendelee kuwa pamoja...
 
Back
Top Bottom