Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Ingawa wakubwa wetu waliamua kukusaliti kwa tamaa zao, ukweli ni kwamba pengo Lako wameshindwa kujaza mpaka sasa. Cha Ajabu sasa ni kwamba hakuna utaratibu unaoeleweka wa kuzungumzia mambo ya Chama. Chama kinaongozwa na matamko ya Viongozi hasa Yule uliyetuasa tusimpokee. Bungeni tunaendelea na ule utoto wa kuzomea na kupiga kelele Kama walevi na sasa hatuna tena hoja za msingi za kuibana Serikali! Hakika tuna hali mbaya hasa Baada ya kuikana Sera yetu ya kupinga Ufisadi na kutetea Rasilimali za Umma. Tunaona aibu kukuomba msamaha maana tulikukashifu kwa majina ya kipuuzi tukijawa kiburi kwa kuaminishwa kwamba uliyemkataa atatupeleka IKULU saa 2 asubuhi tarehe 25 Oktoba, 2015 lakini haikuwa hivyo. Hakika Wafiachama hatutakusau Kamwe