CHADEMA Arusha yasusia Mkutano wa upatanishi

CHADEMA Arusha yasusia Mkutano wa upatanishi

Lema na lissu wanakwenda tabora kesho

Lema akitua Tabora halafu akachafua hali hewa hakika Zitto alivyo na wadudu wengi wa malaria lazima atakwenda India
 
Maridhiano yafanyike baada ya watuhumiwa wa bomu la Soweto kukamatwa na kufikishwa mahakamani na hasa Mwigulu Nchemba. Viva CDM!!!!!!
 
Chadema hawataki maridhiano ya amani!!![/QUOTE
sidhani kama ni kweli kwamba chadema hawataki maridhiano ya amani, tatizo ni jinsi maridhiano haya yanavyokwenda kisanii, huwezi kuitisha maridhiano wakati hujatafuta suluhu ya chanzo kilichopelekea kuvunjika kwa hiyo amani, mimi siyo mwanasiasa but kwa hili, chadema nawaunga mkono kwa asilimia zote
 
Movie ya Soweto bado edit inaendelea?

Tulisema Rais aunde tume kimahakama (judicial commission of inquiry), Kikwete anaogopa nini kuunda tume kama serikali yake haihusiki na mlipuko wa bomu?
 
Wamemtafuta Pia Balozi wa Vatican na Papa kumwambia kuwa wanataka maridhiano bila kukubali hadharani kuwa walipiga Bomu.
 
Peopleeezz!!!!Hewaaaaaa!!!!!
Hiki ndo chama ninachokiamini, chama kina machale ajabu, eti wanataka kukiingiza chaka eee? Siyo chadema!

Wakuu,
Ni kwamba chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA imeshtukia mchezo ulio/unaotaka kuchezwa na Serikali ya CCM kuwaingiza kwenye maridhiano ya amani yasiyo na tija kwa umma na taifa.

Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mutungi aliandika barua kuhusu maridhiano ya amani kati ya vyama vya siasa, polisi, na taasisi za kidini pamoja na wananchi wa Arusha.
Chadema kama chama cha siasa na kama taasisi inayoitumikia jamii kinatambua nia njema kabisa ya Jaji Mutungi, na inamuunga mkono kufanya maridhiano haya yanayogusa jamii.
Hata hivyo nia hii njema ya jaji Mutungi imetiwa doa tena mbaya kabisa na serikali ya ccm na jeshi la polisi. Tukianzia na Jeshi la polisi ambalo ni sehemu ya maridhiano ya amani, jana walifanya uchunguzi wa tukio la kuchomwa moto ofisi yaa chadema mkoa wa Arusha, within a second kabla hata hawajamaliza uchunguzi wakaitisha mkutano na waandishi wa habari, wakatoa taarifa za uchunguzi ambayo ilionekana iko shallow sana, taarifa iliyoonyesha udaifu na kuidhalilisha jeshi la polisi. Kwa taarifa ambayo jeshi la polisi imetoa leo inaonyesha chadema wameichoma ofisi yao wenyewe, yaani mchezo ule ule wa kusema chadema walijilipua wenyewe Soweto, Kijana Ally Zona(RIP) aliuawa na kitu chenye ncha kali, Daudi Mwangosi (RIP) alirushiwa kitu chenye ncha kali na upuuzi mwingi kadha wa kadha!!
Serikali dhaifu ya ccm kwa upande wake ilitegemea maridhiano/mapatano ya Jumamosi yawe sehemu ya chadema kumtambua meya Gaudence Lyimo, meya ambaye alichaguliwa kwa njia ya hila, meya ambaye ndiye chanzo cha mauaji ya January 5 2011, meya ambaye ni chanzo cha kufukuzwa kwa madiwani wetu Arusha, meya ambaye ni chanzo cha mlipuko wa bomu soweto, eti chadema tukae meza moja na ccm!!!!

Nia na dhamira ya CHADEMA ni kila mtanzania kuwa na amani, lakini amani haiji bila kuwa na haki, kwani CHADEMA inatambua kuwa Amani ni tunda la haki, na kwamba CHADEMA itaendelea kupigania haki ya watanzania wote wakati wote ili wawe na amani.

Hata hivyo kwa taarifa nilizopata ni kwamba chadema itaandika barua kwa taasisi zote za dini na za kiraia kuelezea sababu za msingi za kususia mkutano wa Msajili unaohusu upatanishi baada ya kutiwa doa na serikali ya ccm.

CHADEMA inatamka kwamba kabla ya wao kukutanishwa na ccm mambo yafuatayo yafanywe:
1. Meya feki ajiuzulu ili uchaguzi wa haki ufanyike,
2. Serikali iwawajibishe wale wote waliolipua bomu na kupiga risasi za moto soweto Arusha,
3. Serikali itueleze mabomu yaliyotumika soweto yalitoka wapi na yaliingia vipi nchini, na kwa makusudi gani, nani aliingiza, na hatua gani anatakiwa kuchukuliwa.
4. Serikali iwachukulie hatua polisi wote waliowaua raia kwenye mauaji ya Jan 5 2011
5. Serikali iwashushe vyeo polisi wote waliopandoishwa vyeo baada ya kutekeleza mauaji ya raia ya january 5, mauaji ya Daudi Mwangosi na mauaji ya kijana Ally Zona aliyeuawa Morogoro na maeneo mengine ambayo polisi wametekeleza mauaji ya raia wasio na hatia, halafu wapelekwe mahakamani.

Baada ya hapo CHADEMA watakuwa tayari kukaa meza moja na ccm.

Kwa habari zaidi CHADEMA Arusha watazungumza na waandishi wa habari kuelezea zaidi
Kwa hill namuunga mkono mbunge na wananchi wake kwa msimamo wao Tanzania yote ingekuwa kama Arusha magamba wange kuwa wameisha.na hii ni salamu kwa mutungi kujua jinsi police wanavyo Fanya kazi kiccm.mbunge Lema hongera sana kwa hili umekuwa kisiasa.maana nidhamu ya woga hafai maana kwa nje ni jambo zuri lakini kuna siri kubwa imejificha.
 
Hii serikl xakijinga san sasa kama ni cdm wamelipua si wawakamate nakuwatia hatian au wenyewe hawtakiwa kutiwa nguvun
 
Hivi Mungi we si msemaji wa chadema arusha?

Hivi kama primary investigation inaonesha kuna dalili za nyie wenyewe kuhusika mlitaka wasiseme?

Hivi.mbona kwenye updates za mkutano boss wenu lema alisema mtakwenda?

Kwanini mkatae maridhiano ya amani? Hivi chadema mnataka vita?

Hivi kwanini chadema arusha mnajaribu kuvuruga amani ya nchi?
Hivi kwanini chadema arusha mmekuwa wasemaji wa chadema taifa?

Hakika kwa style hii hakuna mwananchi mwenye utinamu atawapa ridhaa ya kwenda ikulu.

Kwa hali ilivyo sasa ili nchi hidumu kwenye amani lazima chadema wakae mbali na ikulu.

Ni wazi chadema kama mgekuwa mnaongoza nchi mgewatupa wapinzani wenu mtoni.

Dr.W.Slaa kwanini chadema ina kataa amani?mnataka vita?
 
Last edited by a moderator:
tulisema rais aunde tume kimahakama (judicial commission of inquiry), kikwete anaogopa nini kuunda tume kama serikali yake haihusiki na mlipuko wa bomu?

wekeni basi huo mkanda tuuone maana tume haito undwa. Utembezeni kwenye mikutano kama mlivyo fanya kwenye picha za lema.
 
No war no way, kuwang'oa ccm sio kazi rahisi coz wana mizizi kama ya mnazi nchi nzima, but in god we trust utawala huu wa kifisadi utang'ooka tu ( kutokana na mpasuko ndani ya ccm kuelekea uchaguzi 2015 ), in dr.slaa i trust
 
kama kuipigania ccm ni sawa na kumpigania shetani , basi bila shaka maridhiano na haramia shetani haiwezekani .
 
Nani afanye upatanisho na Shetani? P.M. Mwenyewe kasema raia wapigwe, kama siyo unafiki ni nini?
 

mnajitekenya na kucheka wenyewe. susieni na pesa kutoka serikalini ili tujue hamtaki kuchangamana na serikali iliyopo madarakani. huku hamtaki maridhiano huku mnalilia posho; chadema kwa unafiki mko sawa.
 
Back
Top Bottom