Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Chama cha demokrasia na Maendeleo (chadema )wilaya ya Arusha,kimelalamikia mwenendo wa zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura kukosa mwitikio kutokana na wananchi kutohamasishwa vya kutosha
Chadema kimedai kuwa kipo tayari kutoa magari 20 katika jiji la Arusha ili yasaidie kuhamasisha watu kujiandikisha kwa kuwa msimamizi wa uchaguzi jijini hapa,Msena Binna ameshindwa kuhamasisha wananchi ipasavyo jambo ambalo wanahisi kuwepo kwa vitendo vya kukihujumu chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Katibu wa chadema wilaya ya Arusha ,Innocent Kisanyage ametoa kauli hiyo mapema leo katika ofisi ya mbunge wa Arusha mjini wakati akiongea na vyombo vya habari na kulalamikia mwenendo wa zoezi la uandikishaji pamoja na mawakala wao kuzuiwa kukagua daftari kabla ya kuanza kuandikisha.
Kisanyage akiyekuwa ameambatana na madiwani kadhaa wa chama hicho jijini hapa,amesema chama chake kimeandika barua ya malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi jijini hapa, lakini hadi sasa hawajapata majibu yoyote na wanafikiria hatua ya kuchukua.
Naye mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amekosoa hatua ya jeshi la polisi wilayani hapa kuzuia mkutano wake uliokuwa ufanyike Leo kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokez kujiandikisha daftari la mpiga kura katika uchaguzi mdogo wa serikali za mtaaa.
Amesema amefikia hatua ya kufanya mkutano huo katika jimbo lake baada ya kuona kwamba wananchi hawajitokezi vyakutosha kujiandikisha baada ya kukosa hamasa jambo ambalo anahisi huenda chama chake kikahujumiwa.
Amesema chadema ipo tiyari kutoa magari 20 na sh,6000 kwa ajili ya kusaidia kutoa hamasa kwa wananchi waweze kujitokeza kujiandikisha kwa muda huu uliobaki kabla ya zoezi hilo kufungwa Agosti 14 mwaka huu siku ya jumapili.
Akiongelea malalamiko hayo msimamizi wa uchaguzi jijini la Arusha,Msena Binna amesema kuwa kimsingi malalamiko yanayotolewa na chadema hayajamfikia ofisini kwake na suala la mawakala kuzuia kuona daftari la kuandikisha wakati wa kuanza uandikishaji alidai mawakala wao wanachelewa kufika kwenye vituo.
"Mimi sijapata barua ya malalamiko ya chadema na kama yapo waje ofisini na suala la mawakala kuzuiwa kuangalia daftari ni kwamba wanachelewa kufika na kukuta zoezi linaendelea na wakishaanza kuandikisha mawakala hawaruhusiwi kukagua daftari" Amesema Binna.
Ends......