Chadema Arusha yashtukia mchezo mchafu kukihujumu daftari la kura

jembejembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Messages
398
Points
1,000

jembejembe

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2016
398 1,000
Chama cha demokrasia na Maendeleo (chadema )wilaya ya Arusha,kimelalamikia mwenendo wa zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura kukosa mwitikio kutokana na wananchi kutohamasishwa vya kutosha

Chadema kimedai kuwa kipo tayari kutoa magari 20 katika jiji la Arusha ili yasaidie kuhamasisha watu kujiandikisha kwa kuwa msimamizi wa uchaguzi jijini hapa,Msena Binna ameshindwa kuhamasisha wananchi ipasavyo jambo ambalo wanahisi kuwepo kwa vitendo vya kukihujumu chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Katibu wa chadema wilaya ya Arusha ,Innocent Kisanyage ametoa kauli hiyo mapema leo katika ofisi ya mbunge wa Arusha mjini wakati akiongea na vyombo vya habari na kulalamikia mwenendo wa zoezi la uandikishaji pamoja na mawakala wao kuzuiwa kukagua daftari kabla ya kuanza kuandikisha.

Kisanyage akiyekuwa ameambatana na madiwani kadhaa wa chama hicho jijini hapa,amesema chama chake kimeandika barua ya malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi jijini hapa, lakini hadi sasa hawajapata majibu yoyote na wanafikiria hatua ya kuchukua.

Naye mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amekosoa hatua ya jeshi la polisi wilayani hapa kuzuia mkutano wake uliokuwa ufanyike Leo kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokez kujiandikisha daftari la mpiga kura katika uchaguzi mdogo wa serikali za mtaaa.

Amesema amefikia hatua ya kufanya mkutano huo katika jimbo lake baada ya kuona kwamba wananchi hawajitokezi vyakutosha kujiandikisha baada ya kukosa hamasa jambo ambalo anahisi huenda chama chake kikahujumiwa.

Amesema chadema ipo tiyari kutoa magari 20 na sh,6000 kwa ajili ya kusaidia kutoa hamasa kwa wananchi waweze kujitokeza kujiandikisha kwa muda huu uliobaki kabla ya zoezi hilo kufungwa Agosti 14 mwaka huu siku ya jumapili.

Akiongelea malalamiko hayo msimamizi wa uchaguzi jijini la Arusha,Msena Binna amesema kuwa kimsingi malalamiko yanayotolewa na chadema hayajamfikia ofisini kwake na suala la mawakala kuzuia kuona daftari la kuandikisha wakati wa kuanza uandikishaji alidai mawakala wao wanachelewa kufika kwenye vituo.

"Mimi sijapata barua ya malalamiko ya chadema na kama yapo waje ofisini na suala la mawakala kuzuiwa kuangalia daftari ni kwamba wanachelewa kufika na kukuta zoezi linaendelea na wakishaanza kuandikisha mawakala hawaruhusiwi kukagua daftari" Amesema Binna.Ends......IMG_20191010_103005.jpeg
IMG_20191010_101959.jpeg
 

Kaizer0104

Member
Joined
Jul 26, 2018
Messages
80
Points
150

Kaizer0104

Member
Joined Jul 26, 2018
80 150
Je wewe unataka wawe na options gani zaidi ya kulalamika?
[/QUOTE/]
Stratejia ya siasa ina njia mbili;
1.Kuionyesha jamii kuwa una nguvu(aura) ya kutawala/kuamua jambo fulani kwa vitendo, Hii ndio mbinu kuu katika siasa(and it last very long), mara nyingi jamii inavutiwa na mtu anayejinasibisha kuwa na nguvu hasa hasa kwa njia ya ushawishi na kutumia mtaji wa kisiasa kulazimisha maamuzi fulani.Hili upinzani hawana, mara nyingi movements zao huishia hewani (no impact).

2.Kujihurumisha (seeking public sympathy) hapa walifanikiwa sana 2015 kwa kutuaminisha mzee Edo alionewa pale lumumba, baada ya hapo hii mbinu imefeli vibaya, (Note: public sympath can't last long) inabidi warudi kwenye mbinu #1.
 

Uwazitu

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Messages
489
Points
500

Uwazitu

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2019
489 500
Kwanini daftari la wapiga kura na vitambulisho vya mpiga kura vya Tume ya Uchaguzi visitumike katika uchaguzi wa serikali za mitaa?

Kwanini Tume ya Uchaguzi isifanyie marekebisho ( uhakiki ) daftari la wapiga kura ikiwa ni pamoja na kuingiza kwenye orodha wale wote waliotimiza umri na vigezo vya kuwa wapiga kura, Kama sheria inavyotaka?

Je, baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Tume ya Uchaguzi nayo itaanza zoezi la kuandikisha wapiga kura?

Fedha na nguvu zinazotumika sasa kwanini zisifanye kazi kwa daftari la uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020?

MAMA SAMIA, UMEJIANDIKISHA, NI SAWA,

JE, NI SAHIHI KUGHARAMIA KITU KIMOJA MARA MBILI?

AU KUNA MPANGO WA KUPIGA HELA KWENYE ZOEZI KUANDIKISHA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU?

HUU SIYO UFISADI NA WIZI WA FEDHA ZA UMMA?

KUNAJAMBO GANI LILILOFICHIKA?

Ufafanuzi tafadhali juu ya zoezi hili.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
18,724
Points
2,000

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
18,724 2,000
Lema anajiliwaza tu nimetoka ziara ya Arusha na Moshi chadema wengi hawana mpango wa kupiga kura sio uchaguzi huu tu Bali hata uchaguzi mkuu ujao.Arusha chadema ndio kabisa wengi hawataki na kuhama Lowasa Kutoka chadema kurudi CCM ndio kabisa chadema wengi Arusha hawataki kujiandikisha Wala kupiga kura.Imewachefua haswa.

Ila Lema sababu Ni mdau wa kula ruzuku ya Chadema na Mbowe wake namwelewa anachoongea hayo magari watakayosambaza na pesa Ni Lengo la kukwapua pesa za ruzuku kea kisingizio Cha uhamasishaji.Chadema chungeni ruzuku yenu hasa kipindi hiki .
 

Uwazitu

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Messages
489
Points
500

Uwazitu

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2019
489 500
Hawa CHADEMA nao sasa, yani huo mchezo ni Arusha tu?! Huko kwingine nani anaangalia?!
Majaliwa alifichua madudu ya morogoro, alipoenda iramba akayakuta mengine.

rais naye akayakuta katavi na rukwa.

Lema kasemea ya Arusha, Msigwa atasema ya Iringa, Silinde atasema ya Momba (a.k.a Kamwambie Mmeo, Diwani na Mbunge wako) , Selasini atasema ya Rombo, ya Mlimba yatasemwa Kiwanga na ya Kilombero yatasemwa na Lijualikali, Madiwani nao watasema na Wenyeviti wa Mitaa nao watasema.
 

Forum statistics

Threads 1,343,334
Members 515,022
Posts 32,781,073
Top